Kipindi Maalum TBC kuhusu hali ya Usafiri wa Reli Tanzania

Mhafidhina

JF-Expert Member
Feb 6, 2008
549
22
Wanajamii,

Sina uhakika kama kila mtu anakifuatilia kipindi kimoja kinachorushwa na TBC1 (Jerry Muro) kuhusu hali halisi ya usafiri wa Reli Tanzania haswa kati ya DSM na Kigoma.

Kwa kweli nimekua nikikifuatilia kwa umakini sana kipindi hichi na nimeumia roho sana mno mno kuona hali halisi ya usafiri ambao hata ng'ombe au mbwa hawezi kusafiri kwa shida kiasi hicho.

Napenda kumpongeza sana mno muandishi wa habari Jerry Muro kwa habari hii ambayo ameifanya kwa kuichunguza kwa undani hali halisi na kuifuatilia yeye binafsi ikiwa ni pamoja na kusafiri ndani ya treni hizo na kujionea hali halisi wasafiri wanayoipata wakiwa kwenye safari hii ya mateso makali. Kweli habari hii imeaunika hadharani uozo mkubwa uliopo wa usafiri wa Reli Tanzania lakini pia, uzembe mkubwa uliopo kwenye shirika la reli nchini na shrika lililoingia Ubia la RITES.

Kweli imenigusa mno mno. Kipindi hichi kinarushwa kila siku saa nne kamili usiku na TBC1
 
Back
Top Bottom