Kipindi maalum tbc kwa promo ya fastjet

Mgombezi

JF-Expert Member
Mar 23, 2009
610
178
attachment.php

DSC05142.JPG DSC05142.JPG
Nimeona TBC wameandaa kipindi maalumu kwa ajili ya utambulisho wa FastJet, ambapo walikuwepo waandishi wa habari na baadhi ya viongozi wa serikali. Hivi ni sahihi kwa TBC kuandaa/kuonyesha kipindi hiki ukizingatia kwamba tuna shirika letu la taifa la ndege. Hawa FastJet ni washindani wetu katika biashara, inakuwaje tunawapa promo washindani wetu. Je serikali ina hisa katika shirika hili? Halafu watanzania tunawaona hawa kama wakombozi wakati biashara ya budget airline ni kawaida na ipo duniani kote.
 
Mkuu wamelipia kama matangazo mengine ya biashara za makampuni binafsi.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums

Ningeweza kuwaelewa kama hicho kipindi kingeandaliwa na video production nyingine na kuja kurushwa tu TBC, ningeweza fikiri hivyo; lakini hapa TBC ndio wameandaa; watangazaji tunaowalipa mshahara kutokana na kodi zetu wameliponda shirika letu waziwazi.
 
Ni sahihi maana TBC inabidi iwe neutral katika mambo ya biashara, sio kupigia debe kampuni mbovu ili mrandi ni ya serikali.
 
Ningeweza kuwaelewa kama hicho kipindi kingeandaliwa na video production nyingine na kuja kurushwa tu TBC, ningeweza fikiri hivyo; lakini hapa TBC ndio wameandaa; watangazaji tunaowalipa mshahara kutokana na kodi zetu wameliponda shirika letu waziwazi.

Uwezekano mkubwa ni kwamba - wamelipia airtime pamoja na production ya tangazo/kipindi hicho chote. Sidhani kama kuna makosa yoyote ya kidhana, kiitikadi za kibiashara kwa TBC kufanya hivyo. 'Matter of fact hii inaonesha zaidi kuwa wapo neutral kibiashara.
 
Wanashinda wanatangaza maendeleo uchwara ya ccm hela watapata wapi? Hawana hata sera ya utangazaji ,kila kitu lete tu
 
attachment.php

View attachment 72752View attachment 72752
Nimeona TBC wameandaa kipindi maalumu kwa ajili ya utambulisho wa FastJet, ambapo walikuwepo waandishi wa habari na baadhi ya viongozi wa serikali. Hivi ni sahihi kwa TBC kuandaa/kuonyesha kipindi hiki ukizingatia kwamba tuna shirika letu la taifa la ndege. Hawa FastJet ni washindani wetu katika biashara, inakuwaje tunawapa promo washindani wetu. Je serikali ina hisa katika shirika hili? Halafu watanzania tunawaona hawa kama wakombozi wakati biashara ya budget airline ni kawaida na ipo duniani kote.

Kama ndo tunafikiria namna hii, basi tunasafari ndefu ya kujikomboa kifikra na kiuchumi
Kwa mtazamo huu ungefurahi kama serikali isingetoa kibali kwa precision air, fast jet n.k ili kulinda atcl.

Ungefurahi pia kama serikali isingetoa kibali cha kufanya biashara kwa vodacom, tigo, airtel n.k kwa sababu kuna TTCL.

Mzee funguka kifikra. Achana na propaganda za kisiasa. Kuendelea kiuchumi siyo lazima kuwa na state owned companies
 
Watu wanafikiri kila biashara ya ndege duniani ya Taifa flani,
Emirates, KQ, Qantas haya ni mashirika yenye ushirika kati ya serikali na watu binafsi. Hata ATC ingewekwa kwenye soko la hisa pale DSE sidhani kama ingeendeshwa kwa hasara na kujifia.
 
Mie naona sawa maana hata hilo shirika letu limeshakufa kwahiyo bomba tu.

Shirika letu la ndege limebakiwa na ndege moja tu tena ya kukodi ambao mkataba wake unaisha kesho that means kuanzia dec shirika litakuwa halina ndege ila limepeleka mainjinia itali kuangalia ndege zinavyotengenzwa!! Job true true kazi kweli kweli zika likwe likwe.
 
Back
Top Bottom