Wapendwa wanajamvi la JF, napenda kuwapongezeni kwa kazi nzuri tuliyoifanya ya kukifikisha chama chetu na Rais wetu Dr. Slaa hapa tulipo hii Leo. Ni ukweli usiofichika kwamba CHADEMA tumemefanya kazi nzuri naimewakuna wengi wapenda maendeleo na wanaochukia dhuluma wanayofanyiwa watanzania na serikali ya mafisadi. Tumeona mafisadi wameongezeka pia mwaka huu maana CCM sasa ni chama cha wafanyabiashara wanaoingia Bungeni ili kulinda maslahi haramu wanayojipatia ndani ya nchi yetu.
Naamini kila mmoja wetu anatambua kuwa bado tunayo kazi ngumu ya kuikomboa nchi hii kutokana na udharimu unaoendelea hivi leo nchini kwetu. Ugumu wa kazi yetu hauko katika kupambana na mafisadi ana kwa ana bali upo katika kuwaamusha usingizini watanzania waliolala huko vijijini. Mimi naamini nchi hii itakombolewa kwa elimu ya urai kwa watanzania walioko vijijini ambao ndio wengi na ndo wapiga kura.
Naamini kipimo cha ushindi kipo katika uchaguzi wa serikali za mitaa 2014 maana ndiyo hujenga msingi wa ushindi wa uchaguzi mkuu. Unapokuwa na viongozi wa serikali za mitaa wa chama chako inamaana kuwa chama kimewafikia wananchi wa maeneo hayo. Wananchi wanachagua chama kilichokaribu nao. Tumeshuhudia namna ambavyo pasipo kutarajiwa NCCR-Mageuzi wamepata wabunge katika baadhi ya majimbo, si kwa sababu walikuwa wazuri lakini ni kwa sababu walikuwa wanaonekana wapo katika hayo majimbo kwa muda mrefu.
Kwa maoni yangu 2014 si mabli na ukizingatia ukubwa wa hii nchi tunahitaji muda wa kutosha wa kukitambulisha chama kwa wananchi. Tunahitaji kupita kila kijiji na kufafanua matatitozo ya ufisadi yanavyoipeleka nchi hii pabaya.
Mimi naamini wananchi wengi hawaipendi CCM ila hawajui wachague nini badala yake. Mimi nimejaribu kuchunguza wakati wa kampeni nikaona kuwa tatizo lilikuwa ni muda mdogo wakumfanya Dr. Slaa afahamike kwa wannchi wa vijijini. Tumefanya kazi ngumu ya kuwashawishi wazazi wetu huko vijijini lakini ilikuwa ni vigumu kutuamini kwa sababu hawakuwahi kukisikia chama cha CHADEMA wala Dr. Slaa.
Nchi hii ni ya Chadema na wapinzani wengine 2015 kama tutatajipanga vizuri maana tumeona jinsi watu walivyoweza kuhamasika na kubadilika katika kipindi cha siku 70 tu na kuleta haya mabadiliko makubwa ambayo CCM hawamini macho yao hata kidogo.Ukweli ni kwamba Chadema ndiyo inatawala nchi hii maana halmashauri katika majiji na miji mingi zitaongozwa na Chadema sasa.
Tunahitaji kuanza mapambano sasa ya kushinda kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa hapo 2014. Tusifanye makosa ya kuuchukulia uchaguzi huu kuwa hauna maana kwetu itakuja kula kwetu 2015.
Tushutuke sasa tuanze kazi mpaka kieleweke, Ruzuku ya chama na michango ya wakereketwa ndiyo iwe kazi yake kwa miaka hii mitatu inayokuja.
Naomba kuwasilisha.......................