Kiravu-tunaomba majina ya mawakala wa chadema waliosaini fomu za matokeo ya hai na ub


Jatropha

Jatropha

JF-Expert Member
Joined
Apr 9, 2009
Messages
1,152
Likes
144
Points
160
Jatropha

Jatropha

JF-Expert Member
Joined Apr 9, 2009
1,152 144 160
jana tar 04 nov 2010 wakati wa kutangazwa kwa matokeo ya kura za urais, tume ya uchaguzi iliwakaribisha waandishi wa habari waliokuwepo kuuliza maswali. Moja kati ya maswali yaliyoulizwa ni madai ya dr slaa aliyoyatoa tar 03 nov 2010 kuhusu kura zake kupunguzwa kwa makusudi akitoa mfano wa matatu ya majimbo ya hai, ubungo na geita.

Akijibu swali hilo mkurugenzi wa tume hiyo ndg rajabu kiravu alisema kuwa tume imefanikiwa kupata fomu za kujumlisha matokeo kutoka katika majimbo hayo na akataja kuwa idadi ya kura katika majimbo ya hai na ubungo iko sahihi na imethibitishwa na mawakala wa chadema. Ila akakiri kuwa tume ilifanya makosa katika jimbo la geita kutangaza kura za dr slaa pungufu.

Kwa kuwa tuhuma hizi ni nzito sana, nilitarajia majibu ya tume yatakuwa exhaustive enough kwa kutaja jina la mawakala wa chadema wanaoonekana katika fomu za matokeo kwa majimbo ya hai na ubungo. Kutotaja majina ya mawakala hawa bado kumebakiza wingu zito katika suala hili.

Tunamuomba dr slaa atuulizie swali hili ili tupate majibu ya kuridhisha kama kweli mawakala wa chadema walishiriki na kuthibitisha ujumlishaji wa kura za dr slaa katika majimbo ya hai na ubungo.
 
Mwanamayu

Mwanamayu

JF-Expert Member
Joined
May 7, 2010
Messages
8,385
Likes
2,449
Points
280
Mwanamayu

Mwanamayu

JF-Expert Member
Joined May 7, 2010
8,385 2,449 280
Kama waligushi tiketi za ndege ya serikali aliyotumia Salma watashindwa kwenye hili?
 

Forum statistics

Threads 1,239,125
Members 476,369
Posts 29,343,429