Kipindi cha Nyerere -vs- Kipindi cha Kikwete | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kipindi cha Nyerere -vs- Kipindi cha Kikwete

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by skasuku, Nov 28, 2008.

 1. s

  skasuku Senior Member

  #1
  Nov 28, 2008
  Joined: Apr 19, 2008
  Messages: 113
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Naomba nirushe hili swali na tuweze kuchangia maoni yetu:

  Je ni raisi yupi kati ya Nyerere na Kikwete ambayo wakati wakuchukua/wakupewa madaraka amekutana na changamoto (challenges) kubwa zaidi?
   
 2. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #2
  Nov 28, 2008
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Kwa upande wangu naona hakuna hata mmoja wote Nyerere ameipokea nchi kutoka kwa wakoloni ikiwa imejaa mashamba ya mkonge,buni na vyenginevyo na Kikwete nae hana changamoto amerithi utawala.
  Changamoto au chalenge itapatikana wakati Nchi itakapopata mtawala kutoka Chama kingine na sio CCM ,ni maoni yangu.
   
 3. Pundit

  Pundit JF-Expert Member

  #3
  Nov 28, 2008
  Joined: Feb 4, 2007
  Messages: 3,741
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Ni vigumu kulinganisha administration mbili zilizokuwa katika nyakati tofauti.Hii pamoja na sababu nyingine, inatokana na ukweli kwamba, challenges alizozikuta Kikwete zilikuwa zimepozwa au kuchochewa na kazi ya Nyerere, kwa hiyo kuwalinganisha inakuwa ni swala gumu. Ingekuwa hawa ni marais wa nchi mbili tofauti ingekuwa rahisi kulinganisha challenges walizokutana nazo.

  Baada ya kusema hivyo, kwa kujua kuwa chochote kitakachosemwa kitatiwa mawaa na ukweli huu, naweza kusema kuwa.

  Nyerere obviously alikuwa na challenges kubwa zaidi. Alipochukua nchi kulikuwa na wasomi wachache sana na hakukuwa na miundombinu ya kutosha. Alichukua mkusanyiko wa makabila na kupata challenge ya kuwafanya wote kuwa nchi moja, alichukua nchi yenye system ya uchifu, basically traditional kingdoms na kufanikiwa kuifanya nchi inayoamini katika usawa wa binadamu. Zaidi ya hapo, alipitisha lengo la kuwaunganisha Watanganyika kwa kuunda Tanzania ambayo ilikuwa muungano wa Tanganyika na Zanzibar.Ndoto zake za umoja wa Afrika unaoanzishwa na umoja wa majirani zilizimwa na Kenyatta ambaye alileta ukabila katika mazungumzo ya muungano wa Afrika ya Mashariki. Nyerere aliweza kusomesha watu wengi na kufanya Tanzania kwa wakati mmoja iwe miongoni mwa nchi za juu kabisa katika literacy Africa.

  Lakini hata kama kuna ubishi kuhusu mafanikio yake, swali lilikuwa na challenges, si mafanikio.

  Kikwete challenges zake karibu zote zilikuwa ndani ya uwezo wake.Ukiachilia mbali uchumi mbovu, ambao wananchi wengi kama sio wote wanajua kwamba sio kosa lake Kikwete binafsi na hivyo wangeweza kumsamehe kama kungekuwa na maendeleo kidogo katika uchumi, Kikwete aliingia madarakani kwa mbiu ya "Ari Mpya Kasi Mpya" ambayo iliwapa wananchi matumaini ya mabadiliko.Alikuwa na challenges ndogo ukimlinganisha na Nyerere kama vile kuimarisha muungano ambao umelegalega , kukiimarisha chama chake, kukomesha rushwa na kurudisha imani ya wananchi katika uongozi wa CCM. Ingawa Kikwete amekuwa na challenges ndogo kuliko Nyerere, mpaka sasa zinaelekea kumshinda.
   
