Kisa cha al Noor Kassum na Ally Sykes 1957

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,887
30,233
KISA CHA AL NOOR KASSUM NA ALLY SYKES 1957

Leo asubuhi tarehe 19 November, 2021 nimeona taarifa ya kifo cha Al Noor Kassum.
Al Noor Kassum ametumikia Tanzania katika nyadhifa nyingi tofauti.

Nimekutana na Al Noor Kassum wakati naandika maisha ya Ally Sykes, '''Under The Shadow of British Colonialism: The Life of Ally Sykes.''

Ally Sykes alinifahamisha kuwa ilikuwa mwaka wa 1955 tayari wameshaunda TANU na Julius Nyerere amekwenda UNO na kurudi.

Hali ya siasa katika majimbo ilikuwa inachemka lakini yeye alikiona cha mtema kuni kwani serikali ilimhamisha Dar es Salaam kwenda Korogwe kama adhabu kwa kuwa mmoja wa waasisi wa TANU akiwa na kadi no. 2 ya chama hicho.

Ally Sykes alipokuwa Korogwe Waingereza hawakumuacha waliendelea kumsakama kwani walijua hata huko Korogwe alikuwa anaendelea na shughuli yake ya kuifitini serikali kwa wananchi.

Iko siku wakamvamia nyumbani kwake kufanya upekuzi lakini jana yake rafiki yake jina lake Alphone Akena aliyekuwa katika jeshi la polisi alimtahadharisha kuwa atakuja kupekuliwa kwa hiyo achukue tajadhari.

Siku ya pili Ally Sykes alivamiwa nyumbani kwake lakini hawakukuta kitu.
Haukupita muda akahamishiwa Moshi.

Moshi mpango madhubuti ulikuwa umesukwa wa kumtia hatiani, kumfedhehesha na kisha wamfunge.

Joseph Kimalando alihudhuria mkutano wa mwaka wa 1954 wa kuunda TANU kama mjumbe kutoka Northern Province yeye na Japhet Kirilo.

Kimalando akawa anajizungusha kufungua tawi la TANU Moshi mjini na hii ikasababisha mgongano kati yake na Yusuf Olotu ambae alikuwa anataka kufungua tawi.

Ally Sykes toka akiwa ofisi ya TANU, New Street Dar es Salaam kabla ya uhamisho alikuwa anamtia hima Yusuf Olotu na wenzake wafungue tawi bila ya Kimalando.

Hii ikasababisha uhasama baina ya Ally Sykes na Joseph Kimalando.
Mwaka wa 1957 Ally Sykes akahamishwa kutoka Korogwe kwenda Moshi.

Mtego ulikkuwa umeshategwa huko Moshi unasubiri kufyatuliwa.

Mwanamke wa Kimarekani Maida Springer kiongozi wa wafanyakazi weusi Marekani alitembelea Tanganyika mwaka wa 1957 na akaenda Zanzibar akiongozana na Nyerere na Zuberi Mtemvu kisha wakaja Moshi.

Ally Sykes akatayarisha mkutano Machame Girls School na katika watu ambao aliwashawishi kukuhudhuria mkutano ule wHamza Aziz na Iddi Mwajasho ambao walikuwa kwenye kozi Police Trainng School (PTS) pale Moshi.

Nyerere na Bi. Maida walizungumza kwenye mkutano ule.
Vitu viwili viliudhi serikali.

Kwanza Nyerere kufika Moshi na pili mkutano wake Machame Girls School na kuhudhuriwa na vijana maofisa wa polisi - Hamza Aziz na Iddi Mwajasho.

Waingereza wakaona sasa wakati umefika wa kufyatua mtego wao.

Siku moja Ally Sykes yuko ofisini akaingia Afisa Mzungu ofisini kwake kaongozana na Police Inspector Mwafrika wakamkamata kwa kosa la kupokea rushwa.

Hapakuwa na ushahidi.
Ally Sykes akasimamishwa kazi na akapelekwa mahakamani.

Mama yake Ally Sykes Bi. Mruguru bint Mussa na Abdul Sykes haraka sana wakaenda kwa Al Noor Kassum wakati ule kijana mdogo ndiyo kwanza katoka masomoni Uingereza na ana ofisi yake mjini, wakaenda kwake aende Moshi akamtetee Ally Sykes.

Siku ya kesi asubuhi Al Noor Kassum akaingia Moshi akitokea Dar es Salaam na ndege ya East African Airways iana ya Dakota, kaja kumtetea mteja wake Ally Sykes.

Baba zao wakili Kassum na mteja wake Ally Sykes walikuwa wakifahamiana kwa miaka mingi na kuna wakati walikuwa pamoja katika Dar es Salaam Chamber of Commerce.

