Jane Msowoya
JF-Expert Member
- Aug 20, 2017
- 4,046
- 7,118
AKwa kuzingatia hoja yako tuchukulie mfano huu kati ya watu hawa wawili A na B , A alisema "kazi hii nimeifanya kwa masaa 10 imenichosha Bora niende nyumbani nikafanye usafi wa nyumba nzima" mwenzie B kwa kutumia mantiki ya "uchovu" aliona mwenzie ameongea jambo linalo pishana na mantiki hiyo.
Upande wa pili ulikuwa hivi, kazi aliyokuwa akiifanya ni kukokotoa hesabu za gawio la wanahisa wa kampuni yao hivyo alikaa kwa muda mrefu na kuuchosha ubongo, alihitaji kufanya aina nyingine ya kazi ili kuupumzisha ubongo kwa kufanya kazi za nguvu na kutembea tembea.
Moja ya tafiti inasema kufikiri kimantiki ni mchakato wa kuwa uwezo wa kumbukumbu za matukio ya muda mfupi Kisha kuzihusanisha na matokea ya matukio ya baadae.
Kwa mfano huo B hakuona kwa hidden logic ya A kwamba angeweza kuupumzisha ubongo kwa kazi za usafi, hii inamaana hakufikiria tukio la muda mfupi (ukokotoaji) la mwenzie kabla ya kushangaa fikira za mwenzie.
A na B Nani alikuwa sahihi?
Sent using Jamii Forums mobile app