Kipima Joto ITV: Polepole, Prof. Kitila, Mtatiro - Mageuzi ndani ya CCM, je ni mfano wa kuigwa...?

N'yadikwa

JF-Expert Member
Aug 10, 2014
7,121
10,230
Hoja mezani: Mageuzi Ndani ya CCM, Je ni mfano wa kuigwa na vyama vingine?

Moderator: Julieth Robert

Wageni Studio:

  1. Julius Mtatiro - CUF
  2. Prof.Kitila Mkumbo - ACT Wazalendo
  3. Humphrey Polepole - CCM
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole
  • CCM ni Taasisi
  • CCM kinafanya major transformation yaani kwenda hatua bora zaidi
Mageuzi yanatazamwa ktk maeno matatu
1. Leadership transformation. ..Aina ya viongozi bora anasema Humphrey
Uongozi lazima upatikane kwa hoja kwa sababu,kwa sifa na kwa mujibu. wa katiba.

2. Mfumo na Muundo wa CCM, namna ambavyo CCM kinatengeneza miongozo yake et al

  • Wanataka kutazama namna taarifa zinavyotoka ngazi ya chini hadi juu.
  • Wanataka Uongozi wa Juu uwe karibu sana na wanachama
  • Wanataka pafike mahala chama kiwasaidie wanachama
3. Mageuzi Makubwa ya kiutawala,Rasilimali fedha,Rasilimali watu Wanataka chama kiwe self reliant.
  • Wanataka kuongeza tija.
  • Wanaboresha mfumo wa namna CCM kinavyoajiri.
  • Wanahakiki Rasilimali zao,waziongezee thamani ili ziendeshe chama
  • Mfumo utakaowezesha Uongozi wa juu kujua mapato ya chama tokea chini bila kufika huko kwa namna rahisi.
Kasisitiza KIONGOZI wa CCM awe na kofia moja ya uongozi ili kuongeza ufanisi na kupunguza gharama. Anasema wataonyana kijamaa , lazima wanachama wasikilizwe.

Mshauri wa ACT-Wazalendo, Prof. Kitila Mkumbo
Tunapozungumzia mageuzi tunaangalia mambo manne. Je, CCM wamefanya mageuzi kweli tutaona kwa hoja hizi, anasema.

  • Mabadiliko ya kiitikadi. Amefananisha mageuzi ya Uingereza ktk vyama
  • Mageuzi ya Kisera. Anawachallenge CCM hawajafanya mageuzi ya kisera.M/kiti mpya hajasema kama kuna mabadiliko ya kisera.
  • Mabadiliko ya kiutendaji yaani operational transformation / change. Anasema hilo ni jepesi na ndilo pekee walilogusa CCM this time huko Dodoma
Mtatiro kainama anaandika.

ACT hawawezi kuiga kwani CCM haijafanya mageuzi yoyote isipokuwa mabadiliko ya kiutendaji.

Julius Mtatiro - CUF
Nimefurahi kukutana na wenzangu hapa.
Mjadala huu ni kwa faida ya wananchi wote, sio CCM peke yao.

- Kama kweli wanasisitiza dhana ya KOFIA MOJA MTU MMOJA basi aanze Mwenyekiti kuvua moja wapo.

- Humphrey amekaa hapa kutuambia mabadiliko makubwa ambayo vyama

- Nashangaa suala la itikadi ya chama cha siasa ni msingi mkubwa wa kutoa dira lakini CCM hakina itikadi ile ilishakufa!

- Unapozungumzia mageuzi, unazungumzia dhamira!...Hayati Mwalimu JK Nyerere alikuwa na dhamira ktk kila alilofanya. Je, wanalofanya akina Humphrey yanawagusa wananchi!? hapana! Mfano moja ya suala walilopaswa kulijadili kwenye mkutano ule ni suala la Katiba ya nchi. Suala la katiba yao ya chama sio suala kubwa linalogusa maslahi ya dola wanayoiongoza.Mtatiro anasema Humphrey ni rafiki yake haswa!

- Mtatiro anasema alitarajia kuona ajenda zinazogusa maisha ya wananchi kwa sababu lengo la chama dola sio chama tena ila mageuzi ya dola wanayoiongoza

- Mnapofanya mabadiliko tunawapima kwa kauli zenu...anatoa mfano wa kauli ya Mwenyekiti kuhusu wale waliompigia makofi mtu fulani, kwamba haikuwa kauli ya fundisho.

- Kimekuwa chama cha ndio mzee sasa..kamaliza

Swali kwa Humphrey Polepole
SWALI: Mabadiliko hayo yanamgusaje mwananchi?
JIBU: Humphrey anaanza kwa kusema hawa si vyama vya upinzani bali ni vyama vyenye mawazo mbadala kwa hiyo kwake sio vyama vya upinzani.
Anaendelea...CCM kina itikadi, Anapinga kwamba CCM hakina ITIKADI!

Anasoma Katiba sehemu inayozu gumzia Ujamaa na Kujitegemea kwa kurejea Azmio la Arusha. Anapinga kwamba CCM hakina Itikadi.

Anajitetea azmio kuu lilikuwa kufanya marekebisho ya Katiba kwa hiyo hoja nyinginezo hazikuwa central ktk mkutano huo maalum.

Anaendelea kutetea hoja ya itikadi...Ujamaa na Kujitegemea kwamba tusiwe tegemezi.Ujamaa wa Tanzania umejengwa ktk usawa et al na sio ujamaa wa kisayansi ule wa kimaksisi!

  • Ujamaa wetu ni wa kutoka nyumbani.
  • Ujamaa wanao u embrace sio ule wa akina Carl Max ni ule wa kutoka shinani/nyumbani.
  • Sera za CCM sio za kukurupua kama za vyama vingine...CCM kina muongozo,muelekeo unaoonyesha dira ya wapi kinaenda na hiyo inatengeneza Dira ya Taifa.
  • Kv Elimu Bure chini ya 5th phase govt...anasema haya yanatoka ndani ya chama kwani huo ndio USAWA unaosisitizwa na CCM...tumetengeneza madawati haya yote yana msingi ndani ya Sera ya chama
  • CCM idadi ya watu pekee ni funzo kwa CUF wenye watu Milioni Mbili na ushee huku akiwagonga nyundo akina Mtatiro anasema Mtatiro ni Mkiti na Lipumba upande wa pili...ACT nao Kiongozi wao anatazama Kigoma tu!
  • Utaratibu wa nidhamu ndani ya chama pia ni shule kwa upinzani.
Profesa Kitila Mkumbo
- Bado anasisitiza mabadiliko walofanya ni ya ki operational zaidi na ni ya kawaida tu hayo.

- Anakumbushia suala la KOFIA MOJA MTU MMOJA alijibu ameruka...anajibu nitarudi kujibu!

- Kitila anasema CCM kili adopt baadhi ya mambo ktk Azmio la Arusha ambayo hakiyatekelezi na mengine kiliyaondoa hivyo anakazia hoja ya itikadi kwamba bado chama hakina itikadi thabiti.

- Anasema ni muhimu nafasi ya Mwenyekiti wa chama ikawa tofauti na Rais.Anatoa mifano ya wengine anasema imesalia CCM na ZANU PF ambavyo Mwenyekiti ni rais pia. Kwa hiyo wajifunze kwamba suala la mtu mmoja kofia moja hawajaanza kulitekeleza.

WANANCHI MTAANI
- Maamuzi magumu yanaweza kujenga au kubomoa chama.

- Kufukuzana kunajenga makundi,anaefukuzwa ana watu wengi nyuma yake...kufukuzana hakuna tija.

-Maamuzi magumu yanafanywa hata Upinzani umekuwa ukifanya hivyo kwa hiyo inaweza kujenga ama kubomoa.

Julius Mtatiro
- Anamsikitikia Humphrey na CCM akisema wanachama kukutana Dodoma just kwa ajenda ya kurekebisha au kuidhinisha katiba (kama anavyoongezea Kitila off mic) ni kuchezea fedha walipaswa kujadili mustakbali wa uchumi wa nchi ambao upo ktk hali isiyo nzuri.

- Ni rahisi kujifunza kwa vyama vidogo kama ACT kuliko CCM...anatolea mfano wa ACT kiongozi kutangaza mali zake anasema hili ni la kujifunza

- Wamepiga marufuku mikutano ya kisiasa halafu wanaandika wanasimamia Demokrasia! anahoji kama lipo la kujifunza hapo!

