Mgombezi
JF-Expert Member
- Mar 23, 2009
- 610
- 178
Nimeona TBC wameandaa kipindi maalumu kwa ajili ya utambulisho wa FastJet, ambapo walikuwepo waandishi wa habari na baadhi ya viongozi wa serikali. Hivi ni sahihi kwa TBC kuandaa/kuonyesha kipindi hiki ukizingatia kwamba tuna shirika letu la taifa la ndege. Hawa FastJet ni washindani wetu katika biashara, inakuwaje tunawapa promo washindani wetu. Je serikali ina hisa katika shirika hili? Halafu watanzania tunawaona hawa kama wakombozi wakati biashara ya budget airline ni kawaida na ipo duniani kote.