Dahafrazeril
JF-Expert Member
- Jul 28, 2015
- 1,500
- 2,055
Sabalkheri wana Jamii Forums?.
Naanza kwa usaili na nitamaliza pia kwa usaili. Usaili ni kuuliza masuala ya msingi. Kuanzia unachokiona, unachokisikia, unachokidhania, unachokishika na kadhalika. Hivi ndivyo walivyofanya kina Socrates, Pythagoras, Galileo Galilei, Fantz Fanon, Mwl J.K.Nyerere na orodha inaendelea...
Huu waraka ni Nasaha kwa Wizara ya Elimu, mzazi, mlezi, kaka, dada na Jamii yote ya Watanzania wenye tafakuri za kina na wenye mapenzi ya dhati kwa Taifa lao la sasa na la baadaye. Maagizo haya yametoka kwa Mungu. Ni sharti Mzazi amlee mtoto katika njia impasayo kwakuwa (Mtoto) hatoiacha kamwe hata atakapokuwa Mzee ( Mithali 22;6). Nb; Silaha zinaandaliwa wakati wa amani na si wakati wa vita.
Hivi karibuni, miezi kadhaa ilopita nimekuwa nikifuatilia kwa ukaribu uso na mashaka kipindi cha SKONGA kiendeshwacho katika luninga kupitia East Africa Television (EATV).
Nikiandikacho hapa ni ushuhuda wa nilichokishuhudia na ninachozidi kukisaili (siyo kuhadithiwa) kama pengine ambavyo huenda ukawa ndiyo kwanza unalisikia jina hili la kipindi cha SKONGA katika maandishi haya. Ninatazama kipindi hiko na ninazidi kukitizama kila panapobidi. Kama pia uliwahi kukitizama ni vizuri lakini pia kama hukuwahi kukitizama ni vizuri pia. Nitajaribu kudokeza kidogo ili sote tupate taswira kamili juu ya kipindi hiki.
Kiekweli, bila kupepesa ukope wala kumungunya maneno kuna walakini katika Taasisi yetu ya Elimu, Taasisi ya Familia na Taifa kwa ujumla. Kuna kasoro katika mitaala yetu ya kielimu. Silabasi zetu hazimuandai Mwanafuni kukabiliana na mazingira ya wakati wa sasa na ujao.
Kuna wakati wa Q & A (Questions and Answers) katika kipindi hiki cha SKONGA. Kiukweli hapa ndipo ninapochoka juu ya wanafunzi wetu. Round knowledge ya mambo anuai, current news na kadhalika ni baadhi tu ya mambo yanayoifanya kipindi hiki kiwe cha vichekesho na pengine si kusadifu lengo la kuanzishwa kwake.
Tuna upungufu Mkubwa sana wa Maarifa (General knowledge) vichwani kwa Wanafunzi wetu. Si wanafunzi wa S/Msingi, Sekondari na hata Vyuoni. Ni unazi, utunduwizi, ufisadi na ufisidi, umaamuma, ushabiki, utovu wa adabu, mbwembwe, ulimbwede, dharau na kedi, migoda mikogo na kadhalika.
Wanafunzi hawa hawafahamu mengi na wameridhika na hali walizonazo. Pengine hili si kosa lao, rafiki yangu mmoja anapenda kuniambia "Aliyetuloga keishakufa". Maswali yaulizwayo katika kipindi hiki ni ya kawaida mno ila wanayakosa makusudi. Tatizo ni nini?. Nani apewe lawama?.
Hivi mwanafunzi wa Kidato cha nne unashindwa vipi Square root ya 144?. Kirefu cha USD, TAZARA, BOT, EAC nk?. Humfahamu vipi Shaaban Robert?.
Mbona tunafahamu kirefu cha WCB, Washindi wa Miss Tanzania/World?. Mbona tunafahamu sinema za Kikorea na waigizaji wake?. Mbona tunafuatilia Fiesta kama tumerukwa na akili?.
Wanafunzi hawahawa wanamiliki simu za mkononi bila Mzazi/mlezi, Mwalimu kufahamu. Bora basi hata wangekuwa wanatumia simu hizi katika masuala ya msingi lakini wapi?..Ukibahatika kuzishika hizo simu utavunjika moyo sana na pengine atapandwa na presha (Bp) bure. Huku ni kufeli kwa Taasisi za kifamilia. Wazazi na Jamii kwa ujumla hawayaelewi madhara ya utandawazi ndiyo maana watoto wengi wanavutiwa na vikolombwezo hivi viso na mantiki..
Nilifikiria sana na kupata majibu kuwa "Ndiyo maana tu wepesi kufuatilia Big brother na Miss world kama tumerukwa na akili kuliko kufuatilia washindi wa Tuzo ya Nobel kwa mwaka huu". "Ndiyo maana tu wepesi kufahamu jina la Miss Tanzania kuliko jina la mwanafunzi aliyepata maksi za juu katika mitihani ya darasa la saba mwaka huu". Kwanini wanafunzi wetu ni wahanga wa kufuatilia masuala yaso wajenga?.
Hizi ni Zama za 'Maarifa na Taarifa (Information age). Uelewa wa Mambo na ujenzi wa hoja ndivyo vinvyompa mwanafunzi nafasi ya kuwa bora zaidi ya mwingine na si usadikifu pofu wa kimakundi, ushabiki uso na mantiki na Umaamuma. Ukiona nafsi yako inataka kujua vilivyo bora zaidi sambamba na visomo, pima mashauri kwa kusudio lenye kuakisi mapenzi mema, nia kuu zaidi na upendo usio na mipaka juu yote na kila kitu.
Ni sharti Ubongo, Nafsi na Roho ya Mwanafunzi iJifunze si tu ya watu wa asili ya kabila moja, bara moja, rangi moja na kadhalika. Dunia yote na watu wake ni jamii yake na ni fahari za utu, mwangaza na fanaka kujaliwa kheri na kweli moja iliyo ni Uzima. Misimamo ama itikadi iso na staha si vya kupewa nafasi kabisa, ni sharti kuvibeza kwa akili na roho huku utunduwizi na ujinga vikifutiliwa mbali.
Ninachohitaji kukikusudia hapa ni kutoa ushauri kwa wahusika na haraka iwezekanavyo juhudi za makusudi zichukuliwe mapema ili kujinasua katika kile Prof Chachage alichokiita "Collective imbecilization".
Tusijipumbaze kihalaiki katika hili. Mwanafunzi achukue wajibu wake, Mwalimu na mzazi pia. Hakuna kutegeana katika hili. Utegevu ukiwepo, lazima pengo lionekane.
USHAURI.
Wazazi, walezi, kaka, dada na kadhalika waelekeze nguvu za ziada kwa walengwa (wanafunzi) kwa kuwawezesha kuwekeza zaidi katika Maarifa ikiwa ni pamoja na kuwasimamia vizuri katika matumizi yao ya muda. Kwenda katika sinema zisizo na tija, vibanda vya luninga, Kuzidisha michezo, kutazama luninga sana ni moja ya mambo ya kukatazwa na mwenye dhamana kwa mwanafunzi.
Ni vyema mwanafunze apate utulivu wa akili (Calmness of mind) walau kila siku ili ajiboreshe zaidi na zaidi. Kushughulika na mambo mengi yaso na tija ni kuuharibu ubongo wa mwanafunzi na madhara yake ni makubwa sana kwa siku za usoni.
Tuache kujenga Baa majumbani na badala yake walau tujikite katika ujenzi wa Maktaba (Library) kwa ajili ya kujisomea na kuongeza wigo mpana wa Uelewa kwa wanafunzi wetu na kujenga Taifa la wasomi wanaojitanua kimawazo.
Wanafunzi wanunue/ wanunuliwe vitabu vya kujisomea (Kiada na ziada). Siyo ununuzi wa vitabu vya mitaala ya shuleni tu. Vitabu nje ya mitaala (Riwaya, Tamthiliya, Ushairi nk). Mkusanyiko wa maudhui yapatikanayo katika vitabu vya Ushairi, Riwaya na Tamthiliya huweza kuwa na mchango chanya kwa wanafunzi kuliko magazeti ya udaku pamoja na vitabu visivyowajenga kimaarifa.
Hapa najua wengi watazungumzia gharama (cost) za vitabu ila ukweli ni kwamba, Tatizo siyo gharama ya kitabu. Tatizo ni gharama atakayoilipa mwanafunzi kwa kutokusoma kitabu. Sisi ni matokea ya yale tunayojifunza kwahiyo kama huna wigo mpana wa mambo basi wewe si chochote. Na kwa mujibu wa tafiti "Maarifa unayoyajua sasa yatakuwa yamepitwa na wakati baada ya miaka miwili hadi mitatu". Kila uchwao tujifunze na kujifunza tena.
Mithali 4 : 13
"Mkamate sana elimu, usimwache aende zake; Mshike, maana yeye ni uzima wako."
Proverbs 4:13
"Hold on to instruction, do not let it go; guard it well, for it is your life."
One Thing; #Be Wise with your comment(s).