- Hivi sasa tupo ktk wakati mgumu, miradi mikubwa yote tunategemea wafadhili tunaomba mambo mengi ametoa mifano ya Tz kuomba ijengewe kiwanja etc

Moderator anaruhusu simu...

Julius Mtatiro - Itikadi ya CUF hapo awali ni kutajirishwa, kwamba mwananchi atawezeshwa...hata ilibadilishwa na sasa CUF ni chama cha Kilibelari,Ulibelari wa kiafrika!

Humphrey Polepole
- CCM hakijawahi kuchukua mali za Serikali na kuzifanya zake...Kina mali nyingi wakati huo zikiwemo kampuni kv MECO

- UDOM , Mwl Nyerere college yote ilikuwa mali ya CCM tulitoa kwa serikali,hata UDSM ilianzia Lumumba mali ya CCM.

- KOFIA MOJA MTU MMOJA - Dhamira ipo tumeanza ngazi za chini tutaendelea.

- Hawa walisema tunataka rais mkali ,asiesafiri sana leo wamegeuka.

Simu kutoka Iringa: Leo hii ukimvua mhe Rais kofia ya uenyekiti wa chama unawapa nafasi watu kufanya ujanjaujanja

Humphrey Polepole anaendelea
- Kwa hawa waloondolewa wanaweza kufikiriwa kwa miezi 48 ijayo.

- Ametakiwa na MODERATOR afafanue suala la kofia moja anajibu kwamba safari ya mageuzi ndio imeanza

Simu kutoka Mbeya: Polepole anaposema hawajachukua mali za Serikali vipi kuhusu viwanja vya mpira mbona kila kiwanja eti chao!

Humphrey Polepole anajibu: Tuna viwanja 22 na vingine waliachia vilikuwa zaidi ya hivyo. CCM huwa wanachangishana wanajiendeleza!

Prof. Kitila Mkumbo anaingilia: Humphrey tofautisha CCM ya kabla ya 1992 na baada ya hapo,Chama kilikuwa sehemu ya mtanzania.

Polepole anampinga Prof. Kitila: Sio kila mtanzania kabla ya 1992 alikuwa mwanachama hivyo mali zote tangu wakati ni za chama na zilitafutwa na wanachama. Anamshutumu Kitila kutumia nafasi yake kupotosha!

Humphrey Polepole anaendelea...

  • Tumedhibiti uvujaji wa mapato bandarini na kwingine
  • Tunaleta mpango wa Bima ya afya nchi nzima
  • CCM haijifunzi ANC inajifunza CPC cha China
  • Hakuna aliezuiwa kufanya siasa

Julius Mtatiro
- Yanayotekelezwa CCM isijinasibu kwani ni kodi ya wananchi na ndio majukumu ya serikali.

Kumalizia: Kabla ya 1992 kila mtanzania alikuwa mwanaCCM hata jeshini ilikuwa lazima uwe na kadi. Hivyo hizo mali mlizomiliki kabla ni za serikali. Hoja ya mali hizo kurejeshwa serikalini haijafanyiwa kazi.
 
Utawala wa mtu mmoja nalo lizungumziwe bila kusahau ya bwana yule usituangushe mtatiro
 
Mnao waona na kuwasikia, Mwulizeni Polepole NINI hasa SIASA/Falsafa ya CCM. Je, bado ni Ujamaa na Kujitegemea?je, bado wanaamini katika: Binadamu wote ni ndugu zangu na Afrika ni Moja?
 
Mnao waona na kuwasikia, Mwulizeni Polepole NINI hasa SIASA/Falsafa ya CCM. Je, bado ni Ujamaa na Kujitegemea?je, bado wanaamini katika: Binadamu wote ni ndugu zangu na Afrika ni Moja?
Pole pole kasema wao falsafa yao ni ujamaa na kujitegemea.
 
Polepole-polepole amesaliti watanzania nchi za wengine huyo jamaa angetiwa shaba
Hivi akili ya nyumbu wotr ndo imefikia hapo mwisho wake..??
Angepigwa shaba labda kama Hiyo iwe nchi ya wana ufipa na Jirani yao Buguruni lakini sio CCM chama kubwa lenye kuwapenda watanzania wote hata kina lissu ambao wana enjoy amani na umoja wa nchi hii.
 
Back
Top Bottom