Yule Afisa wa Polisi Muingereza na yule Inspector Mwafrika hawakutokea mahakamani lakini Hakimu akaamuru kesi iendelee bila ya wao kuwepo.

Al Noor Kassum alikataa akasisitiza kuwa kwa kuwa hao ndiyo waliomkamata mtuhumiwa ni lazima wawepo mahakamni awahoji.

Upande wa serikali haukuwa na hamu kabisa ya kumleta yule Mzungu na askari wake Mwafrika kuhojiwa mahakamani na hapo ndipo ukawa mwisho wa kesi.

Mwindaji aliposikia mtego umefyatuka alidhani mtego wake umenasa paa kuja kuangalia anamkuta chui.

Mwindaji akarudi kinyumenyume kuelekea nyumbani kwake kwani mwindaji yeyote mwenye akili timamu hawezi kwenda kutegua mtego ulionasa chui.

Fitna hii yote walipanga Waingereza wakishirikiana na Joseph Kimalando.

Mara kwa mara Ally Sykes akiniambia kuwa Al Noor Kassum alikuwa akisikilizwa sana na Aga Khan na Mwalimu Nyerere.

Al Noor Kassum wakati Bi. Titi yuko kifungoni na viongozi wengi wakimnyanyapaa Bi. Titi yeye alikuwa akimpelekea vitu jela vya kumsidia katika ile hali ngumu ya ufungwa.

Na alipotoka wakati hali ya Bi. Titi ni ngumu baada ya kutoka kifungoni, Al Noor Kassum alikuwa akimnyooshea mkono Bi. Titi kumpunguzia shida zake za maisha.

Screenshot_20211119-223617_Facebook.jpg
 
View attachment 2016733
Tatizo udini ndio umemjaa mtoa mada.
 
Vipi Babu,za siku....vipi huyu Kassum na familia yake hawa hawakubaguliwa kiudini na Mwalimu Nyerere!?
 
Lombo,
Napenda nifanye sahihisho dogo.

Ukiwa unapendezewa kuniadhimisha kwa umri wangu itapendeza na kwa hakika ni sawa ukaniita baba.

Sababu ni kuwa kwa umri wangu wa miaka 69 wewe huwezi kuwa mjukuu wangu ila ni mwanangu.

Nakuambia haya kwa kuwa kwa mila zetu wewe ukiwa mjukuu wangu hapa utaweza kunitania upendayo.

Wajukuu zangu wote ni chini ya miaka 7 kwa hiyo hawa wajukuu zangu wewe ni sawa na baba yao ikiwa ni mwanamme la ni mwanamke wewe ni mama yao.

Itachekesha kama hawa wajukuu zangu siku ukija kunitembelea nyumbani wakakuita babu.
 
KISA CHA AL NOOR KASSUM NA ALLY SYKES 1957

Leo asubuhi tarehe 19 November, 2021 nimeona taarifa ya kifo cha Al Noor Kassum.
Al Noor Kassum ametumikia Tanzania katika nyadhifa nyingi tofauti.

Nimekutana na Al Noor Kassum wakati naandika maisha ya Ally Sykes, '''Under The Shadow of British Colonialism: The Life of Ally Sykes.''

Ally Sykes alinifahamisha kuwa ilikuwa mwaka wa 1955 tayari wameshaunda TANU na Julius Nyerere amekwenda UNO na kurudi.

Hali ya siasa katika majimbo ilikuwa inachemka lakini yeye alikiona cha mtema kuni kwani serikali ilimhamisha Dar es Salaam kwenda Korogwe kama adhabu kwa kuwa mmoja wa waasisi wa TANU akiwa na kadi no. 2 ya chama hicho.

Ally Sykes alipokuwa Korogwe Waingereza hawakumuacha waliendelea kumsakama kwani walijua hata huko Korogwe alikuwa anaendelea na shughuli yake ya kuifitini serikali kwa wananchi.

Iko siku wakamvamia nyumbani kwake kufanya upekuzi lakini jana yake rafiki yake jina lake Alphone Akena aliyekuwa katika jeshi la polisi alimtahadharisha kuwa atakuja kupekuliwa kwa hiyo achukue tajadhari.

Siku ya pili Ally Sykes alivamiwa nyumbani kwake lakini hawakukuta kitu.
Haukupita muda akahamishiwa Moshi.

Moshi mpango madhubuti ulikuwa umesukwa wa kumtia hatiani, kumfedhehesha na kisha wamfunge.

Joseph Kimalando alihudhuria mkutano wa mwaka wa 1954 wa kuunda TANU kama mjumbe kutoka Northern Province yeye na Japhet Kirilo.

Kimalando akawa anajizungusha kufungua tawi la TANU Moshi mjini na hii ikasababisha mgongano kati yake na Yusuf Olotu ambae alikuwa anataka kufungua tawi.

Ally Sykes toka akiwa ofisi ya TANU, New Street Dar es Salaam kabla ya uhamisho alikuwa anamtia hima Yusuf Olotu na wenzake wafungue tawi bila ya Kimalando.

Hii ikasababisha uhasama baina ya Ally Sykes na Joseph Kimalando.
Mwaka wa 1957 Ally Sykes akahamishwa kutoka Korogwe kwenda Moshi.

Mtego ulikkuwa umeshategwa huko Moshi unasubiri kufyatuliwa.

Mwanamke wa Kimarekani Maida Springer kiongozi wa wafanyakazi weusi Marekani alitembelea Tanganyika mwaka wa 1957 na akaenda Zanzibar akiongozana na Nyerere na Zuberi Mtemvu kisha wakaja Moshi.

Ally Sykes akatayarisha mkutano Machame Girls School na katika watu ambao aliwashawishi kukuhudhuria mkutano ule wHamza Aziz na Iddi Mwajasho ambao walikuwa kwenye kozi Police Trainng School (PTS) pale Moshi.

Nyerere na Bi. Maida walizungumza kwenye mkutano ule.
Vitu viwili viliudhi serikali.

Kwanza Nyerere kufika Moshi na pili mkutano wake Machame Girls School na kuhudhuriwa na vijana maofisa wa polisi - Hamza Aziz na Iddi Mwajasho.

Waingereza wakaona sasa wakati umefika wa kufyatua mtego wao.

Siku moja Ally Sykes yuko ofisini akaingia Afisa Mzungu ofisini kwake kaongozana na Police Inspector Mwafrika wakamkamata kwa kosa la kupokea rushwa.

Hapakuwa na ushahidi.
Ally Sykes akasimamishwa kazi na akapelekwa mahakamani.

Mama yake Ally Sykes Bi. Mruguru bint Mussa na Abdul Sykes haraka sana wakaenda kwa Al Noor Kassum wakati ule kijana mdogo ndiyo kwanza katoka masomoni Uingereza na ana ofisi yake mjini, wakaenda kwake aende Moshi akamtetee Ally Sykes.

Siku ya kesi asubuhi Al Noor Kassum akaingia Moshi akitokea Dar es Salaam na ndege ya East African Airways iana ya Dakota, kaja kumtetea mteja wake Ally Sykes.

Baba zao wakili Kassum na mteja wake Ally Sykes walikuwa wakifahamiana kwa miaka mingi na kuna wakati walikuwa pamoja katika Dar es Salaam Chamber of Commerce.

Yule Afisa wa Polisi Muingereza na yule Inspector Mwafrika hawakutokea mahakamani lakini Hakimu akaamuru kesi iendelee bila ya wao kuwepo.

Al Noor Kassum alikataa akasisitiza kuwa kwa kuwa hao ndiyo waliomkamata mtuhumiwa ni lazima wawepo mahakamni awahoji.

Upande wa serikali haukuwa na hamu kabisa ya kumleta yule Mzungu na askari wake Mwafrika kuhojiwa mahakamani na hapo ndipo ukawa mwisho wa kesi.

Mwindaji aliposikia mtego umefyatuka alidhani mtego wake umenasa paa kuja kuangalia anamkuta chui.

Mwindaji akarudi kinyumenyume kuelekea nyumbani kwake kwani mwindaji yeyote mwenye akili timamu hawezi kwenda kutegua mtego ulionasa chui.

Fitna hii yote walipanga Waingereza wakishirikiana na Joseph Kimalando.

Mara kwa mara Ally Sykes akiniambia kuwa Al Noor Kassum alikuwa akisikilizwa sana na Aga Khan na Mwalimu Nyerere.

Al Noor Kassum wakati Bi. Titi yuko kifungoni na viongozi wengi wakimnyanyapaa Bi. Titi yeye alikuwa akimpelekea vitu jela vya kumsidia katika ile hali ngumu ya ufungwa.

Na alipotoka wakati hali ya Bi. Titi ni ngumu baada ya kutoka kifungoni, Al Noor Kassum alikuwa akimnyooshea mkono Bi. Titi kumpunguzia shida zake za maisha.

View attachment 2016733
wewe Mohamed Said unatakiwa kuokoka, umpe Bwana Yesu Maisha yako ili uepuke jehanum ya moto wa milele. ushauri tu.
 
Back
Top Bottom