Kirung'u/kichui ni ugonjwa wa aina gani, ugonjwa huu ni common maeneo ya Moshi, Arusha!

HUNIJUI SIKUJUI

JF-Expert Member
Apr 4, 2015
1,303
2,000
Kwa kichaga (cha kwetu) Rung'u maana yake ni chui, kwa hiyo sijajua kwa lugha nyingine unaitwaje na unaweza kua na majina mengine maeneo mengine kwa hiyo hilo sio jina rasmi nje ya kwetu

Uko kama pumu/sio, pumu/tb/ sio tb yaani kifua kinabana mwanzo mwisho na kukohoa sana( kwangu haikua kikavu) mpaka leo nimeshindwa kuuelewa, harufu kali/ marashi ni hatari ukiyanusa! Huu ugonjwa ulinisumbua sana nikiwa mdogo, lakini baadae nilipona kwa kupewa miti shamba, yalikua ni magome ya mti kidogo saizi ya ganda la chenza, yakachemshwa nikanywa,haikupita sekunde kumi nilisikia mvurugano wa hali ya juu tumboni nakumbuka nilitapika sana mpaka nikapotea fahamu (bibi alijua nimekufa), yule mganga alikimbia!

Baada ya kusikia nimezinduka, akaja na dozi nyingine (ilikua nipewe mara mbili), lakini bibi alikataa aliogopa kwa aliyoyaona! ikabidi yule mganga arudi na ile dawa! bahati mbaya bibi hakuuliza ule ni mti gani, miaka kadhaa baadae baada ya kua mtu mzima nikawa namuulia bibi juu ya ile dawa ila ananambia kwa yale aliyoyaona hakutaka kujua chochote juu ya ile dawa, yule mganga alitaka kumpa akae nayo lakini bibi alikataa maana aliiona ile dawa sawa na kifo! Miaka kadhaa mbele bibi akanambia yule mganga alishakufa kwa hiyo alikufa na ujuzi

Kabla ya hapo nilikua natumia dawa za hospitali miaka yote lakini hazikuwahi kunitibu,kifua kilikua kinabana mwaka mzima, nilikula sana supu ya ngal'aa (crabs) lakini wapi. Nikikumbuka hichi kitu ndo hua napata imani dawa za mitishamba zinafanya kazi japo mm ni msomi! Tangu siku iyo sijawahi kusumbuliwa na kifua mpaka leo ni mtu mzima

Swali, huu ugonjwa unaitwaje??? Na je mpaka sasa hakuna tiba?? Kuna anko wangu unamsumbua sanaa huu ugonjwa na inaonesha hospitali wameshindwa kumpa solution ya kudumu kama niliyopata mimi! HELP
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom