Kipigo cha kushtukiza: Yote maisha, tusigombane, tuangalie tumejikwaa wapi, turekebishe na maisha yaendelee!

mbingunikwetu

JF-Expert Member
Feb 17, 2015
13,651
18,021
Chonde chonde wana msimbazi wenzangu, tujiangalie na kujitathmini kwa uwazi, tusiruhusu kugombana, turekebishe na tusonge mbele!! Adui zetu tusiwape faida!! Ila tusifumbie macho udhaifu wa wazi uliopo kwenye timu yote.

Tujue tumejikwaa na kukosea wapi! Turekebishane kwa upendo na maisha yaendelee!! Anayecheka acheke sana, lakini mwisho wa siku atakayecheka mwisho atacheka sana na atakayenuna mwisho atanunà sana!

Msimu ndo unaanza, uto jiandaeni kununa sana!
 
Bora tumepigwa mapema hope udhaifu umeonekana naamini huko kombe la shirikisho wachezaji dhaifu tulio nao sitegemeei kuwaona lakin viongozi wanao uza match kesho asubuh walimwe barua mapema
 
Hapana lazima uchunguzi ufanyike, wale Galaxy wamepewa ushindi wa zawadi na wachezaji wetu wajinga wasiojitambua.
 
Jana Simba pamoja na mambo mengine walikata pumzi. Beki za kushoto na kulia zilipotea kabisa, baada ya Galaxy kucheza mpira wa kasi kipindi cha pili.
 
Hapana lazima uchunguzi ufanyike, wale Galaxy wamepewa ushindi wa zawadi na wachezaji wetu wajinga wasiojitambua.
Wachezaji wasiojitambua wale jeuri yao! Lakini uchunguzi ufanyike kwa umakini mkubwa kubaini ssbabu halisi!!
Liee fundisho pia kuhusu kuuza wachezaji bila mpangilio makini. Hatusemi wachezami wasiuzwe, lakini aliye nguzo kuu kama Chama auzwe tu kwa sharti la kwamba mchezaji mbadala aliye bora zaidi AMESHAPATIKANA TAYARI NA SIYO TUTAMTAFUTA!!.
Chama alikuwa anawawezesha na kuwachezesha wengine hivyo timu nzima ikaonekana ni bora! Mchezeshaji na mbunifu akitoka timu nzima imeonekana ni mbovu!!
Nakumbuka Makelele alipotoka Real Madrid aliacha pengo kubwa sana na timu iliyumba sana!! Viera alopotoka Arsenal timu iliyumba sana!! Kila timu huwa na mchezaji nguzo!!
 
Aisee kile kipigo kinauma, acha uchunguzi ufanyike
20211025_063620.jpg
 
Utakuwa unafanya kosa kubwa sana ukimwona Simba amenyeshewa mvua halafu ukafikiri ni paka!! Hii ni tahadhari kwa utopolo!!
 
Kwa wale wachezaji wapumbavu na ule upumbavu wao wa jana,huyo atakuwa paka tu. Tumesajili sana ‘Wavulana’ kuliko ‘Wanaume’
 
Chonde chonde wana msimbazi wenzangu, tujiangalie na kujitathmini kwa uwazi, tusiruhusu kugombana, turekebishe na tusonge mbele!! Adui zetu tusiwape faida!! Ila tusifumbie macho udhaifu wa wazi uliopo kwenye timu yote.

Tujue tumejikwaa na kukosea wapi! Turekebishane kwa upendo na maisha yaendelee!! Anayecheka acheke sana, lakini mwisho wa siku atakayecheka mwisho atacheka sana na atakayenuna mwisho atanunà sana!

Msimu ndo unaanza, uto jiandaeni kununa sana!
Kipigo kwenu lilikuwa ni suala la muda tu, timu ilishaonyesha dalili siku nyingi lakini mliendelea kushupaza shingo, Kama unatolewa na majimaji iliyochangamka unategemea nini mbele ya safari
 
Tatizo wamefanya usajiri mbovu- wachezaji wote waliosajiriwa Hakuna mwenye kiwango cha kuridhisha- na ndio maana unaona wanakaa benchi- Banda- Duncun- na Sakho wanaanzia benchi- Kanuti anacheza lakini naye kiwango chake ni hafifu sana-kipindi Cha kina Chama na Nicksoni - Morrison- Dilunga- na Bwalya hawakupata nafasi kikiosi cha kwa kwanza- Sasa hivi ndio tegemeo kwa sababu hawa wapya wamefeli- Simba walikuwa kwenye mpango wa kumsajiri Aucho - ghafra wakamuacha wakaja na kanuti- Lwanga ni mzuri akicheza double na kiungo mwenzio- na Aucho ndio pacha wake- hatukusajiri mshambuliaji- wakati tunajua hakuna washambuliaji makini- Wawa nae kachoka- Bora hata Onyango- Kapombe na Shabalala- nao tia maji tia maji- yajao yanafurahisha- ngoja tuone shirikisho- itakuaje- maana kwa uchezaji huu club bingwa huko mbele tunge-aibika tu.
 
Hakuna hata mchezaji mmoja wa Simba aliyejitokeza hadharani na kuomba radhi mashabiki. Kwenye mpira kuna kufungwa ila jana ilikua uzembe na uungwana ni kukubali makosa
 
Ni ujinga!! Kuomba rachi ilikiwa ni muhimu ili kuonesha wanajali maumivu waliyotusababishia mashabiki. Man U walipibwa 5 bila na liverpool lakini walau baadhi ya wachezaji na ko ha walijitokeza kuomba radhi!!
 
Captain John Bocco naye kakausha
 
Wachezaji wasiojitambua wale jeuri yao! Lakini uchunguzi ufanyike kwa umakini mkubwa kubaini ssbabu halisi!!
Liee fundisho pia kuhusu kuuza wachezaji bila mpangilio makini. Hatusemi wachezami wasiuzwe, lakini aliye nguzo kuu kama Chama auzwe tu kwa sharti la kwamba mchezaji mbadala aliye bora zaidi AMESHAPATIKANA TAYARI NA SIYO TUTAMTAFUTA!!.
Chama alikuwa anawawezesha na kuwachezesha wengine hivyo timu nzima ikaonekana ni bora! Mchezeshaji na mbunifu akitoka timu nzima imeonekana ni mbovu!!
Nakumbuka Makelele alipotoka Real Madrid aliacha pengo kubwa sana na timu iliyumba sana!! Viera alopotoka Arsenal timu iliyumba sana!! Kila timu huwa na mchezaji nguzo!!
aliemuleta na aliekua anamlipa mshahara ndo huyo huyo aliemuuza, wewe ni nani mpaka unahoji hivyo?
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom