Kipigo kwa wasiotaka kushiriki mafunzo ya mgambo! TISS inakuwaje?

GAZETI

JF-Expert Member
Feb 24, 2011
5,279
6,647
Katika hali isiyokuwa ya kawaida baadhi ya wakazi wa kata ya Tandahimba wilayani Tandahimba mkoani Mtwara wamelazimika kuyatoroka kwa muda makazi yao kutokana na zoezi linaloendelea la mafunzo ya mgambo. Zoezi hili limekuwa likienda sambamba na matumizi ya nguvu na vipigo kwa wale ambao hawataki kushiriki mafunzo hayo.

Hili linatokea kukiwa na kumbukumbu mbaya ya miaka miwili iliyopita ambapo baadhi ya wanawake wa vijijini walibakwa katika operesheni ya kuwalazimisha wanakijiji kujiunga na mafunzo ya mgambo. Hata pale baadhi ya wananchi walipopeleka malalamiko yao kwa mkuu wa wilaya walifukuzwa.

TISS (TANZANIA INTELLIGENCE AND SECURITY SERVICES) Tunaandaa nini tunapompa mafunzo ya kijeshi mtu ambaye amepata vipigo na kunyanyaswa? Unaandaa nini kumpa mafunzo ya kijeshi mtu ambaye mkewe au ndugu yake kabakwa?

Si kazi yangu nende vijiji vya Mivanga na Chaume mukafanye uchunguzi juu ya matukio haya ya miaka miwili iliyopita. Nendeni Tandahimba mukajionee kile kinachofanyika.
 
Dah mkuu! niliwahi kwenda kibiashara maeneo unayoyataja Sikumbuki kama tukio lile ni la miaka miwili iliyopita naona kama mitatu vile, ni kweli hilo tukio lilinikuta nikiwa huko walihusika baadhi ya wanajeshi na mgambo. Mi nilifikiri kuna hatua zilichukuliwa kumbe ni Ruksa askari kubaka! Lakini kuna mkoa mwingine nako nilikutana na tukio kama hilo. Ndio nchi yetu hiyo tusubiri siku tu!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom