Kipindi cha Jahazi CLOUDS FM

East African

JF-Expert Member
Nov 27, 2013
704
989
Nilikuwa mpenzi mzuru wa kufuatilia kipindi cha Jahazi cha Clouds FM hasa wakati kikiendeshwa na Gadna, lakini tangu aondoke hakuna kinachoendelea hapo. Ni kelele za watangazaji hasa Kibonde anaboa hazi basi maana anajifanya anajua kila kitu.

Kipindi kinaanza saa 10;00 hadi 1;00 uck takribani masaa 3 lakini hakuna cha maana tunachoweza kujifunza. Ni segment moja tu ya taarifa ya habari ya saa 12;00 ndiyo inayovutia, lakini mambo yanayobaki ni porojo tupu za Kibonde na sasa amewaharibu hata wale wenzake ambao wanaonekana kuwa na kauelewa kidogo.

Nakuomba mkurugenzi wa matangazo na vipindi uliangalie hili kwani unapoteza washabiki wengi sana katika kipindi hiki cha Jahazi. Hakuna jipya zaidi ya kusikia salamu za Kibonde(ASALAM ALEIKUM na habari za town ambazo eti anazisoma kutoka katika magazeti ya asubuhi ambayo habari zake zisha expire.

Pamoja na hayo napenda kumpongeza sana sana Mtangazaji maarufu Millard Ayo wa kipindi cha Amplifaya kweli huyu dogo yuko safi sana hana masihara katika kipindi chake na ninapendekeza apewe tuzo ya kipindi bora zaidi cha CLOUDS FM.
 
kwani mwenye kipindi ni nani hasa!!?mana kila kitu yeye hadi wenzake hawasikiki?ana bore sana aisee,
 
Umeona ee? mimi nilkuwa mpenzi sana wa hiki kipindi hasa ule mchanyato wa Gadner na Kibonde ulivutia sana, baada ya Gadner kuondoka na Kibonde kujiingiza katika siasa za kushabikia ujinga, basi sinaga hamu tena, nikahamia kipindi cha taarifa za jioni za radio one, Kibonde ameshakuwa mzigo Clouds na amejiharibu mwenyewe
 
Nilikuwa mpenzi mzuru wa kufuatilia kipindi cha Jahazi cha Clouds FM hasa wakati kikiendeshwa na Gadna, lakini tangu aondoke hakuna kinachoendelea hapo. Ni kelele za watangazaji hasa Kibonde anaboa hazi basi maana anajifanya anajua kila kitu.

Kipindi kinaanza saa 10;00 hadi 1;00 uck takribani masaa 3 lakini hakuna cha maana tunachoweza kujifunza. Ni segment moja tu ya taarifa ya habari ya saa 12;00 ndiyo inayovutia, lakini mambo yanayobaki ni porojo tupu za Kibonde na sasa amewaharibu hata wale wenzake ambao wanaonekana kuwa na kauelewa kidogo.

Nakuomba mkurugenzi wa matangazo na vipindi uliangalie hili kwani unapoteza washabiki wengi sana katika kipindi hiki cha Jahazi. Hakuna jipya zaidi ya kusikia salamu za Kibonde(ASALAM ALEIKUM na habari za town ambazo eti anazisoma kutoka katika magazeti ya asubuhi ambayo habari zake zisha expire.

Pamoja na hayo napenda kumpongeza sana sana Mtangazaji maarufu Millard Ayo wa kipindi cha Amplifaya kweli huyu dogo yuko safi sana hana masihara katika kipindi chake na ninapendekeza apewe tuzo ya kipindi bora zaidi cha CLOUDS FM.

east african fm oooops sorry east african.....wewe unaona hivyo...kuna wenzio wanaona kinyume na wewe na wanaweka matangazo ya mamilioni.......
 
mkuu naunga mkono hoja, hata mie tangu atoke gadna sina hata hamu ya kusikiliza kipindi hicho, kinabore tu, sijui huwa hawana kitu cha kuongea au uwezo na uelewa mdogo wa mambo, mbona vipindi vingine vinavutia kama power blackfast, leo tena, na XXL, kwani elimu ya kibonde ikoje?, mwisho nampongeza sana millard ayo, kijana huyu anajua sana kupangilia matukio na jinsi ya kuendesha pia kipindi, kusaga mulika sana jahazi, watakuharibia kituo chako cha redio
 
Enzi za Gadna nilisikiliza sana kipindi cha Jahazi, lakin hii leo kila nikijitahidi, papuu, sipati cha maana.

Nkahamia daladala ya EA Radio.

Japo baadhi ya segments za leo tena ya Dina Marios huwa nasikiliza.
 
Back
Top Bottom