Kirefu cha ''RB''

JAYJAY

JF-Expert Member
Oct 31, 2008
7,494
7,517
Habari zenu wandugu!
Kuna jamaa kaniuliza swali kuwa RB ile ambayo mtu akiripoti tukio polisi huwa anapewa kirefu chake ni nini? Sikuwa na uhakika na jibu langu lakini nilijibu nadhani itakuwa ''Report Book'' ila sina uhakika. Mwenye kufahamu kwa uhakika naomba anisaidie.
 
yah ni report book
habari zenu wandugu! kuna jamaa kaniuliza swali kuwa RB ile ambayo mtu akiripoti tukio polisi huwa anapewa kirefu chake ni nini? sikuwa na uhakika na jibu langu lakini nilijibu nadhani itakuwa ''Report Book'' ila sina uhakika. mwenye kufahamu kwa uhakika naomba anisaidie.
 
RB- report book
PF3- Police Form No 3.
kuna forms za taarifa ya kupotelewa mali,forms za kuomba kufanya ukaguzi nk
 
me nadhani ingeitwa report paper(rp) ama sijui maana ya book niambie tafadhali muokoe jahazi

mpendwa,

najua shida yako ni kwa sababu ukipewa hiyo inayoitwa RB huwa unapewa kikaratasi hivi tena saa nyingine kidogo kimechanwa tu kwenye daftari la kuandikia!

kuna fomu maalum za RB kama alivyosema WAMURUBHERE hapo juu ila nadhani ni kutokana na uhaba wa stationeries tu huko kwenye vituo vya polisi ndio maana saa nyingine wanachana vikaratasi kutoka kwenye madaftari na kuandika hizo RB.

practically ukitoa taarifa inayoingizwa kwenye report book, hupewa kikaratasi fulani chenye reference number ya hiyo taarifa kwenye hiyo report book. kimsingi unapokwenda kumchukulia mtu RB polisi humaanisha unakwenda kutoa taarifa na utarudi na reference number yako ya hiyo taarifa kama uthibitisho kuwa tukio husika limeripotiwa polisi na itakayosaidia kufanya rejea ya kiupelelezi pindi mshitakiwa/mtuhumia anapokamatwa na kutiwa chini ya ulinzi wa pilisi.

kwa hiyo ingeweza pia kusemwa kuwa naenda kumchukulia RB number na ingekuwa sawasawa kabisa. ila kusema report paper (RP) si sahihi

hizo fomu zinatumika kutunzia kumbukumbu za kipolisi,hata hiyo report Book (RB) - yaani kitabu cha taarifa nayo ni fomu ya polisi yaan PF 162
 
Back
Top Bottom