Kipi umewahi kudanganywa na mpenzi wako, ikapelekea kuvunja mahusiano hayo?

EMMYGUY

JF-Expert Member
Aug 6, 2015
10,841
24,816
Habari Mkuu!

Natumaini u mzima wa afya, pole pia kwako wewe unayesumbuliwa maradhi. Naamini Mwenyezi Mungu atakuponya.

Najua mara zote katika mahusiano ya kimapenzi kuna changamoto nyingi ambazo ni lazima uzipitie, kuna zingine zinakuimarisha na kukufanya uyafurahie mahusiano hayo na zingine pia hukutoa kwenye mlengo mzuri na kukufanya uyachukie mapenzi.

Ni jambo gani uliwahi kudanganywa na mpenzi wako, katika uchunguzi wako ukabaini umedanganywa. Na vipi ulipitia maamuzi yapi? Je, ulimwambia ukweli wa kile ulichikigundua ama uliamua kuachana nae kimya kimya bila kumwambia ukweli?

Mimi, niliwahi kuambiwa kuwa yeye ni mjamzito, lakini mda ulivyozidi kwenda kama miezi mitatu nikaja kugundua kupitia rafiki zake walioniambia kuwa hana ujauzito wala nini. Kwa kipindi hicho chote alikuwa ameshabagua tayari hata baadhi ya vyakula na hata pafyumu na hata matunda pia.

Nilijaribu kuangalia gharama nilizotumia kwake kwa mda alioniambia kuwa ni mjamzito, zilikuwa ni kubwa. Ikanibidi nifanye maamuzi, siku hiyo sikuwa nimeenda kazini nikaamua kumuitisha ndani na kumwambia ukweli na kuanzia siku hiyo nikavunja mahusiano yale.

Vipi kwako, ji kipi uliwahi kudanganywa na mpenzi wako?
 
Hii yote ni kutokana na kufanya mapenzi kabla ya ndoa. NO SEXY BEFORE MARRIAGE
Asilimia kubwa ni wengi wanaoingia mahusiano kabla ya ndoa, na ndizo ndoa zinazokuja kudumu kuliko zile za hadi waoane.
 
Back
Top Bottom