Kipimo cha furaha na maendeleo ni nini?

NostradamusEstrademe

JF-Expert Member
Jul 1, 2017
3,032
4,028
Nilikuwa nasoma mahali list ya nchi kumi tajiri zaidi duniani kuanzia ya kwanza hadi ya kumi kulingana na viwango vya GDP.
1.Quatar 2.Luxembourg 3.Singapore 4.Swizerland 5.Brunei 6.Norway 7.Iceland 8.Kuwait 9.UAE 10.Hong Kong
Kilichonishangaza ni kukosekana kwa Marekani,Urusi na China.Nimejifunza kuwa mataifa haya yanaitwa yenye nguvu na uchumi mkubwa kumbe ni matambo ya nguvu za kijeshi ila wananchi wake sio kwamba wanafuraha sana.
Nikafungua tena nchi 10 tajiri zaidi katika Afrika nikakuta
1.Nigeria 2.Africa Kusini 3.Misri 4.Algeria 5.Angola 6.Morocco 7.Ethiopia 8.Kenya 9.Sudani kaskazini 10.Tanzania.
Kwa nchi ya Tanzania nikashangaa na kufurahi mno mbona tunaitwa nchi masikini.Ila nikagundua waliopanga vigezo hivi wameangalia rasilimali tulizo nazo.
Nikazidi kusoma tena nchi masikini zaidi Afrika nikakuta.
1.Malawi 2.Burundi 3.Jamhuri ya Afrika ya kati 4.Gambia 5.Niger 6.Liberia 7.Madagasca 8.DRC 9.Ethiopia 10.Guinea
Hapa nimeshangazwa na vitu viwili kwanza Ethiopia kwenye nchi tajiri Afrika imo na kwenye nchi masikini imo.Pili DRC yaani Congo ni nchi yenye kila aina ya madini lakini ni masikini ila tunaweza sema shauri ya vita vya wenyewe kwa wenyewe.Ajabu hata Angola kulikuwa na vita vya msituni kwa miaka 27 lakini iko kwenye nchi tajiri Afrika ila tunajua wana mafuta.
Nikazidi kuangalia tena nchi6 zenye masikini au mafukara wengi zaidi duniani kwa idadi nikakuta 1.Bangladesh 2.India 3.Ethiopia 4.Afrika ya kati 5.Ethiopia 6.Nigeria.
Hapa napo nimeshangaa kuona Nigeria ni nchi ya kwanza kwa utajiri Afrika ila kwa mwananchi mmoja mmoja masikini wako wengi sana kwa maana hiyo utajiri umehodhiwa na wachache labda ndio maana vita huko haviishi.
Bado sijapata kigezo cha nchi kuendelea ni watu au vitu?
Naomba kutoa hoja.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Usichanganye uchumi wa nchi kwa ujumla (GDP) na uchumi wa mtu mmoja mmoja ndani ya nchi (GDP per capita)...yani sawa sawa ulinganishe mtu bachelor mwenye mshahara wa milioni 1 na mtu mwenye familia ya watu sita halafu ana mshahara wa milioni 2....wataalamu wa uchumi watabaelezea zaidi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom