Kipindi cha BARAGUMU channel ten chazorota baada ya kukosekana kwa Salum Mwalimu

Tuko

JF-Expert Member
Jul 29, 2010
11,178
7,319
Kiukwel hiki kipindi cha asubuhi kilikuwa kimeanza kupata umaarufu kutokana na juhudi zilizokuwa zinafanywa na mwendeshaji Salum Mwalimu. Hata hivyo huyu jamaa kwa sasa hayupo (sijui yametimia niliyowahi kutabiri humu kuwa siku zake Channel ten zinahesabika?).
Jamaa anayeendesha sasa, David Ramadhan ameshindwa kabisa kukipa chachu, kwani anapresent hoja zisizo na hamasa sana na analeta watu wasio na impact sana kwa jamii kama alivyokuwa Mwalimu.
 
Salum Mwalim amevutwa na dadayake mmoja ana cheo cha juu sana vodacom ,tumemkuta pale Vodacom ndio meneja wa mahusiano ya jamii....kama sijakosea ila amelamba shavu!!!
 
duhu, yaani kwenda voda ndio kulamba shavu? wewe unaosha magari nini?


Mbona uko na mtazamo hasi na Vodacom? Hujui kuwa communication sector na banking vinaongoza katika ku attract new skills kwenye HR industry na kwamba Vodacom ni market leader (44%) ya cellular business?
 
mbona uko na mtazamo hasi na vodacom? Hujui kuwa communication sector na banking vinaongoza katika ku attract new skills kwenye hr industry na kwamba vodacom ni market leader (44%) ya cellular business?

kuna takwimu zozote halisi zinazoweza kuthibitisha kuwa
1)vodacom ni leading cellular network?
2)vodacom inakamata 44% ya cellular business?

Kwani idadi ya wateja vodacom inaojiboast nao ni cumulative number ya lines sold, wengi wanamiliki au wamepata kumiliki zaidi ya line moja za vodacom, including myself ambae tangu 2002 nimepata kuwa na line 5 za voda vipindi tofauti tofauti, pili hivi sasa wengi simu zetu za mchina au zile za promosheni so tunamiliki zaidi ya line moja, je hilo haliwezi kufanya ile tofauti ya idadi ya wateja baina ya mtandao mmoja na mwingine kuwa ndogo sana?
 
Back
Top Bottom