NostradamusEstrademe
JF-Expert Member
- Jul 1, 2017
- 3,032
- 4,028
Kipindi hiki cha wimbi la tatu la Corona DELTA linatishia sana uhai kwa watanzania.Hapo hapo unakuta watu wanafanya harusi kukutanisha watu wengi wengi hivi tunajipenda kweli.
SIkatai harusi ni kitu kizuri cha kumbukumbu lakini tungeangalia hali halisi kwa sasa.Mi ningeshauri kuliko kuhatarisha maisha si bora ile michango yote tuliyotoa tukampa bwana na bibi harusi wakaanzie maisha.
Siku ya kufunga ndoa wanaweza kujitoa kimasomaso na wasindikizaji wao na wazazi wao wakifungishwa ndoa kanisani au msikitini au bomani wilayani. Baada ya hapo wanafamilia tu wakawarudi nyumbani wakasherehekea kuliko kukusanya umati wa watu wengi kuambukizana ugonjwa.
Watanzania tubadilike sio lazima ukichanga ukalipizie siku ya harusi kwa kunywa na kula jamani tujali hali ya sasa.