OMOYOGWANE
JF-Expert Member
- Dec 30, 2016
- 3,624
- 9,167
Miaka 600 BC baada ya mapinduzi ya kilimo, watu walianza kutegemea kilimo cha mvua, ikitokea msimu kuwa wa ukame mamilioni ya watu walikufa, ktk hali kama hiyo watu walitawaliwa na hofu kubwa na mashaka kila msimu wa kulima ulipowadia, hapo ndipo wakaanza kuamini kuwa huko mawinguni kuna nguvu flani isiyokua ya kibinadamu inayoshusha mvua, wakaanza kuomba na kutoa kafala ya wanyama,
Walipo vuna mazao mengi walizaliana kwa wingi, lakini pia walikua na hofu ya kuvamiwa na majirani (empire zingine) hapo wakatengeneza mungu wa pili anayehusika na mambo ya ulinzi wa empire,
Pia kulikuwa na mungu anayehusika na kuponya watu ktk empire. Huyu alikuwa ni mungu wa tatu.
Wafalme ndio waliohusika kusimamia hizo imani za miungu ktk empire zao ili kila mtu aziheshimu sababu wasipo ziheshimu basi watapata adhabu ya ukame au mafuriko (hofu),