Kipigo hadi kifo kwa kumbaka mpwawe, binti wa miaka 7

X-PASTER

JF-Expert Member
Feb 12, 2007
11,619
1,799
Kipigo hadi kifo kwa kumbaka mpwawe, binti wa miaka 7

Wananchi wenye hasira wamemuua Bw. Charle Mushozi, maarufu kwa jina la Kalwani (25-30) baada ya kumfumania nyumbani kwao akimbaka mpwaye mwenye umri wa miaka saba.

Kwa mujibu wa habari zilizopatikana mjini hapa na kuthibitiswha na Kamanda wa Polisi mkoani Kagera, Bw. Henry Salewi, tukio hilo lilitokea Novemba 14, mwaka huu saa 11 alfajiri katika Kijiji cha Ibosa Kata ya Nyakato katika Wilaya ya Bukoba.

Kamanda Salewi alisema alfajiri hiyo, baba wa mtoto huyo, Bw. Wilbard Kalebe alikuwa ameondoka kwenda ziwani kuvua samaki kwa ajili ya kitoweo, na nyumbani alibaki mama mzazi wa mtoto huyo, Bi. Veronika Kalebe (38).

Ilidaiwa kuwa wakati wa tukio hilo, mama mtoto huyo alisikia makelele ya mwanawe kwenye chumba anamolala, ambapo alilazimika kuchoka mbio ili kwenda kungalia kulikoni ambapo alipofungua mlango alimkuta mdogo wake huyo wa kiume akitoka kwa kunyata akiwa ameshikilia suruali.

Kutokana na hali hiyo, Bi. Kelebe alilazimika kupiga makelele huku akimfukuza kulelekea nje ya nyumba, ndipo lilitokea kundi la wananchi ambao walianza kumshambualia huku akilia na kuomba asamehewe kutokana na kosa lilotenda.

Alisema kuwa wananachi baada ya kusikia kauli ya kijana huyo akikiri kwamba amembaka mtoto huyo, walipandwa na jazba na kuendelea kumshambulia kwa mawe na marungu hadi kufa.

Hakuna mtu anayeshikiliwa kuhusika na mauaji hayo, na mtoto aliyebakwa alikutwa ameharibiwa vibaya sehemu zake za siri.Habari zaidi katika blogu ya gazeti la Majira
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom