Kipindi cha DK 45 cha ITV ni mdomo wa serikali?

babayah67

JF-Expert Member
Mar 28, 2008
493
79
Kuna kipindi kinachorushwa kila siku ya Jumatatu mida ya saa tatu na nusu usiku kiitwacho Dakika 45, hivi jamani kipindi hiki kimeanzishwa hasa kwa lengo gani???.

Toka kimeanzishwa kipindi hicho kimekuwa kikiwahoji viongozi wa serikali hasa mawaziri ambao wamekuwa wakieleza sera za wizara zao na pia wamekuwa wakiendesha propaganda za kisiasa dhidi ya vyama vya upinzani.

Kwa kuzingatia maadili ya vyombo vya habari nilitarajia kwa mwongozaji wa kipindi hicho cha Dk 45, kuandaa vipindi vinavyowahusisha viongozi wa upinzani kila wanapokuwa wamehusishwa au kutajwa kuhusika na njama zozote dhidi ya serikali, badala yake hakuna kitu kama hicho.Je ule msingi mzuri wa uandishi/utangazaji wa kutoa habari toka pande zote mbili uko wapi hapa???.

ITV jamani katika hili mnasemaje???
 
Kuna kipindi kinachorushwa kila siku ya Jumatatu mida ya saa tatu na nusu usiku kiitwacho Dakika 45, hivi jamani kipindi hiki kimeanzishwa hasa kwa lengo gani???.

Toka kimeanzishwa kipindi hicho kimekuwa kikiwahoji viongozi wa serikali hasa mawaziri ambao wamekuwa wakieleza sera za wizara zao na pia wamekuwa wakiendesha propaganda za kisiasa dhidi ya vyama vya upinzani.

Kwa kuzingatia maadili ya vyombo vya habari nilitarajia kwa mwongozaji wa kipindi hicho cha Dk 45, kuandaa vipindi vinavyowahusisha viongozi wa upinzani kila wanapokuwa wamehusishwa au kutajwa kuhusika na njama zozote dhidi ya serikali, badala yake hakuna kitu kama hicho.Je ule msingi mzuri wa uandishi/utangazaji wa kutoa habari toka pande zote mbili uko wapi hapa???.

ITV jamani katika hili mnasemaje???
Kwa kweli mimi binafsi naona kwamba ITV ni wabunifu wa ukweli. Tatizo siyo kipindi lakini Tatizo ni mwongoza kipindi, huyu jamaa badala ya kuhoji yeye kazi yake ni kusombwa na upepo wa majibu yanayotolewa na wale anaowaalika.

Na hili siyo tatizo la Semunyu peke yake bali ni la waandishi wengi wa tanzania ndiyo maana wakati mwingine Ben Mkapa alikataa kuhojiwa na waandishi wa habari wa bongo kwa miaka yote aliyokaa Ikulu. Hawa waandishi wetu hawasomi kabisa kabla ya kwenda kuhoji mtu yeyote sasa utawezaje kuwa na maswali ya msingi kama hukusoma juu ya kile unachokwenda kuhoji?
 
Propaganda ni Uongo unaofanana sana na ukweli. Vipindi vingine vimetayalishwa kwa misingi ya propaganda. dakika 45 ni propaganda ya CCM madarkani. Pima hadi sasa miaka 50 karibu, je inafanana na hayo yanayo semwa, BLA BLA nyingi sana, utegemezi mwingi sana hauna anyeonyesha njia hata mmoja. Ya Mwalimu Dr. JKN yameliwa na mdumange tu Mwenyezi MUNGU amrehemu Amen........
 
mara ya kwanza nilikuwa nakifuatilia hicho ila baadaye nikaona kinanijaza ujinga,nasikia viongozi wa serikali wanaweka oda kwenda kwenye hicho kipindi tofauti na vipindi vingine kama 'malumbano ya hoja'chanel 10 on monday,kipima joto ambapo wananchi wanahoji vitu na watangazaji wake wanauwezo mkubwa wa kumbana mtu,hivyo vipindi vinahusisha watu mbalimbali kwa kipindi kimoja
hicho kipindi ni mdomo wa serikali ya thithiemu la sivyo mtangazaji angekuwa ameisharekebishwa
briiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii
 
Jamani kweli tunapoteza muda na baadhi ya mijadala .ITV kama wanaweza kuchakachukua picha za taarifa ya habari na wasiombe msamaha unategemea nini kwenye mambo mengine ? Si ni Mengi huyu huyu TV ilishawahi kuonyesha mauaji ya Rwanda na huko Burundi wakati wa uchaguzi muhimu sana kwa maisha ya Watanzania ?

