Kipi ni kigezo muafaka kwa Mwanaume kuoa, Je Ni umri, kipato au upendo wa dhati?

PNU

JF-Expert Member
Jun 19, 2020
377
2,807
Kumekuwa na mvutano wa nafsi kati yetu wanaume, wengine kuoa kwa kufuata mkumbo, wengine kuoa kwa kuwa ana kipato kizuri, wengine kuoa kwa kuwa anaona umri unakimbia na mwengine kuoa kwa kuwa amefanikiwa kumpata yule wanaopendana, Je ni nini asa kigezo muhimu kwa mwanaume ili aweze kuchukua maamuzi ya kuoa??
 
Kuoa sio muhimu,Fanya yaliyo na umuhimu kwenye maisha ya ki leo.

Kuoa ni kumfaidisha mwanamke.

Yapi hayo yenye umuhimu zaidi kwenye maisha ya kileo kushinda kuwa na familia yako?
 
Yapi hayo yenye umuhimu zaidi kwenye maisha ya kileo kushinda kuwa na familia yako?
Kwani kuwa na familia mpaka uoe?

Tengeneza mkwanja ndugu yangu.Acha kutafuta stress za kujitakia.
 
Kigezo mhimu kwangu cha kuoa ni ukamilifu walau wa 75% ya utafutaji wako kufikia lengo,ila ndoa nyingi zimetokana na mashinikizo ya wanawake,kumganda mwanamme kwa kila namna,mimba za mitego na nk.
 
Nahisi kuoa ni kama hisia na utayar ukijiona uko poa unaoa tu sio lazima
 
Kumekuwa na mvutano wa nafsi kati yetu wanaume, wengine kuoa kwa kufuata mkumbo, wengine kuoa kwa kuwa ana kipato kizuri, wengine kuoa kwa kuwa anaona umri unakimbia na mwengine kuoa kwa kuwa amefanikiwa kumpata yule wanaopendana, Je ni nini asa kigezo muhimu kwa mwanaume ili aweze kuchukua maamuzi ya kuoa??
inategemea ntu na ntu, hakuna vigezo uniform kwa wote
 
Me kwakweli sasa nipo serious natafuta mwenzangu wa kuishi naye.

1.Nitampenda
2.Nitamheshimu
3.etc
 
Back
Top Bottom