Kipimo Cha Utendaji wa Serekali Ndio Hiki?

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,903
Akiwa kwenye kampeni alisema haya namnukuu" .. Waziri wangu wa maji nitakayemteua , halafu maji yasipatikane yeye atageuka kuwa maji..."


Ni miezi minne sasa hakuna mfumo au mpango mzuri wa kulifanya jiji LA Dar tu kuwa na maji ya uhakika.


Alichofanikiwa ni kuwatwanga bakora wakazi wa maeneo aliyobomoa umaskini wa milele.


Pili, yapo matrioni ya fedha yanadaiwa kukusanywa mbona hatuoni mkakati wa madawati, nyumba za walimu badala yake wakuu wa Mikoa na wilaya wanaagizwa kutafuta watu wa kutatua kero hizo?


Tatu, bei ya vyakula inaendelea kupanda tunachosikia ni maombi ya serikali dhidi ya wafanyabiashara?


Mfano tu matrioni ya fedha yamekusanywa lakini sioni Faida yake,

Kwa nini walimu, manesi na madaktari na watumishi wengine ambao ndio wafanikishaji wa Sera hizo wamepandishwa cheo lakini chaajabu hawajabadilishiwa mshahara wao?

Kwa nini kweli ikiwa serikali imekusanya fedha nyingi isiwalipe hela za likizo na malimbikizo yao?


Serikali kuu ndio jipu, haikwepi lawama hizi kwani wao ndio wenye dhamana ya watumushi.


Serikali inayoshindwa kuheshimu mambo madogonadogo kama uchaguzi wa meya na stahiki za watumishi itaheshimu uchaguzi Mkuu!


Kipimo halisi ndoo hiki
Hakuna jipya zaidi ya mazingaombwe ya kutumbua majipu ambayo aidha hawakuwa wapenzi wake wakati wa uchaguzi au muda wao wa utumishi umefika kikomo.
 
Back
Top Bottom