Kipindi cha Mpito kuelekea hatma ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kipindi cha Mpito kuelekea hatma ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Abba, Apr 24, 2011.

 1. A

  Abba Member

  #1
  Apr 24, 2011
  Joined: Jul 30, 2007
  Messages: 40
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Naandika haya nikitafakari maduduku, malalamiko ya wananchi hususani wazanzibari kwa upande mmoja kwamba muungano unanyonya/unakwaza na kufifisha maendeleo ya sehemu hii ya muungano n kwa upande wa pili wa baadhi ya watanganyika wameanza kupoteza uvumilivu na malalamiko ya wazanzibari wakati wao wakiamini kwamba wamekuwa wanabebeshwa mzingo ambao hawastahili(umeme wa bure,kodi zisizolingana, mgawanyo wa mapato usistahili etc). Katika haya manunguniko yote serikali zote za ccm zimekuwa ziweka masuala ya kero za muungano kazi ya kufanywa na serikali itakayo kuja.

  Ni lazima tukubali kwamba ni bora kuuzungumza muungano na kero zake mapema ilitujue kama tunaweza kuuokoa katika hali dhairi ya kuweza kuvunjika au ni vipi tunaweza kuuboresha.

  Mimi nina mawazo na mawazo haya ni mpango wa muda wa miaka kumi- tuuite transition period wa kuutafakali kama kweli kuna faida za wazi za muungano huu au hakuna na hivyo tuuvunje. Katika kipindi hichi cha transition napendekeza haya yafanyike:

  1.Zanzibar iruhusiwe kukusanya kodi zake zote pamoja na kodi ya makapuni chini ya TRA-ZnZ kwa uangalizi wa TRA-Muungano

  2.Zanzibar ighalimie kuendeshwaji wa serikali yake bila kusaidiwa na serikali ya muungano

  3.Zanzibar ilipie bei harisi ya umeme kutoka bara na ilipe kwa muda unaotakiwa na ikichelewa watozwe riba

  4.Bidhaa zote zinazotoka zanzibar kuingizwa bara zilipe kodi kwa mfumo wa EA custom union. Hivyo hivyo bidhaa zote zinazotoka bara kwenda znz ziattract same kodi

  5.Baraza la wawakilishi lipewe mamlaka chini ya waziri wa fedha ya kupanga, kukusanya na kutumia kodi

  6.Wizara za muungano za ulinzi, mambo ya nje na mambo ya ndani zibaki chini ya serikali ya muungano katika kipindi cha mpito kwa nia njema ya kulinda usalama na sera ya mambo ya nje kabla uamuzi wa mwisho

  7.Ifanyike sensa ya wanzanzibari wote wa bara na visiwani kwa kupata record sahihi. Vile vile ifanyike sensa ya wabara na hizi ziwe katika daftari tofauti

  8. Kufanya referrendum baada ya kipindi hiki cha mpito kama walivyo fanya sudani ya kusini kuhusu hatma ya muungan na kura ya wanzanzibari iwe ndiyo final say wakati kura ya wa bara iwe kwaajiri ya rekodi - sio na uamuzi katika hatma ya kujitenga au kutojitenga.

  9. Matokeo ya kura yaheeshimiwe na pande zote na iwapo kura ya wanzanzibari itaamua kuvunja muungano uwekwe mchakato wa kuzitoa raslimali za zanzibar kwenye muungano na mwishowe muungano uvunjwe.

  Ni mawazo yangu katika kipindi hiki cha mpito watanganyika na wazanzibari wakuwa wameona, wamepima na kubaini kama kuna faida au hakuna katika muungano!
   
 2. A

  Albimany JF-Expert Member

  #2
  Apr 24, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 279
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 45

  Mbona unapata tabu wakati mambo yote yengeamuliwa na hiyo kura ya maoni tu?

  Ianze kura ya maoni kuulizwa nchi mbili hizi kua zinahitaji muungano au hazitaki?

  Na kwa kuwaepushia gharama ya kura ya maoni ndugu zetu Watanganyika,napendekeza kura ianzie zanzibar kwakua nina uhakika Muungano utakataliwa.
  Kwahio hakutahitajika kuingia gharama za ziada Kwa siri-kali ya Tanganyika.
   
 3. Makaimati

  Makaimati JF-Expert Member

  #3
  Apr 25, 2011
  Joined: Apr 4, 2011
  Messages: 462
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Tupige kura kuulizwa kama tunataka uhuru wetu?

  Kwani tulipounganishwa tuliulizwa kama tunataka au la"

  Uvunjike tu tugawane mbao.
   
 4. A

  Abba Member

  #4
  Apr 25, 2011
  Joined: Jul 30, 2007
  Messages: 40
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sidhani kama umetafakali hoja iliyopo. Kwa mtazamo wako baraza la wawakilishi linaweza kutoa hoja ya kuvunja muungano na kumshinikiza rais kuitekeleza lakini haitakuwa imewashirikisha wananchi.sina taabu kama mwishowe watu watanzania wataamua kuuvunja muungano. Kwangu mimi uwepo utaratibu muafaka kuelekea kupiga kura ya maoni ikiwa ni pamoja kipindi cha kutafakari! Southern Sudan wamefanya kwanini sisi tushindwe?
   
 5. Makaimati

  Makaimati JF-Expert Member

  #5
  Apr 25, 2011
  Joined: Apr 4, 2011
  Messages: 462
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0

  Sudan ilikuwa nchi moja, Zanzibar ilichakachuliwa, ndio sababu
   
 6. Kimilidzo

  Kimilidzo JF-Expert Member

  #6
  Apr 25, 2011
  Joined: Jan 3, 2011
  Messages: 1,346
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 135
  Baada ya kusoma maoni ya jamaa wa kule Zenji wanaitwa MUWAZA nimeshawishika kuwa huu uonevu unaofanywa na watanganyika dhidi ya wazanzibar haukubaliki kwa nchi ambazo zilikubaliana kimsingi kuungana halafu nchi moja inajifanya kuwa kinara wa mwingine. Ingawa mimi binafsi sijawahi hata kukanyaga Zanzibar lakini haya mambo yanayolalamikiwa na wazanzibar yamenifanya niwaonee huruma na kupendekeza heri tuvunje muungano tu kila nchi ijiendeshe yenyewe licha ya kuwa CCM wanang'ang'ania sana muungano lakini hawauenzi. Hebu cheki huu ubazazi;

  MUWAZA inashauri kwamba pana haja muhimu wa haya yote kutizamwa upya, hii inatokana na ukweli usiopingika kwamba kiini cha tatizo ni Muungano wenyewe na sio kero za Muungano tu. Kwa mfano:-
  • Muundo wa kumpora Rais wa Zanzibar Madaka ya kuwa Makamo wa Kwanza wa Rais na kuanzishwa kwa cheo bandia cha Mwenza ni kati ya hatua haramu za kuvunja Makubaliano ya Muungano
  • Kumgeuza Rais wa Zanzibar kuwa Waziri wa Kawaida wa Baraza la Mawaziri la Muungano ni kitendo kingine cha kuvunja Katiba
  • Kumshusha hadhi Rais Wa Zanzibar na kumkuza hadhi Rais wa Tanganyika ingawa hawa ni Ma- Rais wa nchi mbili huru katika suala hili la Katiba Mpya ni hatua isiyokubalika kwa Wazanzibari
   
 7. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #7
  Apr 25, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,475
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Kero za muungano tunaogopa kuzijadili waziwazi ndio maana muungano huu upo katika hatari ya kuvunjika!
   
 8. Kimilidzo

  Kimilidzo JF-Expert Member

  #8
  Apr 25, 2011
  Joined: Jan 3, 2011
  Messages: 1,346
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 135
  Wazanzibari walipiga hatua nzuri tu baada ya mapinduzi. Hebu cheki hapo; Waziri Mkuu wa Zanzibar baada ya uhuru wa 1963, Sheikh Hamad Shamte (kulia) akiiwakilisha nchi yake kwenye Umoja wa Mataifa. Tusiwanyime haki zao wala kuwadharau, tuwape nchi yao.

  [​IMG]
   
 9. Pharaoh

  Pharaoh JF-Expert Member

  #9
  Apr 25, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 843
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Wazanzibari wanadanganywa na pesa za beach, watalii wataliano wanaojaza beach zao nzuri kupumziko, kuogelea na kuota jua, wengi wa mawaziri wa sasa walikuwa beach boys tu, yaani machinga wa kuwauzia vitu wazungu beach, lakini je bara ikizifungua beach zake na visiwa vyake mfano Mafia, Bongoyo, Mbudya na nyingine nyingi na kushawishi makampuni makubwa ya Italy kuwekeza bara kunako urahisi zaidi kwao na hamna udini, wazanzibari hapo watasemaje? zanzibar inaiona bara mpenzani wa kufa na kupona, wawekezaji wanaambiwa bora waende kuwekeza kenya sio bara, Tanzania bara wanaiona zanzibar kama ndugu, rafiki na mwenza wa kweli, na inadhihirisha wanapendwe na kuheshimiwa wazanzibari bara, ilhali watanzania bara zanzibar wanatukanwa kila pahala, kunyimwa fursa zote na kuonewa ovyo.
   
 10. A

  Abba Member

  #10
  Apr 25, 2011
  Joined: Jul 30, 2007
  Messages: 40
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ningependa kujua wewe ni mtanganyika au mzanzibari. Na kama ni mzanzibari, je we unatoka unguja au pemba? Je unaishi Zanzibar au bara? Haya ni maswali ya msingi na siyo wanzanzibari wote watatoa jibu moja so ni muhimu watu wakapewa muda wa kutafakari na kuamua. Na katika hili watanganyika nao waulizwe japo hawatakuwa na kura ya veto endapo wanzanzibari wataamua kujitenga! Kwa taarifa yako Sudan hajawahi kuwa nchi moja kwenye mioyo ya wa sudan wa kusini tangia kupata uhuru! Au ningekuuliza swali nini maoni yako kuhusu kujitenga sudani ya kusini? Je ungependa waendelee kuwa sehemu ya sudan ya kaskazini?
   
 11. Edward Teller

  Edward Teller JF-Expert Member

  #11
  Apr 25, 2011
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 3,818
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Kwa mtazamo wangu sioni umuhimu wa kuwa na sherehe ya muungano-
  maana naona muungano wenyewe una walakini sana-ni bora viongoz wangekaa na kusolve matatizo ya muungano ikibidi waufunje kuliko kwenda na kuangalia halaiki ya watoto ambao wanapigwa na mvua na jua na kuimba nyimbo bila kujua umuhimu wa kitu wanachoimba
  sherehe za muungano zimekuwa ni shoo za halaiki ya watoto ambao wao kwa kuwa hawajui lolote kuhusu muungano wanatumika kuzuga taifa kuwa watoto wanasheherekea kwa furaha-
  inatakiwa sherehe za muungano viongozi watupe progress za mambo tunayoshirikiana na kama yameleta faida au la
  lakini kama itakuwa ni swala la kuangalia halaiki na gwaride ni bora hizi sherehe zisiwepo na muungano wenyewe pia usiwepo
  ngoja tuone hio kesho watakuwa na kitu gani kipya zaidi ya halaiki na ngwaride
   
 12. N

  Nonda JF-Expert Member

  #12
  Apr 25, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,960
  Trophy Points: 280
  Mkuu.

  Kwamba muungano ni utata mtupu,hili halina ubishi.
  CCM wana sera ya serikali mbili kuelekea moja...hii sera haijafutwa.
  Hatua gani za kutatua kero za Muungano....next to null.
  Kero zinaongezeka?....ndio.

  Kuna nchi nyengine karibu na Tanzania na Zanzibar zenye beaches?
  Kenya, Mozambique, South africa, Sychelles, Mauritius, Reunion...jee watalii wanazitembelea nchi hizo?...ndio.

  kwa nini hatujazitengeneza na kuzikuza beaches za "bara" ili kuvutia watalii zaidi? Ni kwa sababu tunawaonea huruma "ndugu" zetu wa Zanzibar ili wapate soko la utalii?

  Muungano unawanuafaisha wachache tu katika Tanganyika pia huko Zanzibar.

  Na kuachwa Muungano uendelee kuwepo katika hali na muundo huu wa leo, basi tunakaribisha maafa siku za mbele.
   
 13. K

  Kilembwe JF-Expert Member

  #13
  Apr 25, 2011
  Joined: Aug 19, 2009
  Messages: 1,132
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Siku huu Muungano ukivunjwa nitafurahi sana maana Zanzibar imekuwa like thorn in the skin, Zanzibar ni mzigo mzito kwa bara ni waongo tu wazanzibar wanapolialia kuwa wananyonywa na bara! nenda TANESCO leo kawaulize ni nani wako katika top three ya wadaiwa sugu! na sijui wanataka nini zaidi wazanzibar tayari wana bebdera yao, wana wimbo wao wa taifa! waende tu!
   
 14. Mahesabu

  Mahesabu JF-Expert Member

  #14
  Apr 25, 2011
  Joined: Jan 27, 2008
  Messages: 5,043
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  DHAMBI YA UBAGUZI NI DHAMBI MBAYA KABISA......ZANZIBAR IKIJITENGA ...KWA SABABU YA ULEVI TU...HASA ULEVI WA MADARAKA.....HAWATABAKI SALAMA......WATANGUNDUA KUNA ........WAPEMBA NA WAUNGUJA ........KISHA WATAGUNDUA KUNA WAZANZIBARI NA WAZANZIBARA.....bado hawatabaki salama....wataona kuna WASHIRAZ NA WA-YEMEN.....
  DHAMBI YA UBAGUZI ITAENDELEA
   
 15. R

  Rangi 2 Senior Member

  #15
  Apr 25, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 171
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Mambo mengine Bwana! Hivi hayo mambo yaliyoongezwa baada ya muungano kuundwa, yalifanywa kwa SIRI?
  Je, mbona kuna wakati rais wa Jamhuri ya Muungano alitoka Zanzibar(Mwinyi) na hivyo kukawa na Rais wa JMT Mzanzibari na rais wa Zanzibar mzanzibar na sikusikia Mtanganyika akilalamika?
  Hebu angalia kwa sasa Makamu wa rais, Waziri wa ulinzi na Mambo ya ndani wote ni wazanzibari (hizo zote ni nyadhifa muhimu).
  In Short:
  Wazanzibari wameuchoka muungano. Muungano utavunjika tu kama sio leo ni kesho.
  Ni kheri uvunjike leo ili tuepukane na mambo ya ajabu ajabu.
   
 16. Joss

  Joss JF-Expert Member

  #16
  Apr 25, 2011
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 729
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Ukivunjika tutakuwa na uhusiano wa kibalozi na nchi jirani ya Unguja. Sidhani kama nchi ya Pemba itakuwa interested.
   
 17. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #17
  Apr 25, 2011
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Tuliingia mfumo wa vyama vingi bila kujiandaa ipasavyo. Tukataka kuwa na katiba ileile wakati hali halisi ilikuwa ni kuundwa kwa katiba mpya. CCM kwa uroho wao wa madaraka na uchoyo wa kushirikiana na wananchi wasiokuwa CCM katika mambo nyeti, wakaona kama makamu wa rais atakuwa rais wa Zanzibar basi endapo chama ambacho si CCM kitashinda kule na CCM kushinda huku basi watakuwa na serikali yenye kuwakilishwa na vyama viwili tofauti vyenye sera tofauti na hivyo kutumia mwanya wa wao kuwa na bunge kuweka viraka katiba ili ikidhi mahitaji yao ya kumnyima rais wa Zanzibar kuwa makamu wa rais. Tulitakiwa kuwa na serikali ya shirikisho, yaani Tanganyika rais wake, Zanzibar rais wake na JMT rais wake na makamu wake ambao kazi yao kubwa ingekuwa ni kusimamia mambo yote yaliyoamuliwa kuwa ya muungano, ikiwemo ulinzi na usalama wa mipaka ya nchi, mambo ya nje, fedha etc. Kungekuwa na federal court, federal congress etc, at the same time Tanganyika inakuwa na bunge lake kama ilivyo Zanzibar. Hakuna ubaya kwenye hilo, ila sijui kwa CCM wanalikataa hili ili hali wanajua wazi kuwa wakati wa kutumia mabavu kuulinda muungano umekwisha, sasa ni wakati wa maridhiano.
   
 18. Makaimati

  Makaimati JF-Expert Member

  #18
  Apr 25, 2011
  Joined: Apr 4, 2011
  Messages: 462
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kwanini unataka kujua hayo ABBA mdogo wangu?

  Kuhusu suala lako la ningependa nini kuhusu Sudan, jibu lake ni very simple.

  Kama wao Wasudan ya Kusini hawajawahi ndani ya miyo yao kuwa nchi moja, hata mimi mpaka sasa siamini katika moyo wangu kuwa Tanzania ni nchi moja, ni kuzidiwa nguvu tu kama ilivyowahi kuwa Sudan Kusini albeit katika mazingira tafauti.

  Mkuu umekuwa too personal lakini kwa sababu unataka kujua, i believe in self determination na ndio maana nataka Zanzibar iondokane na huu "muungano" feki ili ijiamulie mambo yake wenyewe.
   
 19. M

  Mtabe JF-Expert Member

  #19
  Apr 25, 2011
  Joined: Sep 20, 2010
  Messages: 675
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mzee hakuna haja ya transition period wala transition state na hayo mambo yako 10
  ya mpito ni upuuzi mtupu na ni ya kupoteza mda.

  Kuvunja muungano hakumaanishi ugonvi so kura ya maoni inatosha kuamua khatma ya muungano na ifanyike znz tu tutawapa majibu yakutosha.
   
 20. Makaimati

  Makaimati JF-Expert Member

  #20
  Apr 25, 2011
  Joined: Apr 4, 2011
  Messages: 462
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Na hatulipi na hamna vya kufanya.
   
Loading...