Kipindi kigumu cha mpito kuelekea utawala bora, Rais Samia anatakiwa apatiwe ushirikiano wa kweli toka kwa wananchi

sammosses

JF-Expert Member
Jan 24, 2011
1,536
2,000
.

Tanzania ina pitia kipindi kigumu cha mpito kuelekea kwenye mfumo wa utawala Bora,unao zingatia sheria na katiba. Ni kipindi kigumu Sana cha maamuzi mazito tena magumu kurudisha utawala wa sheria.

Wananchi walipokwa mamlaka na madaraka yao kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri ya Muungano ibara ya 8,kitendo cha kurudisha imani kwa waathirika wengi walioporwa mamlaka na madaraka yao bila kujali maumivu ya waathirika wachache wa maamuzi hayo Kuna ifanya serikali kuaminika tena mbele ya wananchi.

Utawala Bora ulipotezwa kwa utashi wa dikitekta mmoja aliye tengeneza channel ya udikitekta kwa watendaji wake sasa unaelekea kupoteza nafasi yake.

Wapo vijana wadogo wanufaika wa utawala wa kidhalimu ambao ulifumbia macho maovu ya watendaji wake sasa wanaelekea kuishi Kishetani kama ambavyo matajiri walivyoishi kwa matakwa ya Mtawala mkuu.

Sabaya ni nembo ya uovu wa kimamlaka iliyo tengenezwa na Mtawala, ndiyo maana hata kitendo chake cha uhalifu mkubwa wa kuchafua diplomasia ya Kimataifa kwa kutumia plate number za umoja wa mataifa (UN) zilionekana Kama ishu ndogo na kuchukulia poa bila kujali athari za mahusiano ya Kimataifa.

Maumivu ya wahanga wa mfumo kandamizi uliopora haki za umiliki ya Mali kumeifanya Tanzania iwe ngumu kwa Watanzania wake kwa kutengeneza maskini kinyume na malengo ya Millennia.

Uvunjwaji wa makusudi na ukanyagaji katiba uliofanywa makusudi ni zaidi ya ujambazi wa kimamlaka katika kujinufaisha binafsi na Mali ya umma,mfumo wa Kishetani unao jihujumu kwa kuuwa vyanzo vya mapato na kumtengeneza rais-mungu mwenye miliki ya kila kitu mpaka uhai wa wananchi.

Wapo wengi waliopewa dhamana ambao kwao katiba ilioneokana Kama kitabu cha hadithi za kusadikika sasa wajiandae kusalimu amri kwa kuwa kila zama zina nabii wake na kitabu chake.

Kinacho sikitisha waathiri na watuhumiwa wakubwa ni vijana wadogo walioleweshwa mvinyo wa madaraka na kujisahau kwa ulevi huo kupita kiasi.

Wapo wafuasi wao,ni viongozi wa CCM kwa ngazi zote ambao wanachukizwa na style mpya ya kipindi cha mpito,wanaendelea kuharibu itifaki na falsafa ya CCM kwa kuamini katika mabavu na nguvu zilizokithiri. Hawa hawapaswi kuvumiliwa hata huko ndani ya chama. Tunataka vyama vinavyo shindana kwa hoja si vyama vya kintaharamwe kuelekea mapinduzi ya amani.

Mwenye akili timamu na anayetokana na zao la amani hawezi kuwa mfuasi wa uovu. Nikupongeze Sana mama kwa hatua stahiki unazochukua.

Pamoja na Sabay bado wengine wanaotukana wananchi hadharani,mkuu wa Wilaya ya Iringa naye ni miongoni mwao. Kwa kuwa cheo ni dhamana wanapaswa kujua kuwa dhamana hiyo inatoka kwa wwnanchi,kuheshimu tu mamlaka ya uteuzi bila kuwaheshimu wenye kutoa mamlaka hiyo ya uteuzi ni kuwakosea adamu wananchi,ajipime bwana Kasesera Kama bado anastahili kuendelea na udc wake wa fadhila.

Wananchi wanapaswa kuwa bega kwa bega kutoa mikingamo hii kuwafichua watendaji dhalimu wasio zingatia maadili ya utumishi wa umma,hivyo hatuna budi kumsaidia rais wanaye mdhihaki kuwa wa katiba ili aweze kuisimamia katiba ipasavyo.

CCM kuendelea kuwanyamazia vijana wake wakaidi kwa kumdhihaki Rais wetu mathalani God CCM maanake ni kuonyesha jinsi gani chama kilivyo poteza imani kwa wananchi,kwa kuamini katika ushindi wa maguvu bila hoja. Mama una kazi nzito ndani ya chama chako kwa kuwa wamezoea kunyonga wewe unayependa kuchinja kwao ni kikwazo.

Mwisho mabadiliko yeyote anayo yafanya mama ni kwa kuzingatia matakwa ya sheria na katiba, had jalishi mna itikadi inayo fanana,muhimu Tanzania kwanza vyama vyenu baadae.
 
mmh

JF-Expert Member
Nov 9, 2010
2,863
2,000
Ulikua na mada nzuriii ila umeharibu kwa kuanza kumkejeli raisi wetu kipenzi hayati JPM.
 
barafuyamoto

JF-Expert Member
Jul 26, 2014
31,584

Kuna mahali umesema KURUDISHA UTAWALA WA SHERIA, lini Tz ilikua na utawala wa sheria na umepotea sasa unatakiwa urudishwe?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom