Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 36,569
- 44,223
Uongozi wowote unaojinadi unakubalika na raia walio wengi hupimwa kwa uchaguzi huru na wa haki. Kudai kiongozi anapendwa na wengi bila kipimo hiki ni ujuha.
Huwezi kusema kiongozi anakubalika na raia wengi kama huyo kiongozi na serikali yake wamepatikana katika uchaguzi ambao Tume ya uchaguzi sio huru, wapinzani wanabughudhiwa kufanya siasa na kampeni, vyombo vya habari haviko huru kuwapa wapinzani nafasi au kukosoa watawala na ametumia faida ya dola kujipatia madaraka.
Huwezi kuwahoji watu wachache kwa TV au redio ukatumia hiko kama kigezo cha kupima viongozi, kwenye nchi zenye demokrasia dhaifu hata kura za maoni "opinion polls" bado sio kipimo cha kuaminika.Mwisho pia huwezi kutumia wingi wa watu waliohudhuria mazishi yake kama kipimo cha kukubalika.
Sanduku huru la kura tu ndio kipimo sahihi.