mutisya mutambu
JF-Expert Member
- Nov 21, 2010
- 208
- 82
wana jf kazi kwenu sasa! hiki kimekuwa kilio cha wengi wanaotafuta kazi,utakuta mtu anasoma sifa zinazotakiwa vizuri na kwa raha sana,lakini akifika kwenye kipengele cha uzoefu kazini hasa wa miaka kadhaa unakuta mtu huyo anakunja sura na kuanza kulalamika,kuwalalamikia waajiri.hapa ndipo mie nakuja na swali, hivi kwa nini kila utajapwo uzoefu wa kazi unataja miaka fulani,hivi hicho ndio kipimo pekee cha uzoefu,mtu akikaa kazini miaka nane basi awe ameshakuwa mzoefu,tutajuaje labda katumia miaka miwili kufany a kazi na mingine sita kupiga porojo tu ofisini,safari za huku na huko pamoja na kunywa na kuongea na simu kazini.kwa nini tusibadiri uzoefu wa kazi ukawa ujuzi wa kazi bila kujari umri wa huyo mtu kukaa kazini kwani ni wengi tu waliokaa miaka mingi kazini na bado si wajuzi ukilinganisha na fresh kutoka vyuoni.