Ukiondoa hili wewe umemuona Chuwa UN kule anashangaa kila kitu link ilikuwa hapa hadharani leo unategemea watu wa aina ile wawe na maswali ya maana kwa hawa wanao watumikia ? Tanzania tuna safari ndefu sana kwa kweli .
 
Magamba hayo yanatangaza "mafanikio" ya 50yrs ya uhuru wa Tanzania, Tanzania Bara, au marehemu Tanganyika
 
Nashukuru watazamaji wameshtuka kama mimi nilivyoshutuka na kipindi hicho ya cha dk 45. Kwa kweli kipindi hicho hakina tofauti na kununua ukurasa kwenye gazeti na kuandika lolote lililo upande wa mnunuzi wa ukurasa. Ilibidi kipindi kiwe balaced, tuambiwe na upande wa pili. Mfano kama week hii anakuwepo waziri wa katiba na sheria basi wiki inayofuata awekwe waziri kivuli au mwanaharakati yeyote mwenye uelewa wa wizara hiyo. Au aanze waziri kivuli kisha waziri mhusika ajibu hoja. Vinginevyo wote wawekwe kwenye meza moja watueleze kwa kulumbana kwa hoja. Au kama hivyo haiwezekani basi watupe wasaa wa kupiga simu na kuhoji hayo yanasemwa kuliko ilivyo sasa inakuwa kamavile ni mahubiri ya kanisani ambayo audience inatakiwa kusikiliza tu.

Nakumbuka kuna kipindi alikuwepo waziri Membe, aliongea jinsi serikali isivowatambua "waasi"wa Libya, kwamba ni wahuni tu wenye pick up! Lakini sasa tunaambiwa hata AU inawatambua, tumemwona hata Rais wetu amepiga picha na kiongozi wa waasi hao huko New York. Sasa ni kipi kimebadilika? Kipindi cha dk 45 ni ubunifu mzuri kama utafanyiwa marekebisho, ila kama kilivyo sasa hakipendezi!
 
Watawabeba mwisho wa siku watagungua hawabebeki........we acha wafu wazike wafu wenzao
 
Niliangalia kipindi alipohojiwa magufuli na nadhani membe! Since then cjawah tena ku-tune..! Mimi nadhani hicho kipind ni moja ya dept zilizoanzishwa na Nnnauye Jr katika kitengo cha Itikadi na Uenezi.
 
Mwizi na nayefanikisha wizi wote ni wakosefu. Imebidi ITV itafute namna ya kujiweka karibu na magamba.
 
muongoza kipindi hajui kuulza maswali

Sio kweli kwamba muongoza kipindi hajui kuuliza maswali, bali maswali huwa yanaandaliwa na kupelekwa kwa mhojiwa mapema naye kuyatafutia majibu.

Yangekuwa ni maswali ya papo hapo ungeona wanavyo jikanyaga kanyaga. Kama waziri mkuu alitaka apelekewe maswali atakayoulizwa kwenye kipindi cha maswali kwa waziri mkuu mapema ili ajiandae kwa majibu unategemea nini kwa mawaziri kama si usanii kama huu unaofanywa na itv.
 
Vyombo vyetu vya Habari ni bure kabisa hususani hii ITV ndio uozo mtupu ,hata haifai kujadiliwa kwa ukiukwaji wa taaluma ya kutoa habari.
Siku zote wamekuwa wakionyesha wazi kuwa wao wanaegemea upande mmoja pasipo kujali facts.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom