Kipima Uongo

akashube

JF-Expert Member
Dec 24, 2009
401
23
Kuna mama mmoja alifariki na kujikuta amefika mbele ya malaika wa mwenyezi Mungu ambaye alimfikisha kwenye chumba kilichojaa saa nyingi za mshale zisizo na kioo.

Yule mama akataka kujua zile saa zisizo na vioo kazi yake ni nini. Yule malaika akamwambia hizo zinapima uongo anaosema mwanadamu duniani, na kwenye chumba hicho kila binadamu kuna saa yake.

Ghafla yule mama akaona saa moja ambayo mshale wake hautembei akauliza ni ya nani. Malaika akamwambia hiyo ni ya mama Theresa na imewahi kutembea mara mbili tu basi ikasimama.

Alipotazama vizuri yule mama aliona saa chache sana ambazo hazitembei lakini nyingi zilikuwa zinatembea kwa kasi kubwa. Hivyo akaamua aulize kwa malaika ili amwonyeshe saa ya mume wake ilipo.

Malaika akamwambia ooh hiyo iko ofisini kwetu tunaitumia kama feni.
 
hahahahahah lol inaelekea mumeo alikuwa mwongo sana lol
 
Huuwii asubuhi yote umeamua kunitanua mbavu zangu hii ungileta after lunch!kweli kazi ipo jf!jf for life
 
It's good hakuomba aonyeshwe za wanasiasa, nahisi zingekuwa zinatumiwa kugenerate umeme. :nono: :yield:
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom