akashube
JF-Expert Member
- Dec 24, 2009
- 401
- 23
Kuna mama mmoja alifariki na kujikuta amefika mbele ya malaika wa mwenyezi Mungu ambaye alimfikisha kwenye chumba kilichojaa saa nyingi za mshale zisizo na kioo.
Yule mama akataka kujua zile saa zisizo na vioo kazi yake ni nini. Yule malaika akamwambia hizo zinapima uongo anaosema mwanadamu duniani, na kwenye chumba hicho kila binadamu kuna saa yake.
Ghafla yule mama akaona saa moja ambayo mshale wake hautembei akauliza ni ya nani. Malaika akamwambia hiyo ni ya mama Theresa na imewahi kutembea mara mbili tu basi ikasimama.
Alipotazama vizuri yule mama aliona saa chache sana ambazo hazitembei lakini nyingi zilikuwa zinatembea kwa kasi kubwa. Hivyo akaamua aulize kwa malaika ili amwonyeshe saa ya mume wake ilipo.
Malaika akamwambia ooh hiyo iko ofisini kwetu tunaitumia kama feni.