Kisa cha ajabu; Mtoto azaliwa bila ubongo!

DATAZ

JF-Expert Member
May 25, 2012
2,445
5,968
Mkazi wa Kijiji cha Mlowo mkoani Songwe, Loveness Kweka (25), amejifungua mtoto wa kiume asiye na ubongo na mfupa wa juu wa kichwa. Mtoto huyo amezaliwa wiki iliyopita katika Hospitali Teule ya Mkoa wa Songwe mjini Vwawa.

Akizungumza na HabariLEO kwa simu, Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo, Dk Lukombodzo Lulandala alisema mtoto huyo alizaliwa akiwa hai na uzito wa kilogramu 2.5.

Dk Lulandala alisema mtoto huyo ni wa pili kwa Loveness na alijifungua kwa njia ya kawaida baada ya ujauzito kukamilisha miezi tisa.

“Mtoto licha ya hitilafu hizo alizo nazo za uumbaji, amezaliwa kwa njia ya kawaida akiwa hai akiwa na uzito wa kilo 2.5... Mtoto na mama yake waliendelea kuwa chini ya uangalizi wa wauguzi kwa zaidi ya saa 23 tangu alipozaliwa, lakini ndugu wa mwanamke wakisisitiza wamchukue wakamlee nyumbani…”

“Nilipowahoji walionesha hisia zao za kumtompenda mtoto walimchukua akiwa hai ila kwa sasa sina taarifa zake kama yuko hai au la,” alisema. Dk Lulandala alisema baada ya mimba kutungwa siku nane za mwanzo hitilafu za uumbaji zinaweza kujitokeza na kusababisha mtoto azaliwe akiwa hana ubongo au mgongo wazi hivyo hitilafu za uumbaji zisihusishwe na imani za kishirikina.

“Akiwa tumboni pamoja na hitilafu za uumbaji mtoto ataendelea kuishi bila matatizo kwa sababu kila kitu anategemea kupata kutoka kwa mama yake tumboni,” alisema.

Alitahadharisha kuwa mimba katika miezi mitatu ya mwanzo matumizi ya dawa bila ushauri wa daktari si salama kwa wajawazito.

Kwa mujibu wa Dk Lulandala, wanawake walio kwenye hatari ya kujifungua watoto wenye hitilafu za uumbaji ni pamoja na wanaosumbuliwa na magonjwa ya kisukari na wenye uzito mkubwa. Alishauri wanawake wanapokuwa wajawazito wahudhurie kliniki kwa uchunguzi wa kitabibu na ushauri badala ya kunywa miti shamba.

Dk Lulandala alisema, tatizo la watoto kuzaliwa bila ubongo na mfupa wa juu ya kichwa lipo kidunia na kwamba, kati ya vizazi 10,000 watoto 400 wanazaliwa wakiwa na hitilafu za uumbaji.

Alisema utafiti uliofanywa mwaka 2012/2013 ulionesha kuwa watoto 28 walizaliwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili wakiwa na hitilafu za uumbaji.

Chanzo: Habari Leo
 
Genetic iligoma kujiumba kwa mfumo unaotambulika!! mambo haya hutokea tangu enzi za mababu - miaka ya kale walisema ni nuksi katika ukoo kwa hivyo viumbe wa namna hii waliwamaliza ili kuifuta nuksi hiyo.

Ila kwa sasa wazazi huamua kuwatunza sababu waamini ni Muumba ndiye aliyepanga kuwa hivyo na ndiyo zawadi yao waliyopewa.
 
MKAZI wa Kijiji cha Mlowo mkoani Songwe, Loveness Kweka (25), amejifungua mtoto wa kiume asiye na ubongo na mfupa wa juu wa kichwa. Mtoto huyo amezaliwa wiki iliyopita katika Hospitali Teule ya Mkoa wa Songwe mjini Vwawa.

Akizungumza na HabariLEO kwa simu, Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo, Dk Lukombodzo Lulandala alisema mtoto huyo alizaliwa akiwa hai na uzito wa kilogramu 2.5.
Dk Lulandala alisema mtoto huyo ni wa pili kwa Loveness na alijifungua kwa njia ya kawaida baada ya ujauzito kukamilisha miezi tisa.

“Mtoto licha ya hitilafu hizo alizo nazo za uumbaji, amezaliwa kwa njia ya kawaida akiwa hai akiwa na uzito wa kilo 2.5... Mtoto na mama yake waliendelea kuwa chini ya uangalizi wa wauguzi kwa zaidi ya saa 23 tangu alipozaliwa, lakini ndugu wa mwanamke wakisisitiza wamchukue wakamlee nyumbani…”

“Nilipowahoji walionesha hisia zao za kumtompenda mtoto walimchukua akiwa hai ila kwa sasa sina taarifa zake kama yuko hai au la,” alisema. Dk Lulandala alisema baada ya mimba kutungwa siku nane za mwanzo hitilafu za uumbaji zinaweza kujitokeza na kusababisha mtoto azaliwe akiwa hana ubongo au mgongo wazi hivyo hitilafu za uumbaji zisihusishwe na imani za kishirikina.

“Akiwa tumboni pamoja na hitilafu za uumbaji mtoto ataendelea kuishi bila matatizo kwa sababu kila kitu anategemea kupata kutoka kwa mama yake tumboni,” alisema.
Alitahadharisha kuwa mimba katika miezi mitatu ya mwanzo matumizi ya dawa bila ushauri wa daktari si salama kwa wajawazito.

Kwa mujibu wa Dk Lulandala, wanawake walio kwenye hatari ya kujifungua watoto wenye hitilafu za uumbaji ni pamoja na wanaosumbuliwa na magonjwa ya kisukari na wenye uzito mkubwa. Alishauri wanawake wanapokuwa wajawazito wahudhurie kliniki kwa uchunguzi wa kitabibu na ushauri badala ya kunywa miti shamba.

Dk Lulandala alisema, tatizo la watoto kuzaliwa bila ubongo na mfupa wa juu ya kichwa lipo kidunia na kwamba, kati ya vizazi 10,000 watoto 400 wanazaliwa wakiwa na hitilafu za uumbaji.

Alisema utafiti uliofanywa mwaka 2012/2013 ulionesha kuwa watoto 28 walizaliwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili wakiwa na hitilafu za uumbaji.
1601467027399.png
 
Kwa uelewa wangu mdogo najiuliza Kama Hana ubongo anawezaje kuwa hai??? Maana process zote katika mwili wa binadamu zinakuwa controlled na ubongo ikiwemo upumuaji. Sasa Kama hana ubongo anawezaje kupumua achilia mbali 'digestion' na process nyingine ili aweze kuendelea kuishi???🤔🤔🤔
 
Kwa uelewa wangu mdogo najiuluza Kama Hana ubongo anawezaje kuwa hai??? Maana process zote katika mwili wa binadamu zinakuwa controlled na ubongo ikiwemo upumuaji. Sasa Kama hana ubongo anawezaje kupumua achilia mbali digestion na process nyingine ili aweze kuendelea kuushi???
I second you. Ngoja tusubiri madaktari waje.
 
Kwa uelewa wangu mdogo najiuliza Kama Hana ubongo anawezaje kuwa hai??? Maana process zote katika mwili wa binadamu zinakuwa controlled na ubongo ikiwemo upumuaji. Sasa Kama hana ubongo anawezaje kupumua achilia mbali 'digestion' na process nyingine ili aweze kuendelea kuishi???
Hata mimi nimefikiri hilo, na sijaona kwenye maelezo kuwa wanaishi, ngoja tusubiri waelewa zaidi
 
Wamejuaje Kuwa Hana ubongo ilhali ubongo unakaa ndani ya kichwa na sio nje?
 
Hakuna mtu anazaliwa hana ubongo. Ikitokea atakufa instantly kabla hata hajalia
 
Mkazi wa Kijiji cha Mlowo mkoani Songwe, Loveness Kweka (25), amejifungua mtoto wa kiume asiye na ubongo na mfupa wa juu wa kichwa. Mtoto huyo amezaliwa wiki iliyopita katika Hospitali Teule ya Mkoa wa Songwe mjini Vwawa.

Akizungumza na HabariLEO kwa simu, Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo, Dk Lukombodzo Lulandala alisema mtoto huyo alizaliwa akiwa hai na uzito wa kilogramu 2.5.

Dk Lulandala alisema mtoto huyo ni wa pili kwa Loveness na alijifungua kwa njia ya kawaida baada ya ujauzito kukamilisha miezi tisa.

“Mtoto licha ya hitilafu hizo alizo nazo za uumbaji, amezaliwa kwa njia ya kawaida akiwa hai akiwa na uzito wa kilo 2.5... Mtoto na mama yake waliendelea kuwa chini ya uangalizi wa wauguzi kwa zaidi ya saa 23 tangu alipozaliwa, lakini ndugu wa mwanamke wakisisitiza wamchukue wakamlee nyumbani…”

“Nilipowahoji walionesha hisia zao za kumtompenda mtoto walimchukua akiwa hai ila kwa sasa sina taarifa zake kama yuko hai au la,” alisema. Dk Lulandala alisema baada ya mimba kutungwa siku nane za mwanzo hitilafu za uumbaji zinaweza kujitokeza na kusababisha mtoto azaliwe akiwa hana ubongo au mgongo wazi hivyo hitilafu za uumbaji zisihusishwe na imani za kishirikina.

“Akiwa tumboni pamoja na hitilafu za uumbaji mtoto ataendelea kuishi bila matatizo kwa sababu kila kitu anategemea kupata kutoka kwa mama yake tumboni,” alisema.

Alitahadharisha kuwa mimba katika miezi mitatu ya mwanzo matumizi ya dawa bila ushauri wa daktari si salama kwa wajawazito.

Kwa mujibu wa Dk Lulandala, wanawake walio kwenye hatari ya kujifungua watoto wenye hitilafu za uumbaji ni pamoja na wanaosumbuliwa na magonjwa ya kisukari na wenye uzito mkubwa. Alishauri wanawake wanapokuwa wajawazito wahudhurie kliniki kwa uchunguzi wa kitabibu na ushauri badala ya kunywa miti shamba.

Dk Lulandala alisema, tatizo la watoto kuzaliwa bila ubongo na mfupa wa juu ya kichwa lipo kidunia na kwamba, kati ya vizazi 10,000 watoto 400 wanazaliwa wakiwa na hitilafu za uumbaji.

Alisema utafiti uliofanywa mwaka 2012/2013 ulionesha kuwa watoto 28 walizaliwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili wakiwa na hitilafu za uumbaji.

Chanzo: Habari Leo
Kwa mjibu wa Baba mtoto sio kweli
Screenshot_20201002-060837_1.jpg

Sent from my Infinix X680 using JamiiForums mobile app
 
MKAZI wa Kijiji cha Mlowo mkoani Songwe, Loveness Kweka (25), amejifungua mtoto wa kiume asiye na ubongo na mfupa wa juu wa kichwa. Mtoto huyo amezaliwa wiki iliyopita katika Hospitali Teule ya Mkoa wa Songwe mjini Vwawa.

Akizungumza na HabariLEO kwa simu, Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo, Dk Lukombodzo Lulandala alisema mtoto huyo alizaliwa akiwa hai na uzito wa kilogramu 2.5.
Dk Lulandala alisema mtoto huyo ni wa pili kwa Loveness na alijifungua kwa njia ya kawaida baada ya ujauzito kukamilisha miezi tisa.

“Mtoto licha ya hitilafu hizo alizo nazo za uumbaji, amezaliwa kwa njia ya kawaida akiwa hai akiwa na uzito wa kilo 2.5... Mtoto na mama yake waliendelea kuwa chini ya uangalizi wa wauguzi kwa zaidi ya saa 23 tangu alipozaliwa, lakini ndugu wa mwanamke wakisisitiza wamchukue wakamlee nyumbani…”

“Nilipowahoji walionesha hisia zao za kumtompenda mtoto walimchukua akiwa hai ila kwa sasa sina taarifa zake kama yuko hai au la,” alisema. Dk Lulandala alisema baada ya mimba kutungwa siku nane za mwanzo hitilafu za uumbaji zinaweza kujitokeza na kusababisha mtoto azaliwe akiwa hana ubongo au mgongo wazi hivyo hitilafu za uumbaji zisihusishwe na imani za kishirikina.

“Akiwa tumboni pamoja na hitilafu za uumbaji mtoto ataendelea kuishi bila matatizo kwa sababu kila kitu anategemea kupata kutoka kwa mama yake tumboni,” alisema.
Alitahadharisha kuwa mimba katika miezi mitatu ya mwanzo matumizi ya dawa bila ushauri wa daktari si salama kwa wajawazito.

Kwa mujibu wa Dk Lulandala, wanawake walio kwenye hatari ya kujifungua watoto wenye hitilafu za uumbaji ni pamoja na wanaosumbuliwa na magonjwa ya kisukari na wenye uzito mkubwa. Alishauri wanawake wanapokuwa wajawazito wahudhurie kliniki kwa uchunguzi wa kitabibu na ushauri badala ya kunywa miti shamba.

Dk Lulandala alisema, tatizo la watoto kuzaliwa bila ubongo na mfupa wa juu ya kichwa lipo kidunia na kwamba, kati ya vizazi 10,000 watoto 400 wanazaliwa wakiwa na hitilafu za uumbaji.

Alisema utafiti uliofanywa mwaka 2012/2013 ulionesha kuwa watoto 28 walizaliwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili wakiwa na hitilafu za uumbaji.
View attachment 1585628

Mbn unarudia taarifa na wewe
 
Back
Top Bottom