Kipi kinawatofautisha watu hawa? Edward Lowassa, Samwel Sitta na Ben Membe

KAUMZA

JF-Expert Member
Aug 31, 2010
699
237
Haya ni mawazo yangu tu wanajamii!!

Inawezekana wakawepo wengi tu katika CCM wanaoutolea mate urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baada ya JK. Miongoni mwao ni Edward Lowassa, Samwel Sitta na Ben Membe. Kwa nyakati tofauti wamekuwa wakitoa kauli zinazoonesha nia yao hiyo.

Katika mihadhara yao wanayoifanya aidha kwa kuitwa au wao wenyewe kuita watu wamekuwa wakiongelea mambo mengi yanayohusu mustakabali wa Taifa letu.

Lakini unapochaambua sana mambo ambayo huwa wanayaongelea utabaini kuwa Edward Lowassa amewazidi sana wanasiasa wenzake wa CCM(Kwa muktadha wa uchambuzi huu Samweli Sitta na Ben Membe)

Kwa upande wa Lowassa kila anapopata nafasi ya kuongea na wananchi amekuwa akionesha uwezo mkubwa wa kubuni na kutanabaisha njia ya nini kifanyike katika kulijenga Taifa(Sijui kama anachokisema kinatoka moyoni au lengo ni kupata populality), ila kwa kuwa waswahili wanasema kimtokacho mtu mdomoni ndicho kilichopo moyoni hatuna budi kuamini kuwa anayoyasemaa Lowassa ndiyo yaliyopo moyoni mwake.

Lowassa mara kwa mara amekuwa akiongelea suala la ajira kwa vijana na alifika mbali hata kuyaomba mashirika ya dini na ya binafsi kuanza kujenga shule na vyuo vya ufundi ambavyo vitawafundisha vijana fani mbalimbali ambapo mara baada ya kuhitimu wanaweza kujiajiri wenyewe kama siyo kuajiriwa.

Lowassa pia amekuwa akisisitiza suala la elimu bora. Amewahi kuongelea kuhusu kuundwa kwa tume ambayo itafanya uchambuzi wa mfumo wa elimu kama unaendana na mazingira ya sasa na kama itabainika kuwa hauendanibasi mfumo huo ufumuliwe na kusukwa upya(Haya aliyasema katika mahafali ya shule ya Benjamini Mkapa, Dar)

Lowassa akiwa katika harambee ya kuchangia Saccos ya walimu mjini Moshi ameelezea kuwa anayo ndoto kuwa siku moja Elimu kwa watoto wa kitanzania itakuwa bora na maisha yaa mwalimu yatakuwa bora. Na hapa nahusianisha na kauli mbiu yake Kilimo kwanza, Elimu kabla. Akiwa na maana, kama kilimo ni chapter one, basi elimu ni Preamble.

Lakini pia Lowassa amekuwa akikwepa sana kulumbana na wanasiasa wa ndani ya chama chake na hata nje ya chama chake(achilia mbali kauli katika majukwaa ya siasa). Sijawahi kumsikia Lowassa akiwatupia vijembe wapinzani wake (wa ndani ya chama chake au nje ya chama chake) kuwa hawastahili kuwa viongozi.

Kwa upande wa Samweli Sitta na Ben Membe, wamekuwa wakiongelea kero za wananchi kwa kiwango kidogo sana hata kuwa vigumu kujua wamesimamia wapi. Kila wanapopata upenyo wamekuwa wakilalamika na kurusha matope na kejeli kwa mahasimu wao wa kisiasa. Kila Sitta atakapoalikwa au atakapoalika watu ataongelea suala la uchaguzi wa 2015 na alivyotendwa kwa kunyang'anywa uspika wake. Muda wote utamsikia "mimi nimefanya kazi na Nyerere. Msifanye makosa mkampa kura mtu ambaye si muadilifu".

Membe pia wimbo ni huo huo. Hawaoneshi ubunifu wa namna ya kutatua matatizo ya watanzania ili tuweze kuwapa credity. Kama hawatamsema Lowassa katika namna ya mafumbo(wanasheria wanaita innuendo) basi wataingia katika malumbano yasiyo na maana na watani wao wa Chadema.

Kwa haya machache naamini Lowassa yupo mbele ya Samweli Sitta na Ben Membe kwa zaidi ya maili nyingi sana.

Wasalaam
 
You are dead right. Kwenye uchaguzi wowote mtu akibaki kuonya tu kwamba msimchague yule, huku yule anayasema tu yale atakayofanya akichaguliwa, basi wa kwanza keshashindwa kabla ya uchaguzi. Don't discuss people, discuss issues.
 
Sita na Membe ni watu wa visasi na wapo kambi moja na Mwigulu na Nape, Mh Lowasa ni mtu mwenye busara na hana mambo ya visasi
 
Masahihisho; Mzee Edward Ngoyai Lowassa anatarajiwa kushinda ( sio kugombea) kiti cha Urais wa jamhuri ya Watu wa Tanganyika ( sio Tanzania).pia sifa ya kufananisha huwa ni kwa vitu vinavolingana, kuwalinganisha kina Membe na MZEE WETU ni kutokuitendea haki Tanganyika na watu wake, ni sawa na kufananisha Msitu wa Mabwepande na Msitu wa Amazon!
 
je wameusika vipi Na ufisadi kuifisadia nchi. Kwa visasi hao wote wanausika. Kila mmoja amefanya lake na yapo yanaoneka. Kwani nyie CCm hakuna wagombea wengine zaidi ya hao ?
 
Wapiga DEBE naona mpo MAKINI kupata poshp nene..hongera zenu na ushabiki..no more sisiem president.
 
Hakuna tofauti kati ya Membe, Sitta na Lowassa katika uadilifu wakisiasa, kwa kuwa wote hao ni wanafiki wakubwa, matapeli wa kisiasa na waongo wakubwa kwa sababu:

1/Wote ni wanaCCM tena wanachama waandamizi wa ngazi za juu za Chama kwa miaka zaidi ya 25 (Wamehusika katika.kuiua CCM na misingi yake ya utu na uadilifu)

2/Wote ni wanamtandao wa Kikwete(walikuwa ndani ya mtandao wa JK 2005 na wakahakikisha wanafanikisha mipango yao wakitumia Pesa, Fitna na Uongo)

3/Wote ni mafisadi wakubwa hapa nchini (Kila mmoja kwa nafasi yake ametumia kuifisadi hii nchi)

4/Wote wametumwa na Kikwete ili wamrithi Kikwete atakamaliza kipindi chake cha urais.

5/Wote wanatumia nyumba za Ibada hususani makanisa kujipatia uungwaji mkono(Kwa taarifa tu Kesho Benard Mengi atakuwa Moshi mjini kwenye kanisa moja kwa ajili ya uzinduzi wa kwaya na harambee)
 
Hakuna msafi hapo,jiulize kwa nini kipindi hiki wameona mahala pa kusemea ni kanisani wakatiwa kuchangisha harambee? Miaka 4 iliyopita walifanya hivyo?

UKIMUONA NYANI MJINI UJUE KAFUGWA!!!
 
Ukweli tukiwa makini na kuwa wakweli wa dhati, katika hao hakuna rais hapo! Ni lini Tanzania tuipendayo itapata raisi mwenye nia ya kuendeleza watanzania badala ya kujinufaisha binafsi? Mwalimu alisema ikulu ni mzigo, mnakimbilia nini huko? Wanaokimbilia waogopeni kama ukoma! Tunawaogopa hasa mnaotumia mapesa mengi kuingia ikulu, mtayarudishaje Kama sio kupora uchumi wa taifa hili changa? Na mnayomwaga ovyo mnayatoa wapi wakati wengi wanazidi kuwa maskini? Mfereji mnaochota kwa nini msituonyeshe tuchote wote kama mna mapenzi ya dhati na raia wa nchi hii?
 
