Siri ya sifuri
JF-Expert Member
- Sep 21, 2018
- 2,014
- 1,498
Habari wakuu!? Leo nimekumbuka swali la miaka mingi na ambalo halijapatiwa jibu lenye kukubalika kwa wote, Mara zote linapoulizwa kumekua na majibu yasiyolandana hivyo kuendelea kua swali tata lisilo na jibu, nashawishika kulileta kwenu wana Jf nikiamini ni jamii pana yenye wasomi,wataalam na wajuvi wa masuala mengi zaidi. binafsi naamini pesa ni bora zaidi ya elimu, kwa maana elimu inatumika kama nyenzo muhimu ya kutafutia pesa kwa urahisi,kuzipata, kuziendeleza,kuzidhibiti ili zisikupotee kiurahisi, pia kwa mtazamo wangu ni kwamba, kwa MTU mwenye afya njema hii ni pamoja na ufahamu wa kuzaliwa, kuishi bila elimu inawezekana ila kuishi bila pesa ni majanga.