Kipindi cha Al Jazeera Witness Special kilichozuiwa na ITV | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kipindi cha Al Jazeera Witness Special kilichozuiwa na ITV

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MwanaHaki, Jul 8, 2010.

 1. MwanaHaki

  MwanaHaki R I P

  #1
  Jul 8, 2010
  Joined: Oct 17, 2006
  Messages: 2,403
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 145
  Takriban wiki mbili zilizopita, siku ya Jumatatu, kituo cha habari cha kimataifa, Al Jazeera, kilitangaza kipindi chake cha Witness Special, ambacho ni kawaida kutangazwa siku hiyo kila wiki.

  Siku hiyo, kipindi hicho kilichotangazwa kiliitwa MITUMBA, na kilionesha safari ndefu ya fulana ya michezo iliyokuwa ikimilikiwa na mtoto wa nchini Uholanzi - kama sikosei - ambayo ilitolewa kama msaada (donation) pamoja na nguo nyingine zilizotolewa na familia ya mtoto huyo. Huko ulaya, ni kawaida kwa wazungu kutoa nguo kama michango kwa nchi zinazoendelea (?), ambayo inakusanywa na taasisi (?) zinazodai kwamba nguo hizo zinaletwa Afrika kama misaada, kinyume na ukweli kwamba ZINAUZWA. Ndio, hata wazungu nao ni mafisadi pia! Mwashangaa nini?

  Kipindi cha Al Jazeera kilifichua ukweli huu, lakini, cha kushangaza, ITV walikatisha kipindi hicho kabla hakijakamilika, kwa kile kilichotafsiriwa kwamba ni aibu kwetu sisi kuonekana tunavaa mitumba. Fulana ya mtoto wa kizungu hatimaye ilikuja kuishia mkoani Iringa, ITV walikatisha kipindi hicho wakati wa awamu ya mwisho ya kipindi hicho, pale yalipokuwa yakifanyika mahojiano kati ya mtangazaji/mwandishi wa kipelelezi, aliyeandaa kipindi hicho, na mfanyabiashara wa mitumba anayeishi mjini Iringa.

  Kwa wale ambao walikosa kuona kipindi hicho, tembeleeni YouTube kupitia anuani hii  Asanteni.

  Pamoja tutafika!

  ./Mwana wa Haki
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 2. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #2
  Jul 8, 2010
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  sasa watanzania ndio tunauogopa ukweli kiasi hicho au?

  upuuzi mtupu
   
 3. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #3
  Jul 8, 2010
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  mwandishi hajaacha kitu .............

  wachina kawazungumzia, serikali, .............itv wakaona bora yaishe tu waizimie mbalini
   
 4. RealTz77

  RealTz77 JF-Expert Member

  #4
  Jul 8, 2010
  Joined: May 18, 2009
  Messages: 742
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  nilikiona, well wapo wanaofaidika, pia hili linasababishwa na kushindwa kujiendesha wenyewe japo kujishonea nguo, km china wanawweza tengeneza shati kwa sh 1000, why yasitengenezwe hapa? au hata chini yake, wenzetu lazma watatunyanyasa na wataendelea hivyo hadi tutapofunguka! na kuthubutu kujitegemea!leo hii china uchumi juu sababu ya bidhaa hizo ndogondogo, hapa tumekalia sisa tuu, na kulalamika bila vitendo!
   
 5. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #5
  Jul 8, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Mhojiwa wa kwanza anatokea Ujeremani, wale mliokuwa mnawashangilia jana kwene Woza. Yeye anakusanya nguo kwa kuegesha collecting point kwa kubandika nembo ya red cross kwa ulaghai. Mwingine aliyehojiwa yupo Italy.

  The whole story inakumbusha ile vicious cycle ya 'globalisation' and how the mzunguz and ponjoroz won't give us a break.

  Ni hatari lakini salama cha msingi ni uhai tu, mengine yatajiseti mbele kwa mbele.
   
 6. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #6
  Jul 8, 2010
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  duh ...........mimi jamani sijawahi kufika kijijini! sikutaka kuamini kuwa tanzania kuna sehemu iko namna ile .........lakini kumbe ni kweli!

  iko wapi maendeleo kwa kila mtanzania? au ndo hayo ya kuvaa mitumba?
   
 7. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #7
  Jul 8, 2010
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,828
  Likes Received: 10,139
  Trophy Points: 280
  Dah, nimekosa uhondo weee, hebu aandika vyema basi hiyo adress nibofye japo niisome na mie kwani ni mpenzi sana wa hiki kipindi ila juzi nilikuwa na committment nyingine
   
 8. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #8
  Jul 8, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Wamemrusha hewani hadi yule Emoro wa Ubungo Terminal..he he he..
   
 9. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #9
  Jul 8, 2010
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,828
  Likes Received: 10,139
  Trophy Points: 280
  Dah, palikuwa hapatoshi hapo, vipi zile rasta bado anazo na mabegi yao wanayouza..
   
 10. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #10
  Jul 8, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Emoro ni mpiga debe naona kala kichwa cha Upendo coach kwenda Iringa..dah namiss sana safari za kileji..
   
 11. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #11
  Jul 8, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Ze mzunguz when they see us they see money, hadi mtangazaji bila aibu anaongelea threat ya Mchina kwene 'soko lao' la mitumba, this guy was supposed to apologize ..
   
 12. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #12
  Jul 8, 2010
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  mzungu kanimaliza alipoonyesha kiwanda cha nguo cheupeeeeeeeeee huku akionyesha mwanamma anachuma pamba!

  tanzania kweli nchi ya maajabu
   
 13. critique

  critique Member

  #13
  Jul 8, 2010
  Joined: Aug 7, 2008
  Messages: 18
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Acha kabisa hiyo maneno ya kijijini.
  Nilishawahi kukaa somewhere Mtwara ndani huko,dah...jamaa wanaingia kwa nyumba bila hata taa even ya kibatari(Gaijin sijui kama wajua hii..hehe)..halafu takribani mwezi inafululiza.Misosi ni kutegemea typically raw material...mama arudi na kisamvu na kuni,ugali wa muhogo wa mwaka jana....life goes...the days are numbered
   
 14. MchunguZI

  MchunguZI JF-Expert Member

  #14
  Jul 8, 2010
  Joined: Jun 14, 2008
  Messages: 3,623
  Likes Received: 590
  Trophy Points: 280
  Kipindi hiki kilioneshwa kwa mara ya kwanza mwaka jana (2009) naona kimerudiwa na kama kawaida yetu chaneli kama ITV, wanadhani heshima ni kuficha ukweli. Ni hivyo hivyo tulivyojigamba na ile Darwin's nightmare, eti Mwanza hawali mapanki.

  Serikali iliahidi kushitaki lakini sijui iliishia wapi! Serikali ya usanii inadhani tumesahau.
   
 15. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #15
  Jul 8, 2010
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Critique..... Kuna vitu vyengine vikionyeshwa kwenye tv za kimataifa unaweza kujikuta unaukana uraia Mara moja!

  Kwa Hali hiyo ya mtwara ulosema kufa una miaka 40 ni Jambo la kawaida Kama si lazima
   
 16. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #16
  Jul 8, 2010
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Hawa jamaa wa ITV kama ilivyokawaida ya vyombo vingi vya serikali, tabia yao ni kuficha ukweli. Jamaa ameonesha dhahili maisha ya watanzania toka mijini mpaka huko shamba; kote hali ni mbaya bin dhoofu na hakuna hata dalili za kuwa watu watapata ahueni ya maendeleo. Hilo ndilo lililowafanya wakazima channel yao ili wananchi wasikumbuke kile Kikwete alichoahidi mwaka 2005 na ameshindwa kutekeleza na sasa anataka tena aendeleze umaskini wa wananchi kwa miaka mingine mitano.Kumbuka uchaguzi ni mwezi wa kumi wanajitahidi kuziba matundu yote ambayo wananchi watapatiwa ukweli wa ufisadi wa Jakaya!!
   
 17. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #17
  Jul 8, 2010
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,219
  Likes Received: 84
  Trophy Points: 145
  Mitumba huuzwa hata usa jamani. Mitumba si nguo kuukuu. Kwanza mitumba si nguo tu. Mbona tunanunua magari? Nayo tungepewa kama msaada basi
   
 18. Bantugbro

  Bantugbro JF-Expert Member

  #18
  Jul 9, 2010
  Joined: Feb 22, 2009
  Messages: 2,684
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Biashara kubwa tu na pia halali hiyo, hakuna cha ajabu jaribuni kufanya utafiti/google mbona wauzaji mitumba ni wengi tena kutoka ktk nchi za dunia ya kwanza. Watu kila siku tunanunua magari ya mtumba, fenicha, vifaa vya electroniki nguo, viatu n.k.

  Tatizo labda ni kwa wahusika kuuza bidhaa iliyoletwa kwa ajili ya kugawa bure/msaada. Lakini ndio UFISADI huo huo tuliouzoea ktk kila sekta!
   
 19. N

  Ndjabu Da Dude JF-Expert Member

  #19
  Jul 9, 2010
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 3,652
  Likes Received: 409
  Trophy Points: 180
  Hamna lotote. Thread starter ni mwongo na mzushi. Hii ya eti ITV imezuia kurusha hiki kipindi sii kweli. Amejitungia tu upuuzi wake.
   
 20. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #20
  Jul 9, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Na hili ndio legendery jawabu kwa wengi wetu..mtu ukiuliza hiki kitu mboni kiko hivi au vile utaibiwa..'Ohhh mbona US na Europe wanafanya hivohivo'?? This is pathetic.

  Waliodonate hizo nguo intention yao ilikuwa ni kuwasaidia watu maskini huko Africa au Russia, watu ambao kwa asilimia kubwa wanaishi ktk umaskini wa kutupa. Ndio maana mwandishi amejikoki kutokea Ujeremani mpaka Iringa kuifuatilia 'fulana' ilitolewa bure na mtoto wa Kidachi na kuishia kuuzwa mara kadha wa kadha kabla ya kumsikia maskini huyu ambaye ni mlengwa. Intention hapa ni kuonesha jinsi mechanism inavyofeli, na wajanja wachache wanafaidika kuwa kupokea nguo bure na bado wanakuja kuwauzia maskini.
   
Loading...