kigezo Mwalimu alisema hakina nguvu ila kinatumiwa na watu wenye upungufu wa hoja na watumwa wa fikra.. Huwezi kusema CCM mbaya na Mwalimu mzuri ni unafiki na umbumbu au woga, mwalimu kaongoza miaka 23 na 5 ya mwanzo ya Mwinyi alipokuwa mwenyekit wa chama kwani alikuwa akimwagiza Mwinyi lipi afanye na asifanye so Nyerere kaongoza taifa hili miaka 23 na ndo uongozi wake ulioweka msingi wa taifa hili so lawama na sifa za hapa tulipo yeye ni wa kwanza kusifiwa na kulaumiwa.

Pil,Mwalimu kusema kuhusu Ikulu ni mzigo ni maoni yake kama mzigo aliwezeje yeye kukaa miaka 23, si angewachia wenzie waliokuwa na uwezo pia kama Oscar Kambona na wengine, sioni jipya mwalimu alikuwa kama mimi na wew ila yapo ya muhmu aliyoyafanya kama wengine ambao hatuwakumbukia kama Sokoine, Mrema, Kawawa nao walifanya mengi kwa taifa hil si mwalimu pekee hakuwa malaika au Nabii.

Tatu, Lowassa ni bora kila nyanja na hata hali yake ya uchumi ni kutokana na uwezo wake kwani hata me nafanya kazi serikalin ila mke wangu anafanya biashara na tunatumia fursa na kujinyima pia kesho nikifanikiwa wataibuka watu wa haiba ya Sitta na Membe ambao wana akili fupi na maneno huyu mwizi,fisadi na pengine freemason ila wakati natafuta nyie mpo busy clubing na kubadilisha skirt na kuweka heshima bar. binadamu kama vidole na utajiri ni kujituma na si vinginevyo, Lowassa anajituma kwa umma na hata mambo binafsi husikii mwanaye na matukio ya ajabu kama wengine ama wakiwa na vyeo kwenye ofisi za umma kama wengine ni wa tofauti.. 2015 viva Lowassa
 
You are dead right. Kwenye uchaguzi wowote mtu akibaki kuonya tu kwamba msimchague yule, huku yule anayasema tu yale atakayofanya akichaguliwa, basi wa kwanza keshashindwa kabla ya uchaguzi. Don't discuss people, discuss issues.
And what are we doing here, discussing people or issues?
 
Watajwa wote hapo wanatofautiana kwa nyanja nyingi lakini wanaunganishwa na CCM hivyo kuwaondelea utofauti.
Tunahitajika kujikomboa kifikra ili kuondokana na mawazo mgando kuwa lazima wagombea watoke CCM.
Kuna Watanzania wenye uwezo na sifa lakini tumejikita kuwa jadili watu ambao hawawezi kuiokoa nchi hii katika kipindi kama hiki.
Tutumie milango yote ya fahamu, kujifungua toka minyororo ya fikra finyu na tutazame mbele juu ya mstakabali wa nchi yetu kwa mapana tuone watu wanaoweza kuikomboa nchi hii na ikiwezekana tuwaombe waiongeze nchi,kuliko hao ambao wanandoto ya kuitawala nchi kwa lengo la kuneemesha jamii zao na kuiacha nchi taabani.
Kwa vipindi walivyotumikia nchi hii maisha ya watanzania baada ya miaka 50 ya uhuru bado yapo duni na hii ni kutokana na mchango wao kwa vipindi wakiwa kwenye madaraka makubwa.Wamechangia nini?
Ni busara wakae pembeni wastaafu na kuwaachie wengine wapate nafasi ya kuiokoa nchi hii mahali walipofikisha.
 
Mh.Lowassa is the best ukimya wake ni hekima kutoka kwa mungu.
Naamini ni tumani pekee lililobaki ccm.
 
ndugu yangu huyo ni mwanasiasa hao wengine ni wababaishaji tuu wanataka kuihujumu nchii.
 
Back
Top Bottom