Ndege Tausi
JF-Expert Member
- Nov 12, 2013
- 992
- 472
Naunga mkono hoja hii ya ku adopt badala ya kulea mtotot wa ndugu. Kulea mtoto wa ndugu ni kazi sana, mtoto bado ataendelea kukuona wewe sio mzazi wake hata ukimuwezesha kupata mafanikio bado atakwenda kuwasaidia zaidi wazazi wake kuliko wewe. Na mara zote wazazi wa mtoto unayemlea huwa hawaamini kuwa unamlea vizuri mtoto.Ni jambo jema kufikiria hivyo na kuwa na plan B, na ni lipi bora hasa mtoto wa ndugu au adoption, option zote inategemea matokeo unayoyatarajia kutokana na maamuzi yako
1.Ukiwa unataka tu kulea na kusaidia ndugu wanaweza kuwa option nzuri, ingawa option hii inachangamoto ya kuingiliwa na familia husika ya ndugu, na ukiwa na ndugu wa lawama inaeeza kukuweka ktk mazingira magumu( Nimeongea kwa kuzingazia evidence nilizoziona), hii option huwa naiona ni nzuri ukiwa na mtoto mmoja au wawili then ukawa na ndugu wa kusaidia, ila tegemea mtoto anaweza kuondolewa ktk familia yako muda wowote.
2.Option ya kuadopt binafsi naiona nzuri zaidi, kwanza unampa fursa mtoto ambaye angeweza kukulia ktk vituo vya watoto yatima ambavyo sio mazingira rafiki sana ya makuzi, pili unapata fursa ya kumlea kulingana na mnavyoona inafaa, kwa namna yenu na imani yenu, na huyu mtoto mtakuwa naye maisha yenu yote tofauti na ndugu.
Changamoto za kuingiliwa ktk malezi hazipo, na mtoto anakuwa akitambua kuwa nyie ndio wazazi wake.
Kwangu hii ni better option