kipi naweza kuweka kama maonesho ya international day chuoni kwangu

biarakeyz

Senior Member
Jan 19, 2016
183
46
habarini wakuu,
mimi ni mtanzania,niishie nje ya nchi,uwa kila mwaka katika chuo nisomacho tunatamaduni ya kuandaa siku ya maonesho,na siku hii uitwa international day.lakini katika chuo iki niko peke angu,ivo nilikua naomba msaada wa mawazo yenu kipi naweza weka kama mtanzania katika maonesho ayo,kitu icho nilazima kiwe kinausiana na tamaduni ya nchi yako
 
Je, wenzako wanaweka nini kama Identity ya mataifa yao?

Chukua Bendera ya taifa letu, chomeka kwenye kimti, kisha iache ipepee huku unasakata singeli kwa pembeni na picha ya Msaga Sumu au Man Fongo, hakika utatutambulisha kimataifa.

Feel the difference.
 
hahaha nimeipenda iyo mkuu,bendera nisha ipata nilienda kuiomba kwa bolozi wetu nchini apa
 
mimi ningebase kwenye misosi tu
moja
mapishi ya kongoro
waoneshe jinsi ya kutengeneza kongoro
tafuta miguu ya mbuzi ya kutosha kama mia hivi , tafuta chungu kikuuubwa na jiko chemsha mdogo mdogo
mbili
vichwa vya kuku na utumbo wake
na chips mayai
nadhani banda lako litakuwa halina nafasi
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom