Kipindi cha mwaka 2000 na 2019 Kenya ilipata ajali mbili za ndege ya kampuni mmoja na model mpya zote

chizcom

JF-Expert Member
Jul 31, 2016
7,581
15,718
Sio muamdikaji mzuri ila ajali za ndege kiufupi zinapotokea lazima dunia kujiuliza sana na mpaka chunguzi kufanyika.

Ndege ndio usafiri salama sana.

Tuje kwenye mada

Mwaka 2000

Kenya Airways Flight 431
ilikuwa safari ya ndege ya aina ya Airbus A310-300 ambayo ilikuwa imepangwa kimataifa katikati ya Abidjan-Lagos na Nairobi. Ndege hii ilianguka kwenye bahari karibu na pwani ya Ivory Coast, tarehe 30 Januari 2000, saa 21:09:24 GMT , muda mfupi baada ya kutoka kwa uwanja wa Kimataifa wa Felix Houphouët-Boigny.Ilikuwa na jumla ya watu 179 huku 169 walikuwa ni abiria. Hii ilikuwa ni ajali ya kwanza iliyosababisha vifo iliyokumba Kenya Airways.

Iliyopewa jina Harambee Star, ndege iliyohusika katika ajali ilikuwa aina ya Airbus A310-304, mkia nambari ya usajili 5Y-BEN, ilikuwa imenunuliwa ikiwa mpya na kampuni ya Kenya Airways mnamo 1986.

mwaka 2019

Ndege ya Ethiopia 302 (Ethiopian Airlines Flight 302) ilikuwa ndege ya kimataifa iliyokuwa imepangiwa safari yake kutoka Bole International Airport ya Addis Ababa, Ethiopia, kwenda Jomo Kenyatta International Airport ya Nairobi, Kenya ambapo mnamo 10 Machi 2019 ndege hiyo ilidondoka na kulipuka, hivyo kusababisha vifo vya watu wote 157 (abiria, wahudumu na marubani) waliokuwemo ndani yake.

Tukio hilo limetokea ikiwa ni muda mfupi tu ambapo tukio la kufanana na hilo lilitokea mnamo Oktoba 2018 huko Lion Air Flight 610 Jakarta, Indonesia ambapo ndege ya Boeing 737 MAX 8 (Lion Air Flight 610) ilidondoka muda mchache baada ya kupaa.

Ajali hii inatajwa kuwa ndiyo ajali mbaya zaidi kuwahi kutokea kwa ndege za Ethiopia ambapo ajali hii imelizidi tukio la utekaji wa ndege ya Ethiopia 961 Ethiopian Airlines Flight 961 tukio lililotokea mwaka 1996 huko Komoro, pia ajali hii inatajwa kuwa ndiyo ajali mbaya zaidi kuwahi kuua abiria wengi kwa ndege za Ethiopia.

Tuje kwenye tukio la kwanza mwaka 2000
inasemekana ndege Airbus A310-300 ilikuwa toleo jipya na kutokana kuingia teknolojia mpya yake bado ilikuwa na itilafu ambazo ziliwafanya marubani kushindwa kuendesha na kuanguka gafla.

Japo ilifichwa na kuambiwa ilisababishwa na hali ya hewa.

Wadau wanaweza kutueleza vizuri
 
Kenya Airways Flight 431
ilikuwa safari ya ndege ya aina ya Airbus A310-300 ambayo ilikuwa imepangwa kimataifa katikati ya Abidjan-Lagos na Nairobi. Ndege hii ilianguka kwenye bahari karibu na pwani ya Ivory Coast, tarehe 30 Januari 2000, saa 21:09:24 GMT , muda mfupi baada ya kutoka kwa uwanja wa Kimataifa wa Felix Houphouët-Boigny.Ilikuwa na jumla ya watu 179 huku 169 walikuwa ni abiria. Hii ilikuwa ni ajali ya kwanza iliyosababisha vifo iliyokumba Kenya Airways.

Iliyopewa jina Harambee Star, ndege iliyohusika katika ajali ilikuwa aina ya Airbus A310-304, mkia nambari ya usajili 5Y-BEN, ilikuwa imenunuliwa ikiwa mpya na kampuni ya Kenya Airways mnamo 1986.
Hii ndiyo ile ilianguka kwenye mikoko?
 
Hizo ajali zilitokea mfululizo ikabidi uchunguzi wa kina ifanyike ilionekana toleo Hilo lilikuwa na hitilafu kwenye mfumo yao
 
Back
Top Bottom