Kipima joto ITV: Sheria ya mabadiliko ya Katiba

Wote wawili (Shivji na Mnyika) wapo. Hivi sasa Mnyika anafafanua, mchakato unawabana wananchi kwani atakaye-amua kukusanya maoni ya wananchi atapigwa ndani miaka 7 au faini; adhabu ambayo ni kubwa zaidi ya m-hujumu uchumi anatolea mfano wa adhabu iliyotolewa na mahakama kuhusu hasara ya majengo pacha ya BoT

walitumia Masabuli kuweka kipengele hichi.
 
Sheria ya mabadiliko ya katiba....kumbe kuna kipengele kwenye shiria hiyo kuwa kama utakuwa ana kimbelembele cha kuelimisha watu kuhusu huu mchakato wa mabadiliko ya katiba utachukua muvua ya miaka 5 au mpaka 7 jela au faini ya tsh 15m......

Kumbe! Ndo maana Deus Kibamba na wenzake wa Jukwaa la Katiba wamenywea!
 
hii ni zaidi ya elimu,sikufahamu kama hii nchi inawatawala madikteta namna hii,,OMG this country!! Elimu zaidi inahitajika kwa kweli...
 
Prof Issa Shivji anaeleza kwa kina ili suala la Katiba, nimeshangaa kwenye wajumbe 600 wajumbe 400 wanatoka CCM.
 
Prof Issa - hapendelei hii sheria kupelekwa mahakamani maana itakuwa ni kuidharirisha serikali, anapendekeza muafaka wa kitaifa -serikali ikubali ili iweze kurejesha hiyo sheria bungeni ili iweze kufanyiwa mabadiliko
 
Shivji anasema huu mchakato una kasoro na kuna hicho kipengele jamaa walichokitaja hapo juu kuwa kama watu wataenda kukipinga mahakamani sbb kinapingana na katiba iliyopo itakuwa ni aibu kwa serikali
 
Mnyika anasema kwa sheria hii ni kuwa kama wananchi watapiga kura ya hapana basi mchakato wote na kila gharama iliyotumika utaishia hapo
 
according to Mnyika ni kuwa kumbe hata wao wanavyoijadili hiyo katiba hapo studio ni makosa...eti sheria inasema mijadala lazima iwe ni ndani ya tume husika tu
 
Mnyika anasema - iwapo wananchi watapiga kura ya hapana, kuhusu katiba itakayoletwa na tume basi, tunarejelea kwenye ile ya awali- anasema ni mtego ulowekwa makusudi na serikali ikiwa ni somo toka ktk mchakato wa katiba mpya ya katiba ya kenya
 
Hii movi inaonyesha kuwa CDM walikuwa na hoja ya msingi walipotaka vipengele vya hiyo sheria vichambuliwe....inaonyesha Magamba walikurupuka maana hata rais kasaini sheria inayopingana na katiba iliyopo
 
Mnyika anasematusiitazame katika kwa jicho la uchaguzi bali katiba ni kwa maendeleo ya taifa
 
Masako anamuuliza Shivji je inawezekana kwa wajumbe wa katiba kuibadilisha .....shivji anasema kuwa itakuwa ngumu kwa sbb wale waliopitisha sheria hii ndo majority wataijadili so ni yale yale tu
 
Isack Cheyo - mjumbe wa kamati kuu ya UDP - anasema tume itakuwa ni ya watu wawili -rais wa Jamhuri na yule wa Zenji, wao ndo watatunga adidu za rejea. Anaona mswada kama ulikufa yaani uliletwa kwa wananchi - kisha ukaondolewa; kilicholetwa hivi sasa na ambacho hakikupita kwa wananchi ni kitu kipya kabisa; anashangaa kuona mswada huo kuwa sheria bila wananchi kushiriki.
Wajumbe wa tume -anasema watakuwa wale wale wanaolalamikiwa -yaani majaji wastaafu tena wanaoheshimika, anatolea mfano wa tume ya uchaguzi inayoongozwa na hao majaji; ili hali tume ikilalamikiwa kutokuwa huru

Mnafiki tu kwa nini hakupinga bungeni?
 
Hiki kipindi kingekuwa kinaendeshwa tbc,yule bosi mteule wa mkuu angeshapewa notes
 
sheria inasema 50% ya waliopiga kura wakivote YES katiba itapita......na ukichukulia kuwa mfumo wa kupiga kura utakuwa ni mmundo wa tume hii iliyopo basi kuna hatari ya wakajitokeza watu wachache na overall outcome ikawa katiba imepitishwa na watu wachache sana
 
Wamepitisha mswaada mbovu,itaundwa tume mbovu,bunge la katiba litakuwa bovu,na mwisho tutapata katiba mbovu,kwahiyo wananchi kwenye kura ya maoni wataikataa na hapo ndipo Ccm wanapopataka ili tuendelee na hii katiba ya sasa!Wasanii wakubwa wa demokrasia!
 
Dah!...hii katiba inaonekana ni chaka, ni kama sasa tunapotea vile....RAIS anasign sheria inayopingana na katiba iiliyopo? kweli hawa CCM hawajajipanga
 
Prof Shivji - anasema mapungufu mengine ambayo ni hatari zaidi ni kuwa -kama watakaopiga kura zaidi ya asilimia 50 wakisema Ndiyo, basi katiba itakuwa imepita. Angalizo ni kuwa zaidi ya asilimia 50 ni ya wale watakaopiga kura na SIYO waliojiandikisha. Hivyo wakijitokeza watu miln 2, na kati ya hao miln1.10 wakipiga kura ya Ndiyo, basi katiba imepita bila kijali kuwa imepitishwa na watu 1.1ml kati ya watz wote walojiandikisha
 
Isaack cheyo wasiwasi wake ni kuwa kuna uwezekano wa Zanzibar/Bara kusema YES na mwingine akasema hapana na hapo katiba itakuwa kwishney
 
Shivji anahofia katiba kutokupita sbb kama kwa mfano kuna vipengele 500 na wewe ukawaunapinga viwili basi unaendesha kampeni na watu wanaikataa katiba yote, na kwa bahati mbaya ikishakataliwa hakuna kuirudia tena
 
Back
Top Bottom