Kipima Joto ITV: Rasimu ya katiba mpya - Je, inajibu matarajio ya wananchi kwa miaka 50 ijayo?

kelao

JF-Expert Member
Sep 24, 2012
8,132
5,785
Wakuu prof. Kabudi yupo ITV live akifafanua rasimu ya katiba mpya.wenye nafasi tumfuatilie pengine tunaweza ambua kitu..
 
Kwa ufupi anasema hii ni rasimu ya awali,itatolewa rasimu nyingine ambayo itakwenda kwenye bunge maalum la katiba.Hivyo yatarajiwe mengi zaidi kwenye rasimu hiyo. Pia studioni wapo wadau wa jukwaa la katiba.
 
Mmoja wa wasomi waliobobea sana kwenye sheria... Akiongea unatamani uendelee kumsikiliza...
 
Kwa jinsi nilivyomwelewa prof.Kabudi anajaribu kutetea kile walichokubaliana na wanatume wenzake.maoni halisi ya wananchi yapo pembeni.hivi kwenye rasimu wanataka jaji mkuu aendelee kuteuliwa na rais halafu wale walioshindwa kwa hila waende mahakama ya juu kufungua kesi ya kupinga matokeo ya rais huyo huyo ambae anapaswa kumteua jaji mkuu.tafakari chukua hatua..
 
Hoja za prof. Kabudi zinaonyesha wanatume pushed their own agenda kuliko maoni ya wananchi.
 
Ni mwanzo mzuri katika kelekea kupata katiba mpya ya Tanzania na Tanganyika pia. Kila kitu huwa kina mwanzo na mara nyingi mwanzo ni mugumu! Watanzania tuache kulaumu wakati bado tuna nafasi kubwa tu ya kutoa maoni yetu katika kuboresha katiba yetu!
 
Baada ya kumalizika kwa Kipima joto mambo mengi yamejitokeza
1. Watanzania wanaonekana kuisoma rasimu kutoka midomoni mwa watu wachache wenye maslaha yao.
2. Watanzania wengi na hata wasomi na hili linaonekana hata kwenye maoni ya wengi hawajui kuwarasimu hii ni rasimu ya Serikali moja tu yaani ile ya shirikisho hivyo kila mwenye upuuzi wake atauweka katika serikali ya kwao Tanganyika au Zanzibar.
Hivyo ndugu zetu wa Tanganyika jitahidini kuunda Katiba yenu ambayo mtatia kila kitu na mtakuwa na uwezo wa kupanga mnataka nini.badala ya kuendelea ile tabia ya kuwapangia wenzenu!
 
Back
Top Bottom