Kipima joto itv; wizi wa madini yetu nini kifanyike?? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kipima joto itv; wizi wa madini yetu nini kifanyike??

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by commited, Sep 21, 2012.

 1. commited

  commited JF-Expert Member

  #1
  Sep 21, 2012
  Joined: Feb 27, 2012
  Messages: 1,617
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Naaam kipima joto kipo hewani, karibuni muangalie kunawageni 3 toka wizarani akiwepo naibu waziri wa madini bwana masele, na mwanaharakati dr. Shale
   
 2. commited

  commited JF-Expert Member

  #2
  Sep 21, 2012
  Joined: Feb 27, 2012
  Messages: 1,617
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Watu hawa 3 wa serikali wanajisifia kuwa hakuna nchi katika africa inayofanya vizuri katika madini eti kama tz, naibu waziri anasema eti sasa ndio amejua njia za wizi kwahiyo ndio wanajipanga kuwadhibiti....... Daaaah kazi ipo hapa bwana shala anasema swala la kupiga kelele juu ya wizi wamepiga kelele tangu 2001 lakini hakuna kilichofanyika, anasema sheria zetu za madini ni za kucopy na kupaste toka zambia, hawa wa serikali wanakataaa wanasema tz tunafanya vizuri sana katika madini kuliko nchi nyingine africa lohhh kazi ipo hapa
   
 3. commited

  commited JF-Expert Member

  #3
  Sep 21, 2012
  Joined: Feb 27, 2012
  Messages: 1,617
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Bwana masako anauliza, nini kinafanyika endapo mkataba umeshasainiwa na muwekezaji huyo wakati akichimba ikatokea akakutana na madini mengine je nini huwa kinafanyika
   
 4. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #4
  Sep 21, 2012
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Tuwape wataalam wetu wa hapa hapa nchini wakaandae mazingira bora kisera na kisheria na kuimarisha vyombo vya usimamizi visivyoingilika na na executive power kiutendaji.

  Tuwashirikishe zaidi washikadau wa nchi hii katika kila hatua ya mabadiliko kwa faida ya taifa zima na wala tusiwaachiel hawa manyang'au wa Uswisi kuendelea kutupora na kuficha nje ya nchi ajira zetu hizo.

  Tuandae mazingira yenye kuchaangia kuzalisha wawekezaji wengi zaidi wa nyumbani hapa hapa ili nao wawe na uwezo wa kushindana katika sekta hizi.
   
 5. Little Angel

  Little Angel JF-Expert Member

  #5
  Sep 21, 2012
  Joined: Aug 21, 2011
  Messages: 1,218
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  nimeikuta imeanza ila nimesikia mmoja ansema kuwa Eti Sheria ya madini ya Tanzania imekuwa copied from Zambia. the only thing kilichobadilishwa ni neno SHERIA YA MADINI TANZANIA badala ya ZAMBIA. but content yoote ni kukopi na kupaste......
   
 6. F

  FJM JF-Expert Member

  #6
  Sep 21, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Huyo mtu wa serikali awe makini sana na anachosema. Kama kuna mtu anayejua madudu ya sector ya madini Tanzania, pamoja na mikataba mibovu basi Dr Nshala ni mmojawapo. Huyu bwana kamaliza PhD Havard na alienda kusomea mikataba ya madini. Anaijua sekta ya madini kama kiganja cha mkono wake.
   
 7. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #7
  Sep 21, 2012
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,124
  Likes Received: 1,709
  Trophy Points: 280
  Nilishachoka na habari za madini ya TZ
   
Loading...