Kipi ni Kiswahili bora hapa kwani huwa vinatuchanganya sana tuwapo misibani!

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,544
108,865
Kuna Watu huwa wakiwa misibani hupenda kusema moja wapo ya neno hili kwa lugha yetu adhimu ya Kiswahili ambapo Kiukweli Mimi ambaye ni Mgeni hapa nchini Tanzania huwa nashindwa kujua nilishike lipi na mwishowe nabaki tu kuchanganyika.

Utamsikia Mtu wa Kwanza akisema nanukuu " Nimefiliwa na Ndugu yangu bhana... "

mara

Utamsikia Mtu mwingine akisema nanukuu " Nimefiwa na Ndugu yangu bhana... "

Mnaojua Kiswahili je hapa tushike lipi? Kufiliwa au Kufiwa?

Nitawashukuruni sana Watanzania wenye Kiswahili chenu mkinipa ufafanuzi wa hayo maneno ya Kiswahili ili nami nizidi Kubobea katika Kiswahili na taratibu nianze kukisahau Kinyarwanda na Kipuerto Rico changu.

Nawasilisha.
 
Naongezea tu
anayejua tofauti kati ya marehemu na hayati pia atusaidie

_ where ever you are remember me_

 
Hiyo kufiliwa SIJAWAHI KUISIKIA HATA SIKU MOJA.

Sent from my Priceless H40-D00 using JamiiForums mobile app
 
Kufiliwa looooh hamna msamiati kama huo ktk kamusi mkuu bali msamiati sahihi ni KUFIWA
 
nimekuwa nikisikia Wakenya hasa ndo wakitumia 'kufiliwa' ila WaTz wengi ni watumiaji wa 'kufiwa'
 
Hiyo kufiliwa ndio leo naisikia, na ninaomba uendelee kufiliwa tuu, wakufilie mpaka uchoke
 
Kufiliwa ni neno linalotokana na matumizi ya neno hilo kuonesha mtu kaondokewa na mtu wake wa karibu, wakati kufiwa hutumika hasa kwa kuonesha mtu mwingine. Juma kafiwa na baba yake. Pia kufiliwa ni watu wa Pwani ya Kenya ndiyo hutumia zaidi neno hilo!
 
Back
Top Bottom