Kipima joto ITV: Sheria ya mabadiliko ya Katiba

Ritz

JF-Expert Member
Jan 1, 2011
46,892
32,309
Wanabodi...
Kipima joto ITV wageni waalikwa ni Prof Issa Shivji, kutoka kigoda cha mwalimu pamoja na John Mnyika, kutoka Chadema pamoja na Isack Cheyo, kutoka UDP
 
asante kwa taarifa mkuu, ndo anaelezea maana ya bunge la katiba, anasema ni kosa bunge la katiba mpya kuwa na wabunge waliochaguliwa kwa katiba ya sasa, maana wanatakiwa kuilinda sio kuiua, very interesting
 
Nani Shivji au Mnyika?Sina akisesi na tv coz niko kwenye gari nasafiri
 
Nani Shivji au Mnyika?Sina akisesi na tv coz niko kwenye gari nasafiri

Wote wawili (Shivji na Mnyika) wapo. Hivi sasa Mnyika anafafanua, mchakato unawabana wananchi kwani atakaye-amua kukusanya maoni ya wananchi atapigwa ndani miaka 7 au faini; adhabu ambayo ni kubwa zaidi ya m-hujumu uchumi anatolea mfano wa adhabu iliyotolewa na mahakama kuhusu hasara ya majengo pacha ya BoT
 
Sheria ya mabadiliko ya katiba....kumbe kuna kipengele kwenye shiria hiyo kuwa kama utakuwa ana kimbelembele cha kuelimisha watu kuhusu huu mchakato wa mabadiliko ya katiba utachukua muvua ya miaka 5 au mpaka 7 jela au faini ya tsh 15m......
 
Wote wawili (Shivji na Mnyika) wapo. Hivi sasa Mnyika anafafanua, mchakato unawabana wananchi kwani atakaye-amua kukusanya maoni ya wananchi atapigwa ndani miaka 7 au faini; adhabu ambayo ni kubwa zaidi ya m-hujumu uchumi anatolea mfano wa adhabu iliyotolewa na mahakama kuhusu hasara ya majengo pacha ya BoT

Craaaaap
 
Wanabodi...
Kipima joto ITV wageni waalikwa ni Prof Issa Shivji, kutoka kigoda cha mwalimu pamoja na John Mnyika, kutoka Chadema pamoja na Isack Cheyo, kutoka UDP

Huyo wa UDP anaitwa Isaac Momose Cheyo
 
Isack Cheyo - mjumbe wa kamati kuu ya UDP - anasema tume itakuwa ni ya watu wawili -rais wa Jamhuri na yule wa Zenji, wao ndo watatunga adidu za rejea. Anaona mswada kama ulikufa yaani uliletwa kwa wananchi - kisha ukaondolewa; kilicholetwa hivi sasa na ambacho hakikupita kwa wananchi ni kitu kipya kabisa; anashangaa kuona mswada huo kuwa sheria bila wananchi kushiriki.
Wajumbe wa tume -anasema watakuwa wale wale wanaolalamikiwa -yaani majaji wastaafu tena wanaoheshimika, anatolea mfano wa tume ya uchaguzi inayoongozwa na hao majaji; ili hali tume ikilalamikiwa kutokuwa huru
 
Prof Shivji anasema sheria iliyowekwa katika mchakato wa kulekea katiba mpya,ni mbovu na inakinzana hata na katiba iliyopo,anashindwa elewa walifikiria nini kuamua kuweka sheria hiyo
 
Prof Shivji -anasisitiza kuhusu kifungu cha 21(10) kinachotoa adhabu ya chini ya miaka 3 au ya juu ya miaka 7 -kuwa kama rais angelitambua asingeli-saini hiyo sheria, kwani inakinzana na katiba iliyopo. Kwani kusimama hadharani na kujadili nje ya tume husika, mtu atakuwa anatenda kosa la jinai. Anasema, iwapo mahaka zetu zikisema kifungu hiki ni kinyume cha katiba basi, utaratibu mzima wa kukusanya mawazo utakuwa umevurugwa kabisa.
 
Wanabodi...
Kipima joto ITV wageni waalikwa ni Prof Issa Shivji, kutoka kigoda cha mwalimu pamoja na John Mnyika, kutoka Chadema pamoja na Isack Cheyo, kutoka UDP

asante kwa taarifa mkuu.Tupe updates
 
Wanabodi...
Kipima joto ITV wageni waalikwa ni Prof Issa Shivji, kutoka kigoda cha mwalimu pamoja na John Mnyika, kutoka Chadema pamoja na Isack Cheyo, kutoka UDP
Kipima joto cha ITV kinabagua mbona sioni muwakilishi wa CCM?
 
Prof Issa - anashangaa kuhusu bunge la katiba ambalo litakuwa na wabunge 600 kati ya hao 400 watakuwa wa ccm toka tz bara na 200 watatoka Zenji, inamtia wasiwasi kuhusu huu uwakilishi.
 
nilikua nafuatilia,mjadala,umeme umekatika,ila shivj kanipa cha kusema,ilipofika zam ya mnyika umeme umeisha ni wa sola nipo kgm kask_kata ya mkigo,tupen taarifa
 
Shivji: bunge ilo la katiba theluthi mbili ya wabunge wa bunge ilo watatoka magamba,na theleuthi moja watatoka Zanzibar,anauliza je litaitwa bunge la katiba kweli?
 
Mnyika - anafafanua ni kwani CDM waliamua kutoka ndani ya bunge -kwanza mswada kusomwa mara 2 ili hali ukiwa na mapungufu; pendekezo la CDM ilikuwa ni kurekebisha mapungufu ili kuwapa wananchi nafasi kubwa ya kushiriki
 
Back
Top Bottom