 4. Pundit

  Pundit JF-Expert Member

  #4
  Nov 28, 2008
  Joined: Feb 4, 2007
  Messages: 3,741
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Ndugu Mwiba,

  Umeelewa swali? Au unataka kuwa Yogi Berra?

  Swali ni comparison ya challenges alizozipata Nyerere wakati anachukua nchi vs alizozipata Kikwete, zipi zilikuwa kubwa zaidi?

  Sasa utasemaje "hakuna hata mmoja"? Swali si nani alifanikiwa kuzifanyia kazi challenges hizi, ni zipi zilikuwa tough zaidi.

  Kusema kwamba "hamna hata mmoja" kwa maan ya kwamba wote walikuwa na 0 challenge ni utovu wa maoni, kwa sababu nilizozitaja katika post yangu hapo juu.
   
 5. Madela Wa- Madilu

  Madela Wa- Madilu JF-Expert Member

  #5
  Nov 28, 2008
  Joined: Mar 24, 2007
  Messages: 3,074
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  Ni vigumu kupanda Mlima Kilimanjaro hadi kileleni.
  Lakini ni vigumu zaidi kudumu na kujenga kambi pale kileleni japo mwezi mmoja tu.

  Challenge ya Nyerere ilikuwa ni ku rediscover nchi na utu wa watu na kuwaweka tayari kujenga nchi yao.

  Challenge za Marais wote waliofuata ilikuwa ni kujenga uchumi imara wenye kujitegemea na kuweka nidhani katika utawala na sheria.

  Kwa hiyo challenge kubwa ya kikwete ni ni kurudisha nidhamu katika safu zote za utawala serikali na kuanza kuweka misingi imara ya kujenga uchumi mama.
  Ubadhirifu mkubwa wa mali ya umma na ufisadi wa kupindukia ni matokeo ya uongoziwa kitaifa kutokuwa na nidhamu na ari ya kufanya kazi.
  Mtu yeyote asiye na nidhamu hujiweka juu ya tartibu za kila siku,mila,maamuzi ya kijamii na zaidi sheria na katiba ya nchi.
  Ni hawa hawa mafisadi ndiyo wenye tabia chafu ya kutembea na wake za watu mwenyewe akija juu anakatiwa mpunga na kusakiziwa kigori mpaka anasahau.

  Challenge kubwa ya MH Kikwette ni kurudisha nidhamu.

  Nidhamu kwanza.
   
 6. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #6
  Nov 28, 2008
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,203
  Likes Received: 864
  Trophy Points: 280
  Baada ya kutawaliwa na wakoloni kwa zaidi ya karne, Nyerere alikumbana na changamoto kubwa ya kuwafanya watu wetu wajitambue kuwa wao ni wao kwa ajili yao na ni wajibu wao kushirikiana na serikali yao ili kujiletea maendeleo bila kumtegemea tena mkoloni.


  Baada ya kutawaliwa na CHAMA kimoja kwa takriban nusu karne na serikali kugeuka kuwa isiyojali kabisa maendeleo ya raia wake kichumi, Kikwete anakumbana na changamoto ya kuwafanya raia waamini tena kuwa kweli serikali ipo kwa ajili ya wananchi na inajali maendeleo yao.
   
 7. M

  Mkandara Verified User

  #7
  Nov 29, 2008
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Duh! mkuu hili swali zito lakini nadhani linaweza kujibiwa kinamna!..
  Nyerere alitawala wakati wa wajinga wengi... na Kikwete ametawala wakati kuna Wajanja wengi, sasa hapa inategemea hizo challenges unazozungumzia ni zipi..

  Kuyapata Maendeleo ukiwa na wajinga wengi ni kazi nzito sana (hawakuelewi) lakini pia ni kazi nyingine kuyapata maendeleo ukiwa na wajanja wengi (wanaelewa kuliko wewe) hao - Mafisadi!
   
 8. Zakumi

  Zakumi JF-Expert Member

  #8
  Nov 29, 2008
  Joined: Sep 24, 2008
  Messages: 4,817
  Likes Received: 327
  Trophy Points: 180
  Mwiba:

  Maendeleo yanaletwa na watu. Pamoja na mimi kuzichukia siasa za Nyerere, lakini Nyerere aliacha watu ambao walikuwa na upeo mkubwa kuliko wale walioachwa na mkoloni.

  Mkoloni alituachia vitu lakini vitu bila watu ni sawa na kuku na almasi.
   
 9. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #9
  Nov 29, 2008
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Hakuna chochote ni ubovu wa utawala wa CCM ,wote wameikuta nchi katika amani na utulivu,wameshindwa kuliendeleza hilo,na wote wameikuta nchi ni tajiri wameshindwa kuulinda na kuutumia kwa ajili ya maendeleo kwa wananchi.

  Kusema Nyerere alikuta watu wajinga hilo sio kweli,si Nyerere peke yake alikuwa msomi wakati huo ,yeye Nyerere aliwakuta watu wakiwa katika harakati za siasa.Kikwete ni mrithi wa utawala ni kama mtoto wa Mfalme kwenye utawala huu wa sisi au huyu ni mwenzetu.

  Msimamo wangu ni kuwa Challenge itakuja yatakapotokea mabadiliko ya uongozi kichama na si kimtu katika kuiongoza Tanzania.

  Huwezi kusema unakutana au umekutana na Challenge wakati system nzima ya utawala liusalama kiulinzi ipo chini yako inasikiliza amri tu ,nini wafanye,hatua gani wachukue ,leo ukubwa huo na cheo hicho hakitumiki ni kuendeleza kuogopana ,wandugu challenge iliyopo ni kushindwa kwa wakubwa wa Chama tawala kuchukua au kutumia madaraka yao kama viongozi wakuu wa nchi ,wanaheshimiana ,wanalindana ,ni mrafiki jamani katika kuongoza nchi unaleta udugu na urafiki ,kweli tutafika ?,CCM wameshindwa kuendeleza nchi wapo pale pale kila anaekuja anachukua chake mapema , halafu unategemea kuwa anaerithi aendeshe nchi tofauti na wenziwe ambao bado wamo katika system ,si unaona kila Raisi aneondoka huwa anashiriki katika maamuzi mbona nchi nyengine hatuoni utumbo huu si kwenye utawala wala kwenye chama ,huyo hapo Mandela tokea aache Uraisi humsikii katika harakati za kiserikali wala za kichama iweje hapa Tz viongozi wastaafu wawe ving,ang'anizi kama si kukiritimba ni kitu gani ,vipi utamweka Raisi aliekuwepo kuwa anakutana na challenge wakati wote wamo kwenye chungu kimoja.
  Chama mbadala katika uongozi ndicho kitakachokutana na Challenge ya kuhakikisha yale ya kuogopana yote yanafanyiwa kazi kikamilifu na sio kusuasua.
   
 10. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #10
  Nov 29, 2008
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  I like this one!!
   
 11. Zakumi

  Zakumi JF-Expert Member

  #11
  Nov 29, 2008
  Joined: Sep 24, 2008
  Messages: 4,817
  Likes Received: 327
  Trophy Points: 180
  Mwiba:

  Hayo mambo ya vyama mbadala ni mambo ya magharibi. Mashariki watu wanaendelea hata serikali ikiwa ni ya kidikteta au chama kimoja. Au ya vyama vingi lakini ni chama kimoja tu kinachotawala.

  kwa mtaji huo siri ya urembo sio siasa tu. Na kama kitu kuendelea ni lazima kiwe na mbadala basi Tanzania ingekuwa mbali kwenye soccer maana Simba na Yanga hawakai chungu kimoja.

  Kwa maoni yangu tunahitaji uwazi na check and balance.
   
 12. M

  Mkandara Verified User

  #12
  Nov 29, 2008
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Mwiba,
  Mkuu labda hapa umeshindwa kuelewa maana...
  Tunazungumzia Challenges walizokutana nazo viongozi hawa ambazo zisifahamu kwa ujumla wake isipokuwa kama navyosema kila siku unapotaka kutoa hukumu jaribu sana kuangalia WATU na MAZINGIRA..
  Kweli Nyerere alikuta watu ktk harakati za Uhuru lakini hao unaowasema ni wangapi?..Kwa hiyo maendeleo sio swala la kupanda bus na dereva mtu mmoja ila nchi nzima inakuwa kama mashua ambayo kila mmoja wenu anachangia ktk upigaji kasia ili mashua iende mbele.. tatizo ndio hapo, wengine ndio kwanza walishika hizo kasia mkononi kwa mara ya kwanza na kama wewe umewahi kupiga kasia utanielewa nazungumzia nini..Ujinga ni kutokuelewa mkuu sio tusi...
  Na challenges hazizungumziwi harakati za Uhuru pekee bali Uongozi wake wote miaka 23 kama rais wa nchi.. hao wengine waliomtangulia walikuwa viongozi wa chama sio taifa ama wananchi wote. Kulikuwepo na vyama vinginevyo, kina Mtenvu mbona hatuzungumzii challenges walizozipata hao kina Mtenvu na Marealle!..Hii ndio maana mkuu..

  Yawezekana kabisa kuwa CCM wameshindwa kuongoza kama chama isipokuwa kama alivyosema Zakumi tatizo sio CCM pekee isipokuwa muundo mzima wa vyama nchini..Intro ya Demokrasia nchini ni sawa kabisa na Nyerere alipojaribu ku introduce Baiskeli kama chombo cha Usafiri wa masikini..He failed kwa sababu ya Watu na mazingira yetu kama alivyoshindwa ktk kuendeleza vijiji vya Ujamaa...More you fail challenges pia zinazidi ugumu...
  Hadi leo hii ndani ya CCM kuna wananchama ambao kisiasa ni Progressive na wapo ambao ni Conservative na wengine Leberal.. Hii yote within one party sasa jiulize hivi vyama nchini vimeundwa kwa kufuata misingi ipi?..
  Ndio maana inakuwa taabu sana kuweza kuelewa nani anaweza kuwa kiongozi mzuri nchini kwa sababu demokrasia yetu ni ya kuchora!..tumeuziwa picha.
   
 13. Andrew Nyerere

  Andrew Nyerere Verified User

  #13
  Nov 29, 2008
  Joined: Nov 10, 2008
  Messages: 3,025
  Likes Received: 1,203
  Trophy Points: 280
  Challenges za Kikwete,tuanze za hivi sasa,halafu,turudi nyuma.
  1.Migomo ya wanafunzi,
  2. Migomo ya walimu.
  3.Mataztizo ya wastaafu wa EAC.

  Matatizo kama haya yangeweza kutanzaliwa kama angeweza kuwaeleza hawa wagomaji kuhusu Fiscal Polic yake. Angewaeleza kwamba anakusanya hela kupitia TRA,na zingine za wahisani,na kwamba,hela zinazotumiwa na Serikali haziwezi kuzidi hizo zilizopo,ama sivyo itatokea Budget Deficit.
  Kama hawa wagomaji wangeelezwa mambo hayo,wangeweka madai yao katika viwango ambayo Serikali ingeweza kuyamudu.
  4. Matatizo yametokea ya ufisadi kwa kuwa Rais Kikwete ameshindwa kuwathibiti watendaji kazi wake wakuu,kama hao Mawaziri.
  5.Yametokea matatizo ya Foreign Poilicy. Hakuna maendeleo yoyote katika mapigano DR Congo. Tunajiuliza Foreign Ministry yetu inawapa wale watu ushauri gani. Certainly tumemsikia Waziri Membe yuko na haraka sana kupeleka majeshi DR cONGO. Jitahada za kuwapatanisha Kabila na Nkunda hazitoshi,au hazipo. Watu wanapigana kule kwa sababu hali ya vurugu,inawatajirisha. Hakuna sababu yoyote kwa nini majeshi yapelekwe kule kwa vile tu Kabila hataki kuongea na Nkunda. Kabila anasema Nkunda anapigana proxy war,vita ya kutumwa na wengine,kwa hiyo yeye atazungumza na yule anayemsaidia Nkunda kupigana.
  5. Matatizo ya Zimbabwe. Vurugu iliyopo Zimbabwe ni kubwa sana. Sasa hivi tatizo lipo kwa Mugabe. Mugabe ndiye anyezuia upatikanaji wa muafaka. Ingawa pia Tsvangirai lazima aelezwe,anapotaka kuithibiiti Wizara ya Mambo ya Ndani,kwamba Polisi lazima wapate uhuru wa kufanya kazi. Fikiria FBI,na Edgar Hoover,jinsi Congressmen kila mara walikuwa wanamtaka Edgar Joover ajiuzulu,lakini Edgar Hoover alikataa kujiuzulu. Lakini ni jambo ambalo halikuathiri utendaji kazi wa FBI. KwA hiyo Tsvangirai asitegemee kwamba ataweza kuithibiti Polisi percent 100.
  7. Matatizo ya ukame na umeme JK alipoanzan kazi.
  8. Matatizo ya mamilioni ya JK ambayo hayajaleta faida kubwa sana kwa sababu Monetary Policy za Kikwete sioy nzuri.
  9. Matatizo ya majambazi alipoanza kazi,ingawa haya ni matatizo ambayo labda yalitoka kwa awamu ya Mkapa.
   
 14. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #14
  Nov 30, 2008
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Ikumbukwe kuwa mengi ya matatizo yaliyopo sasa ni ya muda mrefu na Kikwete ameyarithi kutoka serikali za awamu zilizopita, hivyo hatua anazochukua zinastahili kupongezwa badala ya kubezwa, kwani huko nyuma kabla yake ukiachilia mbali wakati wa utawala wa mwasisi wa taifa hili, hayati Julius Kambarage Nyerere, hatukuwahi kushuhudia utamaduni huu, wa viongozi kuwajibika kutokana na makosa yao au uzembe uliofanywa na watendaji walio chini yao.

  Mtu asionewe haya kwa sababu ya wadhifa wake, rangi, dini ama kabila lake, sheria zetu zisiwe za kibaguzi, mtuhumiwa wa wizi au kiongozi anayetumia vibaya madaraka yake, bila ya kujali ni nani katika jamii, alishashika ama anashika nyadhifa gani, lazima mkono wa sheria umfikie.

  Huko nyuma baadhi ya viongozi wa umma, walijenga kiburi cha kutoambilika hata pale inapoonekana wazi kuwa mambo wanayoyafanya hayana tija kwa taifa, wakijua kuwa hakuna mtu atakayewagusa.

  Hayo yanatokana na gazeti la leo(IPPmedia) na ndio niliyokuwa nikiyasema kama ni challenge basi itakuwa ni uwajibikaji wa Muheshimiwa Kikwete kutoona haya wala yale awe straight forward kwa mfanya kazi wake yeyote yule wa cheo kikubwa au kidogo.
  Hio ndio challenge ambayo mheshimiwa itabidi aivunjie recodi.Maana ni uwajibikaji tu Nyerere hakuwa katika kundi la uwajibikaji zaidi alitaka watu wenyewe wafikirie wenzao,viongozi wawe wachapakazi mara nyingi alikuwa mstari wa mbele katika kupiga vita uvivu lakini hakuweza kumsulubisha mtu ambae alikuwa mvivu na ndio hadi leo tunao akina Ngombale Mwiru akina Kawawa hawa wote walikuwa wahimizwaji tu na wao wakisikika wakisema na kupigia debe Chama lakini hawakuweza kumwajisha mtu.
   
 15. O

  Ogah JF-Expert Member

  #15
  Nov 30, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  ......kwi kwi kwi kwi.........msee taratibu msee
   
 16. Pundit

  Pundit JF-Expert Member

  #16
  Nov 30, 2008
  Joined: Feb 4, 2007
  Messages: 3,741
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Kulinganisha challenge za Kikwete na za Nyerere ni sawa sawa na kulinganisha challenge za kujenga nyumba -kuanzia msingi kwenda juu- na challenge za mtu kufanya maintenance.

  Nyerere alijenga nyumba, Kikwete kaikuta nyumba anafanyia maintenance.

  Kati ya kujenga nyumba na kuifanyia maintenance wapi kuna challenge kubwa?
   
 17. M

  Mkandara Verified User

  #17
  Nov 30, 2008
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Pundit,
  Kwiii! kwiii! kwii! Mkuu hapo tupo pamoja..
  Labda niseme inategemea na Mpangaji maanake hapo katikati Mkapa kauza nyumba sasa hivi wananchi tumepanga!
   
 18. u

  under_age JF-Expert Member

  #18
  Dec 1, 2008
  Joined: Apr 17, 2007
  Messages: 317
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  mmmh mimi ni bwamdogo lakini namie nimeona nichangie japo vijipointi vya uongo uongo, nyerere hata kama alikutana na challenge lakini namna alivyozikabili challenge zake ni unacceptable, nadhani nyerere aliwajaza watu woga hata wakaogopa kumchallenge na pia aliwawekea system ya ujamaa ambayo ilileta dhiki na badili ya watu kufikiria kumchallenge wakawa wanafikiria jioni watakula nini. kwa maoni yangu nahisi nyerere hata kama alikuta challenge lakini hakuzizima kidemokrasia hivyo hatutomuhesabu kwamba kafanikiwa kuzikabili challenge. nakumbuka enzi za nyerere hususan sisi wazanzibari tulijazwa siasa za woga na dhiki na ulikuwa ukijaribu kuikosoa serikali aidha upo hatarini au unaswekwa ndani. lakini wakati huu wa kikwete anakabiliana na challenge ndogo sana lakini ni za wasomi na pia zimekosa woga somehow. si unaona hata under_age leo anajiskia kuandika anachotaka hapa jf. enzi za nyerere hii jf ingekuwa ishasulubiwa zamaaani na nusu yetu tupo mahabusu hapa. conclusion ni kwamba wote wamefeli kuzikabili challenge zao na ndo maana mpaka leo hatujulikani watanzania kama tupo mahututi au marehemu.
   
 19. M

  Mkandara Verified User

  #19
  Dec 1, 2008
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Under_age,
  Mkuu wakati wa Nyerer hata Marekani ilikuwa marufuku kuzungumzia Ukomunist hurusiwi kuingia na gazeti la mao wala picha ya Mao ama gazeti la Kirusi.. utaletewa mkarimani kama vile wewe ni mrusi...
  Dunia nzima siasa zilizotumika ni za vitisho tu kwa hiyo challenges bado zilikuwepo kila kona ya dunia, na huwezi kufananisha Challenges za Reagan na Bush wala challenge za maisha kati yako na baba yako wote tumepitia wakati tofauti na mazingira tofauti..
  Nina hakika leo hii huko Kaburini Nyerere aliambiwa na mwenyezi Mungu kuwa Obama, Mknywa kwa asili amechukua Urais wa Marekani, itabidi wabishane akifikiria kuwa haya ni maneno ya shetani pamoja na kwamba anayemwambia ni Mungu yule anayemuabudu...
   
Loading...