Kipimo cha MRI & CT- scan

UniqueMan

Member
Sep 7, 2016
69
26
Habarini wakuu! naomba kujuzwa gharama za kipimo cha MRI na CT- scan, nataka kufanya kichwani.

Natanguliza shukurani zangu za dhati kwa wanaJF.
 
Habarini wakuu! naomba kujuzwa gharama za kipimo cha MRI na CT- scan, nataka kufanya kichwani.

Natanguliza shukurani zangu za dhati kwa wanaJF
Mkuu una brain tumor au ni trauma cases!?.
Anyways.
Brain CT scan ni 150000/= kwa MOI.
Brain MRI ni 300000/= kwa MOI.
NOTE
MOI ni Muhimbili orthopedic institute.
 
Specialist wako anatakiwa achague kama unafanya ct scan au mri kwa kuwa yeye ndio anajua anachotaka kuangalia ni machine ipi kati ya hizo itampa jibu sahii.
 
Naomba kujua maana ya hivi vipimo, yaani MRI na CT-Scan
CT Scan ni computed Tomography scan, hiki ni kifaa kinachotumia mionzi kutambua uvimbe (sometimes inaweza ikawa cancer au non cancerous tumor), majeraha na magonjwa katika sehemu za mwili Kamavile soft tissues mfano brain, Total spine (cervical, Thoracic and lumbar spine).
Kwamfano mtu aliyena uvimbe kichwani (Tumor) au mtu aliyepata ajali akaumia fuvu la kichwa mostly tuna tumia CT scan kutambua location of injury. Lakini pia some skeleton diseases tunatumia CT SCAN kuyatambua.

MRI, ni magnetic Resonance Imaging hiki ni kifaa ambacho ni bora zaidi ya CT scan na kinafanya kazi sawa na CT Scan, ufanisi wake ni zaidi ya ule wa CT Scan although chenyewe hakitumii mionzi katika utendaji wa kazi instead kinatumia High magnetic field kutengeneza picha ya sehemu husika.

Faida ya MRI ni kwamba hakitumii mionzi kufanya kipimo so no cell death Kama ilivyo kwa CT Scan na X- Ray examination.

Hasara ya MRI ni kwamba it's too costful kufanya kipimo.

So according to the magnitude of the problem, doctor anaweza recommend mgonjwa afanye kipimo kwa either CT au MRI scan.

Vifaa hivi vinapatikana Mara nyingi zaidi katika taasisi za mifupa (orthopedic), na cancer (Oncology), mfano MOI na Ocean Road cancer institute (ORCI) japo hata katika hospitali nyingine kubwa vifaa hivi vinapatikana mfano Mloganzila Muhimbili, Bugando na hospitali zingine za private.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom