Kipindupindu kuwagharimu viongozi Kyela

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
125,735
239,356
Hivi karibuni Dr Magufuli akiongea na walioitwa wazee wa Dar es salaam (japo wengi wao walikuwa vijana) alisema kwamba amechelewa kuwateua viongozi wa nyadhifa mbalimbali ili kupata muda wa kuangalia wenye uwezo.

Alidokeza kwamba baadhi ya vigezo atakavyotumia kwa atakaowateua ni pamoja na wale wataodhibiti kipindupindu, njaa , ufisadi na kuondoa kero ya upungufu wa madawati.

Kwa vigezo hivi bila shaka hakuna kiongozi yeyote wa wilaya ya Kyela anayestahili kubaki madarakani , na tayari mganga mkuu wa mkoa wa mbeya Dr Seif Mhina anethibitisha ugonjwa huo kuweka makazi wilayani humo.

linaripoti gazeti la Mwananchi.

Wito wangu kwa wana Kyela popote mlipo hapa duniani saidieni nyumbani kwenu hali ni mbaya kuliko mnavyosikia, ni aibu kubwa kwa wilaya nzuri kama kyela yenye nafasi ya kutosha kupata kipindupindu sawa na Tandale kwa tumbo au Buguruni kwa Mnyamani.
 
tukiwaachia wanasiasa pekee hatima ya wilaya yetu iko siku tutakuta ndugu zetu wamepukutika .
 
Back
Top Bottom