Kipindi yupo bikra alinikataa ila baada ya kuzalishwa ananitaka

Mngurimi

JF-Expert Member
May 27, 2020
819
789
Hiki ni kisa ambacho kinaweza kuwagusa wengi hasa wale vijana wa kiume katika maisha ya mahusiano. Mara nyingi unakuta katika pilikapilika za hapa na pale za kusaka mpenzi/mchumba, kijana wa kiume anampenda msichana kwa wakati fulani lakini unakuta msichana huyo hataki kuridhia muda huo hadi pale anapotendwa na mwingine au kutelekezwa.

Miaka ya nyuma kidogo kulikuwa na msichana fulani hivi nilitokea kumpenda sana. Msela nilikuwa nikijaribu kutema cheche kila kukicha bila mafanikio yoyote. Urembo, tabia na upole wake ni vitu ambavyo vilikuwa vikinivutia kiasi cha kutamani kuwa naye. Nilijaribu hadi kutumia marafiki zake wa karibu ili wajaribu kumshawishi, lakini mtoto hakutaka hata kunielewa. Mmoja kati ya rafiki yake mkubwa alisema yule dada bado hajajua na hadhani hata kama ameshakutana na mtu yeyote yule kimwili.

Baada ya kuona nyavu zangu hazinasi, ilibidi nimpotezee niendelee na maisha mengine. Baada ya hapo nilisafiri kwenda masomoni kwa muda wa miaka miwili. Kitu cha kushangaza baada ya kurudi nilishangaa kumkuta dada wa watu akiwa na mtoto wa miezi miwili. Nilishangaa sana japo moyoni nikasema tayari wahuni washamkomesha. Kilichonishangaza zaidi yule dada baada ya kupata taarifa kuwa nimerudi, alitafuta namba yangu na kuomba tuonane.

Kabla ya kumkubalia, nilikataa sana ila baadaye ilibidi nikubali wito wake. Siku ya kuonana iliwadia na katika maongezi yake alikuwa akidai kuwa nimsamehe kwa sababu ananipenda. Kusema kweli, nilikataa na kudai kuwa "laiti kama angekuwa ananipenda, basi angenikubalia tangu mwanzo". Isitoshe mimi tayari nilikuwa kwenye mahusiano na mtu mwingine hivyo isingekuwa rahisi kuwa naye tena.

Baada ya mazungumzo nikamtia moyo na nikamwambia aendelee na yule aliyemzalisha japo kwa maelezo yake anasema, baada ya kujifungua jamaa alianza visa na kukwepa majukumu kisha wakaachana. Kusema ukweli, mimi niliumia maana sina moyo wa chuma wa kustahimili mtu azae na mwingine kisha aje kwangu kama kimbilio.

Swali langu:
Hivi mtu wa namna huyo unaweza kumkubalia kwa lipi?
Kama alikuwa ananipenda ni kwa nini asingekubali tangu wakati ule kiasi cha kunitesa moyo wangu kiasi kile?
Mambo haya huchochewa na nini hasa kwa wasichana?

Karibuni tushauriane.....
 
Huyo yupo desperate baada ya kuzalishwa na kutemwa. Hapo anajiona hana thamani tena ndio maana amekumbuka koloni lake la zamani
Ila mkuu hapa kuna mawili lako likiwa la kwanza na la pill inawezekana huyo msichana/ mwanamke alikuwa anampenda kweli huyo jamaa ila ugeni wa hayo mambo kwake as one of her friend said that she had been a vargin before she got conceived ndiyo yalikuwa yanamfanya amchomolee.
Ushauri kwa mleta mada; kama bado wampenda we mkubalie tu ila ndo hivyo unauchukua mzigo wa malezi ya motto and that's her plan ila hakuna upendo walal nini hapo.
 
Unajua ndugu, ni bora hata ningekuta yupo kwenye uhusiano mwingine tu kuliko kukuta ana mtoto. Nafsi yangu naweza kuwa naidhulumu sana
 
Unajua ndugu, ni bora hata ningekuta yupo kwenye uhusiano mwingine tu kuliko kukuta ana mtoto. Nafsi yangu naweza kuwa naidhulumu sana
Kwa kipindi hiki inabidi uwe mkarimu na mpole kwake, don't be rude to her kutoka na situation anayoiface. Katika atakayokuwa anakushirikisha mjibu kiupole, kiujanja na kutengeza njia ya kukuchukulia na kukuzoea kama rafiki wa kawaida. Ila kwa swala la kuwa wapenzi sikushauri
 
Ndiyo maana nilikuwa nikimtia moyo sana
 
Back
Top Bottom