GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 59,949
- 119,212
Ni mbinu ambayo nilipewa kitambo sana na MTAALAM mmoja wa mapenzi na ambayo kiukweli niliitumia hadi nikaja kumpata Shemeji yenu huyu lakini pia nimeweza kutokuwa mchoyo na nimewapa hadi Wanaume wenzangu na nashukuru Mwenyezi Mungu wote wameitumia na kila siku wananishukuru kwani imewasaidia kuweza kuwapata wenza wao na sasa wanafurahia tu mahaba yao.
Hivyo leo nimeona tena nisiwe mchoyo wa haya MAARIFA na mimi pia niweze kuwasaidia Vijana na Wanaume wenzangu ambao kutokana na kutotulia kwa akina Dada zetu na usumbufu wao pale wanapoanzisha nao mahusiano sasa wameona njia pekee ni kujikita tu katika kupiga punyeto ili kumaliza haja zao.
Ewe Kijana au Mwanaume unayetarajia kuja kuwa na mwenza wako siku za usoni zingatia VIPIMO vyangu hivi vifuatavyo nitakavyokuwekea hapa ili umpate Mpenzi wa kweli na narudia tena VIPIMO hivi haviongopi na vipo sahihi kwa 99.99%.
Ili kujua kama Binti au Mwanamke uliyemuoana na umependa mje kuwa Mume na Mke anakufaa tenga siku saba ( 7 ) tu mfanyie haya yafuatayo:

- Mnyweshe uji wa chumvi asubuhi, ugali maharage na makande kwa hizo siku zote saba. ( Ukina anakunywa na kula na wala hakuambii Bebi naomba sukari au badilisha mboga jua huyo 100% anafaa kumuoa )
- Kama mnaishi kwa mfano Mbagala Kizuiani halafu wote mnafanya kazi mjini basi hakikisha kila siku asubuhi na jioni mnatembea kwa miguu kwenda na kurudi kazini kwa zile siku za kazi. ( Ukiona hakodoi macho kutaka kuomba lifti au halalamiki kuchoka na anatembea kwa spidi ile ile ya ukakamavu jua huyo 100% anafaa kuoa )
- Vaa nguo za jeans ( jinzi ) kila siku moja moja tena zile ngumu kwa makusudi kisha jitahidi uzichafue na zichafuke kwa kutukuka kisha jumamosi au jumapili mbwagie akufulie tena kwa sabuni ya mche. ( Hapa ukiona anazifua halafu hajanuna au hajaomba sabuni ya unga huyo 100% anafaa kumuoa )
- Tenga angalau siku tatu ( lakini ndani ya zile siku zetu saba ) nenda nae Kijijini kwenu kule kijijini kabisa ambako hali ya maisha ni ngumu kisha ukifika nae tu siku hiyo hiyo unampa ndoo tena zile za chuma unampeleka kuchota maji mtoni na pia kesho yake asubuhi tu mnapoamka unamkabidhi jembe na mnaenda shambani kulima. ( Ukimfanyia haya kwa hizo siku tatu mfululizo halafu husikii akilalamika basi jua kuwa huyo 100% atakufaa tena muoe upesi )
- Jitahidi sana ndani ya hizo hizo siku saba katika chakula chenu cha mchana ugali maharage na hayo makande ya usiku basi kinakuwa na pilipili ya kutosha na hakikisha mnakula pamoja huku maji ya kunywa yakiwa hayapo. ( Ukiona katika siku zote hizo anakula na wala halalamiki pilipili kuwa nyingi na haombi maji ya kunywa usipoteze muda kumwekea mashaka huyo anafaa kuoa 100% )
- Katika siku hizo hizo saba jitahidi kwa makusudi utenge tu hata siku tatu hivi ambapo utakuwa unaenda kumchukua mtoto tu wa jirani ambaye ana tabia ya kupenda kujisaidia sana haja kubwa kisha unakuja nae ndani kwako tena hapa unaweza ukavizia ule muda ambao labda unamsikia Mama yake akimuuliza anataka kujisaidia kisha unambeba na kwenda nae kwako tena unakaa nae sebuleni ili " akiukweka " a.k.a kujisaidia haja kubwa tu unamvua nguo ili ayaache pale pale sebuleni kisha unamuita Mpenzi wako aje asafishe. ( Ukiona huyo Mpenzi wako hamlalamikii huyo mtoto na anainama kusafisha " nnya " ya mtoto tena akideki kabisa jua huyo 100% anafaa kuwa Mke kabisa ).
- Hakikisha pia ndani ya hizo siku saba kila siku unamsingizia kuwa ana mahusiano na Mwanaume mwingine hivyo utamuacha muda wowote. ( Katika kumsingizia kwako huku kwa makusudi tena huku mishipa ya shingo ikikutoka na macho kutumbuka ukiona tu anajitetea lakini halii au hatokwi na machozi jua kuwa huyo ni Mke kwa 100% ).