Kipindi cha Jicho pevu Azam TWO ya Azam TV

Abuu Kauthar

JF-Expert Member
Jul 10, 2011
4,178
6,237
Hiki kipindi ni cha kiuchunguzi lakini leo mara ya pili naona habari za kenya tu, mara ya kwanza niliona walivyochambua usanii wa police wa kenya katika sakata la uvamizi wa waliowaita magaidi katika jengo la West Gate...police walivyokwapua pesa na mambo mengine mengi.
Leo ni nimeona namna walivyochambua tukio la kifo cha aliyekuwa waziri(sikumbuki wizara aliyokuwa) marehemu Saitoti hapa pia jeshi la polisi likionekana kuhusika moja kwa moja.
Kwa nini na tanzania kusiwepo waandishi wa namna hii kufichua uovu wa jeshi la polisi katika matukio mbalimbali kama kuuawa kwa Daudi Mwangosi, Deo Filikunjombena wengine wengi waliouawa kwa njia za utata???
 
Azam watafungiwa maana Paruwanja na Jaramandia za Mohamed Ali ni mwiba,Kina Nairoberry,MK254 mwambieni moha aje kufanya uchunguzi wa kifo cha Deo filikunjombe na nyerere warushe ktn.
 
Paruwanja la mihadarati ni noma,niliangalia zote 4, daaah,sijui kwa bongo uchunguzi kama huu itakuwaje
 
Mh!? Kung'olewa meno bila ganzi nako kutahusika maana wabongo tuko njema kwenye ung'oaji wa meno.
 
thubuttuuu yakeeee! alijaribu jerry muro nafkiri uliona kilichomtokea

anayeweza kuthubutu labda sam mahela ila bado mwoga mwoga yule
 
Waziri wa Ulinzi aliuwawa na kenge LA wauza unga!! Hapa bongo ni kitu ambacho hamna mtu Mwenye uthubutu huyu Sam mahela awezi kumfikia Moh hata chembe!! Huyu jamaa Alisha wahi kupiga kambi mpakani na Tanzania Huko Tarakea Rombo akifanya uchunguzi wa Malori yanayo pitisha madawa ya kulevya na bangi % 100 alifanikiwa kunasa!! Huyo Moh ni nuksi aniingia sehemu ambayo haifai kuingia!! Na Alisha pigwa marufuku kuingia Ikulu ya Kenya!!!
 
Kwa uchunguzi ule wa mohamad Ali ungekuwa bongo angepelekwa mabwepande dental hospital fasta
 
Huwa nikianza kuangalia Jicho Pevu YouTube huwa nahakikisha mambo mengine yote nimemaliza.
 
Back
Top Bottom