Kipima joto ITV: Maandamano ya CHADEMA morogoro, je kulikuwa na haja ya polisi kutumia nguvu ile?

Itv bana, wameenda kuhoji watu wa kilimanjaro tu, kipimajoto hiki magumashi.lkn mcheza kwao hutunzwa.
 
Kawaida ya muongo na mwenye kuongeza chumvi katika mambo. hiyo 1% inayobaki imekwenda wapi?

Nikuelimishe kidogo. Majibu ya swali hilo siyo hayo mawili tu (NDIYO na HAPANA). Ni kweli - hayo ndiyo muhimu zaidi, lakini pia yapo majibu mengine kama: SIJUI, au mwingine anakujibu INATEGEMEA, n.k. Asilimia moja (1%) iliyobaki inawasilisha majibu kama hayo
 
Hayo maoni hayawezi kuondoa msingi wenyewe. Binafsi naamini kama CDM walikaidi amri ya Polisi ni dhahiri walijiandaa kukabiliana nao, hivyo ilikuwa ni lazima wajihami. Kinachinisikitisha ni risasi hizi kuwakuta watu wengine badala ya SLAA wenyewe au MBOWE. Kwa nini watangulishe vijana kama chambo? Nimesikia SLAA anasema wanasubiri ripoti ya Daktari ili wachukue hatua za kisheria. Ni hatua gani hizo zitakazolingana na uhai wa mtu uliopotea? Nilitumai, hatua hizo wangezichukua kuzuia kifo hicho badala kuchukua hatua baada ya mtu kufa, huku ni kutaka kutupaka mafuta kwa mgongo wa chupa.

SUBIRI upakwe mafuta kwa ulimi. unadhani kuna haki inakuja bila kuitafuta? mtaka cha uvunguni sharti ainame. maana yake kila mtaka mafanikio ni sharti ajibidishe kuyatafuta. Hata ulaya na Marekani hawajafika hapo walipo kihivihivi ilikuwa ni patashika ya miaka mingi na ndio heshima na ustaarabu vikapatikana.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom