Wapendwa kwema,
Leo nimeletewa malalamiko kwenye ndoa yangu kuwa mke wangu anachonganisha watu hadi wamekosana.
Basi mimi sio wa maneno sana nikamuomba yaishe wamsameheane. Huyo mtu akawa amenielewa.
Baada ya kama ya dakika kumi nikasikia tena watu wana purukushani za kupigana na isitoshe mke wangu ni mjamzito. Nikawaachanisha kisha nikawapeleka ndani wote ili nizungumze nao. Basi nikaongea yakaisha ila nikaona ni maneno ya vibarazani.
Hadi sasa hivi nimekaa wala sijamuuliza mke wangu ilikuwaje namwangalia tu kama vile hajafanya tatizo na kicheko tu.
Sasa hivi ananichokoza niongee lakini niko kimya sana, sitaki niongee.
Hebu mnipe uzoefu wenu, kwenye kesi za hivi huwa mnafanyaje jamani?