Kipindi cha Mama Samia ndio kipindi cha Wakulima wa Mazao ya Nafaka kutoka kimaisha

Mkulima na Mfugaji

JF-Expert Member
Jul 26, 2013
1,013
1,634
Tokea Awamu hii iingie Madarakani naona imeamua kuwachia wakulima hasa wa nafaka wanufaike, kila siku ukienda sokoni bei ya nafaka iko juu, kwani mipaka imefunguliwa na ukichanganya na Athari za mabadiliko ya Tabia ya nchi.

Kama Mkulima umeweza kuhifadhi angalau gunia 20 za Mahindi mwezi February gunia litakua si chini ya Tsh 150000.

Cha msingi kipindi hiki wakulima tutumie Improved seeds na tupandè na Mvua za Kwanza, mbegu hizi hazikuangushi kamwe na mimi ni shuhuda wa hili, nimezipanda masika na vuli na hazijaniangusha.
 
Bandari ya Mtwara safari hii haitumiki kusafirisha korosho, Korosho zote zinasafirishwa kupitia bandari ya Dar es Salaam
 
Improved seed za mahindi ni zipi mkuu. Wiki mbili zilizopita nimetoka kupanda pioneer mf zimeshaota tayari tatizo mvua inaleta ukakasi.
 
Bandari ya Mtwara safari hii haitumiki kusafirisha korosho, Korosho zote zinasafirishwa kupitia bandari ya Dar es Salaam
Walamba asali hawana muda nayo tena..ndio inaenda kujifia...wakimaliza kusafirisha makaa ya mawe ndio kwisha habari yake.

#MaendeleoHayanaChama
 
Omba hali ya hewa iwe mbaya, ikiwa nzuri na kwa.majirani basi hayo mahindi utatupa.
 
Back
Top Bottom